Siku hizi tunapandishiwa bei ya sukari, mafuta na umeme Hawa jamaa wapo tu kinyonge,Spy chiefs waliojenga medani ni Gama, Kitine na Mahiga kuifanya medani iwe medani kweli, (Mawazo yangu haya)
Zama zile za "Hey day" uibe pesa za umma!! unaibaje kwa Mfano. Kitu gani kifanyike "white corridors" isifahamu nchi hii. Zama za kiongozi kuwa na kalamu mbili mfuko wa shati, moja yake, moja si yake. 😁
Zama ambazo ukisaini nyaraka, nyaraka inakutangulia kufika pamoja na kuwa wewe unayo kwenye bahasha. 😁
Zama ambazo Kiongozi haendi Ulaya bila kupita Geneva wakati anarudi au wakati anaenda na taarifa zake zinakuwepo hapo, anazozijua na asizozijua zinabaki hapo. Kiongozi Huendi Amerika iwe kutembea au kikazi bila kupitia au kupata simu toka kwa "Unknown" waliopo Ontario au Toronto. 😁
Mr. HAND anapanga kuchoma benki kubwa kuteketeza nyaraka baada ya wizi wa maandishi kufahamika, vijana washafika hapo benki kubwa siku mbili kabla ya njama hiyo na wametoa kopi nyaraka zote ofisini kwake na wamebakisha vivuli bila yeye na crew yake kutambua, original zikapelekwa "safe place" hapo "logs".
Wamemdaka Geneva, Ticha kawaambia wasimuue wampe "Exile". Mr. HAND alirudi hii nchi baada ya Ticha kuvuta shuka kabla ya milenia.
Ticha anafanyiwa "Coup" jaribio linazimwa kimafia "in the blink of an eye" hapo hapo "logs" shombo la samaki.
Dah kweli muda unakwenda, nimekumbuka mbali japo kumbukumbu zangu haziwahusu na hamzijui. 😁
Mwaka 1978, Iddi Amini anaopigana vita Kyaka na vijana wa Kitine wapo hapo hapo Entebe kama raia wa Uganda wakiangalia kwa karibu uwanja wa ndege wa Entebe, nani anaruka nani anatua kwa namna gani na analeta nini. Ni busara tuu ya Ticha kutotaka kumuua Amin wala kujitwalia nchi ya Uganda. Uganda ingeshakuwa yetu. 😁
Tafsiri.
Logs=Magogo
HAND=Mkono
Exile= Uhamishoni
Coup= Jaribio la kupindua serikali.
Safe place= Sehemu salama
White corridors= Jumba jeupe (Suti nyeusi).
Unknown= isiyofahamika/wa.
😁
Tumepambania bandari isichukuliwa wapo kimya na wameshiriki kuandaa kesi ya uhaini
Tulipojitoa kumpigania katiba mpya walihusika kutuandalia kesi za ugaidi
Kiufupi Hawa jamaa ndo wanahujumu nchi