Wakurugenzi wa TISS tangu uhuru mpaka sasa. Mzee Mzena ashikilia rekodi ya kuhudumu muda mrefu zaidi

Siku hizi tunapandishiwa bei ya sukari, mafuta na umeme Hawa jamaa wapo tu kinyonge,

Tumepambania bandari isichukuliwa wapo kimya na wameshiriki kuandaa kesi ya uhaini

Tulipojitoa kumpigania katiba mpya walihusika kutuandalia kesi za ugaidi

Kiufupi Hawa jamaa ndo wanahujumu nchi
 
Makalla?
Mkuu huko umekwenda mbali.
Hebu taja mwingine.
Steve Nyerere, Mama anamkubali sana huyu dogo kiboko ya Mama Wema Sepetu. Dogo anarekodi mazungumzo nyeti ya watu toka akiwa mtoto kisha anauza baa siri zao na kukuza jina huku akipewa offer za bure.
 
Kwa kweli usalama wa taifa kwa sasa ni kama wametekwa na Ccm hawana habari ya kutetea maslahi ya taifa kama ambavyo wamelala. Wako tayari kutetea maslahi ya viongozi na maslahi yao ndiyo maana mama Abdul anawabadilisha awezavyo.

Issue ya DPW, Loliondo na maeneo mengine, lakini pia ufisadi na hizi wa rasilimali za umma ulivyokithiri unatia shaka sana kuamini Luna chombo madhubuti kilichoapa kulitetea taifa na rasilimali zake.

Ndiyo maana akijitokeza mkosoaji wa kukemea na kutaka rasilimali za nchi zisigawiwe kama njugu wako tayari kukuvunja taya na kukutelekeza uliwe na wanyama wakali.

Na sijui lini usalama utarudi kwenye viwango vyake.
 
Kanali Apson Cornel Mwang'onda. Nimekuta hii identity ktk Salam za rambi rambi
Mzee Apson hakuwahi kuwa mwanajeshi.

Watanzania kwa kuchanganya madesa huwajui?

Majuzi hapa kwenye kurasa za polisi wanaandika mtu kakamatwa kwa kutembea na gari isiyo na "plate number" kiuhalisia neno stahiki ni NUMBER PLATE na sio PLATE NUMBER.
 

Kuna aliyehudumu kwa mwaka mmoja au miezi kadhaa. Huko aliko anaweza kuwa anashangaa kama mimi ninavyoshangaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…