Wakurugenzi wa TISS tangu uhuru mpaka sasa. Mzee Mzena ashikilia rekodi ya kuhudumu muda mrefu zaidi

Wakurugenzi wa TISS tangu uhuru mpaka sasa. Mzee Mzena ashikilia rekodi ya kuhudumu muda mrefu zaidi

Spy chiefs waliojenga medani ni Gama, Kitine na Mahiga kuifanya medani iwe medani kweli, (Mawazo yangu haya)

Zama zile za "Hey day" uibe pesa za umma!! unaibaje kwa Mfano. Kitu gani kifanyike "white corridors" isifahamu nchi hii. Zama za kiongozi kuwa na kalamu mbili mfuko wa shati, moja yake, moja si yake. 😁

Zama ambazo ukisaini nyaraka, nyaraka inakutangulia kufika pamoja na kuwa wewe unayo kwenye bahasha. 😁

Zama ambazo Kiongozi haendi Ulaya bila kupita Geneva wakati anarudi au wakati anaenda na taarifa zake zinakuwepo hapo, anazozijua na asizozijua zinabaki hapo. Kiongozi Huendi Amerika iwe kutembea au kikazi bila kupitia au kupata simu toka kwa "Unknown" waliopo Ontario au Toronto. 😁

Mr. HAND anapanga kuchoma benki kubwa kuteketeza nyaraka baada ya wizi wa maandishi kufahamika, vijana washafika hapo benki kubwa siku mbili kabla ya njama hiyo na wametoa kopi nyaraka zote ofisini kwake na wamebakisha vivuli bila yeye na crew yake kutambua, original zikapelekwa "safe place" hapo "logs".

Wamemdaka Geneva, Ticha kawaambia wasimuue wampe "Exile". Mr. HAND alirudi hii nchi baada ya Ticha kuvuta shuka kabla ya milenia.

Ticha anafanyiwa "Coup" jaribio linazimwa kimafia "in the blink of an eye" hapo hapo "logs" shombo la samaki.

Dah kweli muda unakwenda, nimekumbuka mbali japo kumbukumbu zangu haziwahusu na hamzijui. 😁

Mwaka 1978, Iddi Amini anaopigana vita Kyaka na vijana wa Kitine wapo hapo hapo Entebe kama raia wa Uganda wakiangalia kwa karibu uwanja wa ndege wa Entebe, nani anaruka nani anatua kwa namna gani na analeta nini. Ni busara tuu ya Ticha kutotaka kumuua Amin wala kujitwalia nchi ya Uganda. Uganda ingeshakuwa yetu. 😁

Tafsiri.
Logs=Magogo
HAND=Mkono
Exile= Uhamishoni
Coup= Jaribio la kupindua serikali.
Safe place= Sehemu salama
White corridors= Jumba jeupe (Suti nyeusi).
Unknown= isiyofahamika/wa.
😁
Siku hizi tunapandishiwa bei ya sukari, mafuta na umeme Hawa jamaa wapo tu kinyonge,

Tumepambania bandari isichukuliwa wapo kimya na wameshiriki kuandaa kesi ya uhaini

Tulipojitoa kumpigania katiba mpya walihusika kutuandalia kesi za ugaidi

Kiufupi Hawa jamaa ndo wanahujumu nchi
 
Makalla?
Mkuu huko umekwenda mbali.
Hebu taja mwingine.
Steve Nyerere, Mama anamkubali sana huyu dogo kiboko ya Mama Wema Sepetu. Dogo anarekodi mazungumzo nyeti ya watu toka akiwa mtoto kisha anauza baa siri zao na kukuza jina huku akipewa offer za bure.
 
Kwa kweli usalama wa taifa kwa sasa ni kama wametekwa na Ccm hawana habari ya kutetea maslahi ya taifa kama ambavyo wamelala. Wako tayari kutetea maslahi ya viongozi na maslahi yao ndiyo maana mama Abdul anawabadilisha awezavyo.

Issue ya DPW, Loliondo na maeneo mengine, lakini pia ufisadi na hizi wa rasilimali za umma ulivyokithiri unatia shaka sana kuamini Luna chombo madhubuti kilichoapa kulitetea taifa na rasilimali zake.

Ndiyo maana akijitokeza mkosoaji wa kukemea na kutaka rasilimali za nchi zisigawiwe kama njugu wako tayari kukuvunja taya na kukutelekeza uliwe na wanyama wakali.

Na sijui lini usalama utarudi kwenye viwango vyake.
 
Kanali Apson Cornel Mwang'onda. Nimekuta hii identity ktk Salam za rambi rambi
Mzee Apson hakuwahi kuwa mwanajeshi.

Watanzania kwa kuchanganya madesa huwajui?

Majuzi hapa kwenye kurasa za polisi wanaandika mtu kakamatwa kwa kutembea na gari isiyo na "plate number" kiuhalisia neno stahiki ni NUMBER PLATE na sio PLATE NUMBER.
 
1. Wa kwanza ni Mzee Emilio Mzena, huyu aliongoza mwaka 1961 hadi mwaka 1975. Ndiye Mkurugenzi wa TISS aliyeongoza idara hii kwa miaka mingi zaidi kuliko wengine (miaka 14).

Wengine ni kama ifuatavyo:
2. Dkt. Lawrence Gama: 1975-1978

3. Dkt Hassy Kitinr: 1978 - 1980

4. Dkt. Augustine Mahiga: 1980-1983

5. Luteni Jemerali Imran Kombe: 1983-1995

6. Kanali Apson Cornell Mwang'onda: 1995 - 2005

7. Othman Rashid: 2005 - 2016

8. Dkt. Modestus Kipilimba: 2016 - 2019

9. CP Rajabu Diwani: 2019 - 2023

10. Saidi Hussein Massoro: 2023 - 2023

11. Balozi Ali Siwa: 2023 - 2024

12. Suleiman Abubakar Mombo: 2024 - Hadi sasa

PIA SOMA
- Uteuzi: Abubakar Mombo Ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa, Siwa amestaafu

- Orodha ya Wakurugenzi Wakuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) tangu Uhuru

Kuna aliyehudumu kwa mwaka mmoja au miezi kadhaa. Huko aliko anaweza kuwa anashangaa kama mimi ninavyoshangaa
 
Back
Top Bottom