Wakristo tujitafakari upya taratibu zetu zote za mazishi. Kuna mambo hayako sawa

Hilo dogo .. kubwa kuliko ni ile ya kutokumzika aka taratibu za kanisa yule asiyefata taratibu mfano mwenye wake wawili... kapuku atafukiwa kama mzoga wa mbwa lakini kigogo mpaka askofu atakwepo ref. captain Komba
 
Navyoelewa, kwa Wakatoliki, kanisa la mahali fulani linaruhusu mapadre, au maaskofu wa maeneo tofauti na pale kuja kumzika mtu fulani ambaye alikuwa rafiki yao. Wakati mwingine, kama marehemu ni mtu kwenye ukoo wa padre fulani, huyo padre anaweza akawaita mapadre wengine hata zaidi ya kumi, na hata maaskofu waungane naye kwenye hiyo ibada. Kwa hiyo, usishangae maaskofu wa kusini ambao walikuwa ni marafiki wa marehemu wakija kuendesha ibada ya mazishi yake.

Sioni tatizo kwa maaskofu au mapdre ambao ni marafiki wa marehemu kuendesha ibada ya mazishi yake. Kwani, wewe hutaki siku ukifa marafiki zako wahudhurie mazishi yako?
 
Mambo ya Mwenyezi Mungu yamepokwa na mwanaadamu dhalili aliyeumbwa kwa manii.ndiyo maana yana maswali mengi kuliko majibu
 
Waje kama watu wengine. Kwani padre mmoja hatoshi kuendesha misa?
 
Mwenye kustahili heshima na apewe heshima.
 
Pengo ameshastaafu
 
Kwa waislamu utaratibu ukoje?
 
Hakuna tatizo, wala usisononeke haya yote ni mambo ya kibinaadamu.

Tunayo madaraja katika maisha yetu ya kila siku hata mipango ya mazishi nyumba kwa nyumba tunatofautiana, makaburi nayo yanatofautiaana hata majeneza.

Aina ya chakula na mipangilio yake inatofautiana, misiba ya viongozi wetu jiulize kwann wao ni viongozi wakati sote ni binadaam? Hata wale wenye utaratibu wa kuzika haraka kwa maelekezo ya kitabu chao bado kwa kiongozi taratibu zinabadirika.
 
Hahahahaha duh...
 

Ni maamuzi ya baraza la maaskofu kulingana na hadhi ya Marehemu hakuwa Raisi wa Dar alikuwa ni Rais wa nchi
 
Wewe Rais sio sawa na wewe japo wote NI binadamu stop this nonsense!!
 
Sasa askofu hata akiongoza misa ya kapuku we utajuaje mana misiba ya watu ambao si maarufu huwa haioneshwi live kwny TV so kwangu mimi hoja yako haijakaa sawa mana hakuna ushaidi usioacha shaka kuwa hakuna kapuku aliyesaliwa na askofu
Hata mimi babu yangu ibada ya mazishi yake ilifanywa na maaskofu wawili ilitokea tu maaskofu hao walikuwa kijijini kwetu kwa shughuli zao kutambulishwa
 
Maaskofu nao wamekuja kutoa heshima zao za mwisho, Kwahiyo wakishiriki kwenye misa sio dhambi
 
Mkuu usipotoshe uma Kama huna taarifa sahihi kukaa kimya ni busara.
Mhashamu baba Askofu Ngalalekumtwa ni Askofu wa Iringa. (Rais mstaafu wa TEC)
Rais wa TEC ni Askofu Gervas Nyaisonga.
Hakuna cha kujitafakali maana ukiona Askofu anasalisha huyo mtu ni level yake,jitaidi na wewe kabla hujafa ufanye jambo ambalo Taifa litaguswa nalo,wewe ukae tu mashambani uko kisha unataka ukifa Askofu aje kukuzika.
 
Hilo dogo .. kubwa kuliko ni ile ya kutokumzika aka taratibu za kanisa yule asiyefata taratibu mfano mwenye wake wawili... kapuku atafukiwa kama mzoga wa mbwa lakini kigogo mpaka askofu atakwepo ref. captain Komba
MBONA YULE TAJIRI MREMA WA HOTEL ZA NGURDOTO, IMPALA NA KIBO PALACE. HAKUZIKWA NA PADRI NA ALIKUA NA PESA ZAKE ZA KUTOSHA? HALAFI MNAPASWA MJUE RATIBA YA MAASKOFU NI NGUMU KIDOGO HAWAPATIKANI KIRAHISI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…