Design Your Idea
Senior Member
- Jun 3, 2024
- 154
- 480
Ndiyo, benki nyingi Tanzania zinakubali kiwanja kama collateral, lakini siyo ukubwa wa kiwanja pekee unaoamua. Muhimu zaidi ni kuwa na hati/nyaraka halali za umiliki na kiwanja kiwe na thamani inayoweza kuthibitishwa na valuator anayekubalika na benki.Karibuni
Nina biashara ,ila nataka kuongeza bidhaa, benki ipi ina sera za kuwapatia wateja mikopo kwa kutumia hata kiwanja?
Nina biashara ya hardware mkuuMtaalam, jambo sio kuwa na asset au dhamana, la hasha, kitu kikubwa benki wanazingatia ni uwezo wako wa kurejesha mkopo wao.
Wengi tunafikiri kwa vile nna gari, kiwanja au chochote cha thamani, nnaweza kwenda kukopa benki bila shida yoyote, ni kweli inawezekana, ila lazima waone uwezo wa kurejesha pesa yao kila mwezi kutokana na shughuli/ Biashara/ajira yako.
Benki hawapendi ifike mahali waanze kufanya udalali kutafuta wateja wa kununua kiwanja chako kea kushindwa kulipa.
Hitimisho, kama una kiwanja na una chanzo kingine cha kuweza kulipa mkopo kila mwezi, uwezekano mkubwa ukapata mkopo, ila kama ni kiwanja peke yake, inabidi uyajenge na afisa mikopo.
Ahsantw bossNi kweli kabisa unaweza kukopeshwa, ila wana angalia bei ya soko ya kiwanja; na benk wanakukopesha kwa takriban nusu ya bei ya soko ya kiwanja chako.
Mfano; kama kiwanja chako kwa bei ya soko ya eneo kilipo ni 30mil
Benk wanaweza kukukopea kwenye 15mil hivi, wakizidi sana 20m
Wanafanya hivyo ili ukishindwa kurejesha wakiuze chap
Ahsantw sanaMtaalam, jambo sio kuwa na asset au dhamana, la hasha, kitu kikubwa benki wanazingatia ni uwezo wako wa kurejesha mkopo wao.