Wakurugenzi wapya walioteuliwa watakiwa kuripoti TAMISEMI wakiwa na CV pamoja na vyeti vyao

Wakurugenzi wapya walioteuliwa watakiwa kuripoti TAMISEMI wakiwa na CV pamoja na vyeti vyao

Utaratibu wa sasa hautendi haki.
Hautoi fursa sawa kwa watanzania wote wenye Sifa kupata fursa ya kutumikia Taifa lao.

Ni wale ambao ni ndugu na wanaojulikana na Rais na wasaidizi wake tu ndio wanapata huo upendeleo.

Hii si sawa hata kidogo.

Actually uwezekano wa kupata watu wasio mahiri na Sifa ni mkubwa sana ambapo itaenda kuchelewesha maendeleo ya nchi.

Katiba katiba .
 
Vetting ilitumika kadi ya UVCCM na ndio ilikuwa na nguvu,Leo vyeti vya taaluma,uzoefu je?
Samahani ndgu, naomba kufahamu hivi mfano mtumishi akifanyiwa vetting ni lazima kuteuliwa? Au anawezafanyiwa vetting na bado asiteuliwe wala kupewa nafasi mpya ya kazi/utumishi? Naomba kufahamu
 
Wenzetu Kenya kianzia viongozi wajuu nafasi zinatangazwa publicly na watu wenye Sifa wanaomba na mchakato wa wazi kufanyika wa usaili na hatimae mshindi kutangazwa.

Mfano IGP, Judges n.k
 
Siku hizi ni tofauti.. Kwanza uteuzi kisha ndio vetting .. Usishangae baada ya wiki wengine wakatenguliwa
Wacha wivu. Kama ni kukurupuka tu mbona askofubagonza hajateuliwa si ana PhD ya mormons? Ae wewe, mbona hukubahatisha?
 
Mazingira ya kumwajiri mwalimu na mkurugenzi ni vitu viwili tofauti.

Mwalimu anatuma maombi kwa njia ya mtandao ndio maana wakati wa kuripoti hutakiwa kwenda na nyaraka zake ili zihakikiwe kama ni feki au OG

Lakini uteuzi wa wakurugenzi unafanywa under intensive vetting including kutuma cv na vyeti kwa mamlaka ya uteuzi kwaajili ya mapitio n.k

Sasa imeendaje hawa watu ambao wanafanyiwa vetting before kuteuliwa waambiwe wakaripoti tena na vyeti ambavyo tayari walishatuma?
Hapo sasa!

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
CV ya nini ikiwa mliwateua baada ya kufanya vetting?
Ndio mjue tunapomkosoa huyu mama yenu hatukosoi kwa bahati mbaya bali tunamaanisha dhahiri kwamba uwezo wake wa kuongoza nchi ni mdogo
 
Hawa hawaendi kuwa DEDs hawa ni makala wa uchaguzi kuhakikisha ccm inashinda.
 
Dada yangu (si mama kwangu), Rais Samia Suluhu Hassan aliwahi kusema "Rais huwa hakosei". Kwa usemi huo tu tayari alikuwa kakosea maana hakuna mtu asiyekosea, hayupo na hatakuwepo!

Ndio maana unahitajika upitiaji makini (keen vetting) katika kusoma, kuchambua na kuamua kabla ya kutandika mkeka wowote ule hadharani. Atakuja kuteua aliyekufa au mfungwa!

Sasa ona ambavyo kila uteuzi analazimika kurudiarudia na kurekebisha, hususan baada ya kukosa kutangulia uhakiki makini. Hata bunge la bajeti alilikosea mara kadhaa kwa kuliita bunge la katiba. Akasema: "sijui nina maradhi gani na katiba." Ni maradhi ya kukosea mara kwa mara kwa kukosa umakini!

Si maradhi ya katiba tu, bali hata maradhi ya wizara (mathalani kateua waziri wa tozo kandamizi badala ya waziri wa uchumi na mipango endelevu na yenye tija), maradhi ya mikoa, maradhi ya wilaya na sasa maradhi ya wakurugenzi wa halmashauri. Mkurugenzi mmoja anataka aongoze halmashauri mbili kwa wakati mmoja. Mara paap, kajikuta kakosea tena!

Je, atawezaje (au wasaidizi wake), kusoma na kuchambua kwa makini mikataba mikubwa yenye kurasa zaidi ya 800??!!

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
Ata Katibu Mkuu kiongozi aliteuliwa akiwa Airport na Rais alisema alikuwa hamjui😂😂
 
Back
Top Bottom