Wakuu hivi kuna nchi nyingine bora kuishi duniani kama Tanzania?

Wakuu hivi kuna nchi nyingine bora kuishi duniani kama Tanzania?

Kwa amani na utulivu katika nchi nilizowahi kutembelea, ya kwanza ni Saudi Arabia.

Nchi ambayo nilikuta watu wanaacha maduka wazi wakienda kusali na hakuna anaeiba.
Kule inabidi uwe mwarabu ili hiyo amani ikuhusu. Kuna rafiki yangu alikuwa huko kapewa show ya hatari hadi kakimbia mishahara yake karudi kwao mombasa kuuza nyanya magengeni.
 
Tanzania sio nchi ya kuishi, Ni nchi ya kuishia.

Watu wanao ishi Tanzania ni wachache sana.

Wengi wa watanzania wanaishia,

Watanzania wengi ni walala hoi, Maskini choka mbaya...
Nini kinawazuia wasiwe matajiri mkuu.
 
Kutokana na utamaduni wetu ambao wa kitanzania tuliyouzoea kuishi kijamaa nakubaliana na wewe..

sisi tuna upendo sana....kuna baadhi ya nchi ukitoka tu mkoa mmoja kwenda mwengine unabaguliwa.
 
Kutokana na utamaduni wetu ambao wa kitanzania tuliyouzoea kuishi kijamaa nakubaliana na wewe..

sisi tuna upendo sana....kuna baadhi ya nchi ukitoka tu mkoa mmoja kwenda mwengine unabaguliwa.
Umeisema vizuri, hii kitu ndio naimaanisha. Sijui kama kuna nchi inapatikana.
 
Zipo nchi unaweza ishi vizuri kuliko hapa.
Binafsi ni msafiri mzuri tu na nimejionea.
Kuna nchi kama 6 zipo hapa afrika ni bab kubwa unaweza ishi hata bila pesa wewe ni kufanya kilimo, kuvua samaki na mambo yapo vizuri tu.
Na kuna moja nina mpango nikisha staafu nikaishi uko ni kuzuri kupita maelezo.
yote kwa yote nyumbani ni nyumbani.
 
Kulingana na Mada au Bandiko kuu Jibu ni rahisi

HAKUNA, hakuna nchi bora nyingine kuishi Duniani kama Tanzania.

Hivi jiulize, hawa wote(majina nayahifadhi na wawekezaji uchwara) watoke makwao na vimbelembele vya kuja kuwekeza na kuishi nchini ni kwa sababu gani nyingine zaidi ya Ubora....wanaacha manchi yanayosemekana yana ubora wa kila kitu, kwanini waje hapa kwetu Tanzania?

Na anayebisha aende aendako.

Hatahivyo,Watanzania wanasema hatujardhika na Mkataba wa Bandari baina ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya DPW.
 
Zipo nchi unaweza ishi vizuri kuliko hapa.
Binafsi ni msafiri mzuri tu na nimejionea.
Kuna nchi kama 6 zipo hapa afrika ni bab kubwa unaweza ishi hata bila pesa wewe ni kufanya kilimo, kuvua samaki na mambo yapo vizuri tu.
Na kuna moja nina mpango nikisha staafu nikaishi uko ni kuzuri kupita maelezo.
yote kwa yote nyumbani ni nyumbani.
Mkuu tuwekee hapa, ili siku tukijisikia kutalii basi tupape kipaumbele.
 
Kwa amani na utulivu katika nchi nilizowahi kutembelea, ya kwanza ni Saudi Arabia.

Nchi ambayo nilikuta watu wanaacha maduka wazi wakienda kusali na hakuna anaeiba.
Sawa. Ukiweza, nyenda na Uswizi upalinganishe na Saudi Arabia.
 
Ndio, kuna Parestina, Somalia, Sudan, DRC Congo, Ethiopia, Syria na Africa ya kati.. ni chaguo lako tu mkuu
 
Ni kweli kabisa kuna dereva mmoja wa malori ya nje ya nchi alishawahi kuniambia Tanzania ina nafuu kuliko nchi nyingi za Africa licha ya watu wachache kula meema ya nchi huko kwa wenzetu wana matatizo kutuzidi.
 
Yule waziri alisema twende Burundi 🇧🇮
 
Back
Top Bottom