Tanzania ni nchi bora kuishi ukiwa aina ya mtu mwenye sifa zifuatazo:Kwa uzoefu wangu mdogo, na nchi nyingi nimezijifunza kwa kusoma na kufuatilia maisha yao naona Tanzania licha ya madhaifu yetu ni sehemu bora sana.
Unaweza kwenda popote ukapokelewa utadhani mlifahamiana miaka mingi iliyopita.
Kama hauna ishu za kisiasa na ujanjaujanja maisha yako bomba sana.
Changamoto nyingi kama utazitatua mwenyewe mfano umeme ukafunga Solar au Backup Genset, Maji ukachimba kisima, etc unaishi vzr tu.
Nchi nyingine nashauri twendeni tukatalii tu, ila maisha ya bongo kama unajichanganya na wananzengo yako safi sana.
Nyie mliotembeatembea huko duniani kuna nchi gani bora zaidi ya hii bongo kiamani na mahusiano ya kijamii
1. Mjinga asie jua haki zake.
2. Muoga na masokini asio panda mapambano
3. Alie ridhika na hali yake ya uchumi ata kama anaumia.
4. Mnafiki ambaye anaweza akaishi kwa unafiki unafiki kuchekea kila mtu hata kama umpendi
5. Mtu asie kua na exposure pamoja na elimu upo upo. Nk.