Wakuu mliofanikiwa naombeni mnipe darasa

Vijana hamfadhiliki kabisa yani... last time ilitokea kazi hapo dar supervisor kwemye kampuni ya mitandao ya simu kama airtel, yas au halotel. Nikapigiwa sim niko Unguja nije dar kuifanya au recomendations.

Nikapiga kimya! Kuna kima kibao hum nimesaidia mwisho wa siku wanakuja kuwa vipande vya kimba! (Shits). Yan mkuu kijana yoyote wa jamii forum kokote alipo kama hana kaz ya kueleweka lolote limkute
 
Hata wewe ungekuwa kwa nafasi zao za kusaidika ungekuwa hivyo hivyo tu kama ulivyowaita shits
 
Likitokea deal lingine nipasie mkuu hutajutia
 
Sahau hilo, yaani mtu akupe mbinu ya kuwa tajiri! Piga ua utapata yale yale ya jitume na fanya kazi kwa bidii. Mbinu yake ya kweli hawezi kukuambia, trust me.
 
Mambo mengine ni siri, nitakupa darasa lipi? Muombe tu Mungu wa Israel.
 
Sahau hilo, yaani mtu akupe mbinu ya kuwa tajiri! Piga ua utapata yale yale ya jitume na fanya kazi kwa bidii. Mbinu yake ya kweli hawezi kukuambia, trust me.
Sio lazima unipe mbinu zote mkuu walau nipate kutoka katika kuchakaza ndala na nile milo mitatu hayo mengine nitajiongeza
 
Ili upate ushauri sahihi ni lazima kwanza ungeelezea unafanya uchuuzi gani na kwa staili gani?hobby yako ni nini au uzoefu wako ni kitu gani katika mazingira yako yaliyokuzunguka halafu wadau ndio waanzie hapo kukushauri,huwezi kutoboa kwa kurukia kila aina ya ushauri utakaopewa utapoteza focus na consistency.
Watu wanaofanikiwa ni wale wanaoshikilia msimamo kwenye kile wanachokifanya huku wakiongeza ubunifu.
Nitakupa mfano mmoja ili unielewe,kuna jamaa mmoja hivi yeye biashara yake ni kuuza ndoo na mapipa ya kuwekea maji yaani tangu mimi niko shule nasoma hadi leo hii jamaa bado hajaacha ile biashara na amejenga nyumba zaidi ya 3 kupitia biashara ile sasa mtu huyu angekuwa anarukia kila biashara anayoshauriwa au kusimuliwa asingefanikiwa kwa kiasi kile.
Maisha ndio yako hivyo ndugu.
 
walizingua nini mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…