Wakristo: Vita ya Israel inayoendelea ni ishara tosha kuwa wakati wa kuja kwake mwana wa Adamu (YESU) umekaribia. Tuamke

Vitabu vyenu vya dini vi.ewatia ujinga akili zimepotea. Heri utumwa wa kufungwa minyiroro kuliko utumwa wa kidini ambao utumwa wa kifikra.
 
Upumbavu mtupu aliyekaa na kuandika hili bandiko ni wa kupigwa makofi

Mavi matupu!!!
 
Sio kwamba ni ishara nzuri kuwa Hakuna Mungu!?
 
Ukristo wako unapotosha maandiko KABISAAAAA.
1. Utakatifu wa Taifa la Israeli ni upi?
2. Mungu analitunia Taifa hili kwa jambo gani?
3. Je wewe unamwani Yesu kuwa ni Masihi na Mwokozi ? Na je Israeli inamwamini kama nani?

Hebu soma maneno haya halafu useme yalikuwa yanamaanisha nini?
Daniel 9:23-27
"27 Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu.
Danieli 9:27

37 Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii, na kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwako! Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hamkutaka!

38 Angalieni, nyumba yenu mmeachiwa hali ya ukiwa.
Mathayo 23:37-38

Acha kujidanganya Iseaeli ni taifa sawa na Congo au Japan wote ni sawa machoni pa Mungu .
Wote tunaokolewa kwa Neema ya Yesu wao ni sawa na palestina tu.
Wao walipewe jukumu la kumtanga Mungu na ujio wa Masihi Yesu, walipewa mausia ya Mungu wayafundishe , wakipewa taurati ili iwafikie mataifa yote tena manabii wengi walitoka kwao ,LAKINI walikataa.

Imeandikwa hivi
"
3 Kwa maana ningeweza kuomba mimi mwenyewe niharimishwe na kutengwa na Kristo kwa ajili ya ndugu zangu, jamaa zangu kwa jinsi ya mwili;
4 ambao ni Waisraeli, wenye kule kufanywa wana, na ule utukufu, na maagano, na kupewa torati, na ibada ya Mungu, na ahadi zake;
5 ambao mababu ni wao, na katika hao alitoka Kristo kwa jinsi ya mwili. Ndiye aliye juu ya mambo yote, Mungu, mwenye kuhimidiwa milele. Amina.
Warumi 9:3-5

Soma vizuri imani yako ikishaanza kubagua na kuwainua wengine kuwa bora kuliko wengine hiyo haitokani na Mungu. Isareli ataokolewa kwa taraja ikiwa atachagua, hata hivyo Mungu amejibakizia masalio katika Israeli ambao wewe umepandikizwa kama mzabibu pori
 
Vitabu vyenu vya dini vi.ewatia ujinga akili zimepotea. Heri utumwa wa kufungwa minyiroro kuliko utumwa wa kidini ambao utumwa wa kifikra.
Ni Mawazo yako.
Ambaye hamtumikii Mungu ndiye mtumwa, na siku zote mtumwa hutumikishwa.

Kwaiyo najua siyo wewe ila ni shetani anakutumikisha, Nakuombea hiyo Roho ikutoke katika Jina la Yesu Kristo.
 
Kwanza Elewa hamna sehemu ambayo nimesema Kuwa Israel ni WAKIRSTO na Sijasema Kuwa naitetea Israel.
Daniel alikua anatoa unabii juu watu ambao walikua wakifanya uovu na kuwaua watumishi wa Mungu (Manabii) hapa anaizungmzia Israel.

Lakin kama mwanzo nilivyo Kuambia Kuwa Israel siyo wakristo na hata Yesu alipo kuja Duniani Wala hakumuamini kwa n mwana wa Mungu Bali wao waliendelea na torati yao kwaiyo Yesu walimkataa na mpaka Leo hawamkubali, ila ile siku Yesu atakapo rudi baada ya Israel kupigwa kwenye vita ile ya Masinagogi atawasaidia wa Israel hapo ndo wataanza kumwamini na kumkiri Kuwa MWOKOZI. Pia Utambue kua kupitia hili Taifa Mungu ana watu wake na ni aridhi yake hiyo kutaka kujua watu wake alio jitwalia katka Taifa la Israel soma Ufunuo 7:1.......

Hapa watu wengi wanashindwa kuelewa Kuwa siyo wote Waliopo Israel ni WA Israel au ni wateule wa Mungu not true ni Kama Tz siyo wote waliopo Tz ni watanzania huwez kuja na Statement hiyo Alfu utoe Judgement kua Israel siyo Taifa la Mungu. Siyo Kweli.
 
Hadithi za abunuwasi...😂😅😆😹🤣😸🤭
Ipo siku hizi Hadithi zitakua kweli.

Hakika kitakua kilio Cha Kusaga Meno kwa wale ambao walikua hawamini.
Nakusihi Ndugu yangu badilika Leo Umkiri Yesu awe BWANA na MWOKOZI katika maisha yako.
 
Well Said.
But turudi Nyuma Kidogo Mkuu wakati Mungu akiangamiza wanadamu kwa gharika ya Maji Kipindi kile Cha Nuhu, watu wengi wa aina kama yako walikuwepo wengi sana, tena Wakawa wanajisahau sana yani kama unaenda kumwambia Mtu Kuwa Ipo siku Mungu ataleta gharika ya Maji na Kila Mtu atakufa, njoon tujenge Safina hakika hakuna aliekubali, waliona Nuhu anawatania and is Wrong prediction. Huku uswahilini wanasema ni sawa na kumpigia Mbuzi Kinanda ukitegemea acheze. End of day Mungu anakuja anawangamiza watu kwa Gharika.

turudi kwenye hoja yako ni kweli inaweza Kuwa ngumu sana hili kuaminika kwa watu, lakin haiwez ondoa ukweli kua hilo Tukio linakuja na litatokea, Dunia Kuwa Kubwa siyo Kigezo Kuwa Yesu hawez Kuja, nikwambie tu pamoja na wewe kusema Dunia hii ni kubwa lakin utambue Kuwa Injili inahubiriwa Kila siku na inafika na Kupenya Kila sehemu ni kama vile ww ukiwa na smartphone unaingia Mtandaoni unapata habari za Dunia ndo hivyo hivyo kwa Injili inasambaa Duniani.

Wewe kUhusu kumjua au kutomjua Yesu haiwez Zuia Yesu asije Duniani Big No, haya Mambo Mkuu yanaendaje Kiimani na Kiroho Zaidi ukiishi kwa Imani ya kumwamini Yesu na kumwabudu katka Roho ya kweli Basi amini ipo Siku atakutokea na utamuona.

Mkuu nakusihi sana Mgeukie Yesu awe Njia katika maisha yako.

Siku zote Uongo huwa haudumu ila Ukweli hubaki milele amini Ipo siku Yesu atakuja Dunian na Ishara za Kuja kwake tayari zishaonekana anasema "Myaonapo hayo basi kesheni Mliomba maana ule wakati wa Kuja mwana wa Adamu umekaribia"

Ubarikiwe Mkuu.
 
Sijasoma ila najua ni pumba tu za mtu mweusi na viimani vinavyowafanya kuwa masikini wa kutupwa kwa kushikiwa akili na wajanja waliowaletea hizi ngano za kusadikika ili wawatawale....
Ndo Africa tunasumbuliwa na huu Ujinga Sijasoma alafu hapo hapo unatoa Judgement Huku ukiwa hujasoma kilicho andikwa kwa hakika una shida mkuu.
soma kwanza ndo utoe Judgement
 
Ufunuo 22:11-12

Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu;na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu;na mwenye haki na azidi kufanya haki;na mtakatifu na azidi kutakaswa.Tazama naja upesi,na ujira wangu u pamoja nami,kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.
 
Babubyangu kamsubiri huyo yesu toka utotoni mpaka Ana dead akiwa na 103 years na alikuwa anaongea hivyo hivyo dunia iko mwisho mpaka kaisha yeye

Ila nyie wachungaji nyinyi mna bahati Sana Sheria inawa jua
 
Ufunuo 22:11-12

Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu;na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu;na mwenye haki na azidi kufanya haki;na mtakatifu na azidi kutakaswa.Tazama naja upesi,na ujira wangu u pamoja nami,kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.
Amina Mkuu be Blessed
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…