Wakuu mliofanikiwa naombeni mnipe darasa

Wakuu mliofanikiwa naombeni mnipe darasa

Sio lazima unipe mbinu zote mkuu walau nipate kutoka katika kuchakaza ndala na kula milo mitatu hayo mengine nitajiongeza
Tembea tembea huko kwa waganga ila jua kuna waganga fake pia. Kazi halali utaishia kupata pesa ya kula na kulipa kodi tu. Hao unaowatamani karibu wote ni utajiri wa ndagu au wakuiba pesa tena pesa nyingi. Ukiiba kidogo hutofanikiwa na ndio utakuwa umejizika mazima. Usione watu wanavaa mabangiri makubwa mikononi ukadhani urembo, yameundwa hayo.
 
Mchuuzi wa nini ? Taja unachokifanya kwa sasa, ushauriwe namna bora ya kuongeza wigo wa kipato chako na connection kadhaa
Ukinikuta site nimebebelea chaja, redio na makolokolo mengine pia nasajili lain wakati mwingine na hadi saizi bilabila nipe mbinu/connection mkuu
 
Ili upate ushauri sahihi ni lazima kwanza ungeelezea unafanya uchuuzi gani na kwa staili gani?hobby yako ni nini au uzoefu wako ni kitu gani katika mazingira yako yaliyokuzunguka halafu wadau ndio waanzie hapo kukushauri,huwezi kutoboa kwa kurukia kila aina ya ushauri utakaopewa utapoteza focus na consistency.
Watu wanaofanikiwa ni wale wanaoshikilia msimamo kwenye kile wanachokifanya huku wakiongeza ubunifu.
Nitakupa mfano mmoja ili unielewe,kuna jamaa mmoja hivi yeye biashara yake ni kuuza ndoo na mapipa ya kuwekea maji yaani tangu mimi niko shule nasoma hadi leo hii jamaa bado hajaacha ile biashara na amejenga nyumba zaidi ya 3 kupitia biashara ile sasa mtu huyu angekuwa anarukia kila biashara anayoshauriwa au kusimuliwa asingefanikiwa kwa kiasi kile.
Maisha ndio yako hivyo ndugu.
Ahsante sana mkuu pitia comment #42 nimeeleza ninachikifanya
 
Tembea tembea huko kwa waganga ila jua kuna waganga fake pia. Kazi halali utaishia kupata pesa ya kula na kulipa kodi tu. Hao unaowatamani karibu wote ni utajiri wa ndagu au wakuiba pesa tena pesa nyingi. Ukiiba kidogo hutofanikiwa na ndio utakuwa umejizika mazima. Usione watu wanavaa mabangiri makubwa mikononi ukadhani urembo, yameundwa hayo.
Siamini kuhusu uchawi na uganga wa kichawi labda uganga wa kitabibu pia kuwa na nyumba, usafiri na biashara nahisi ni maisha ya mafanikio ya kawaida na sio utajiri mkubwa au unaonaje mkuu
 
Mimi ni mchuuzi ila ninaeajirika katika sekta zisizo za kielimu na kielimu pia, najiita hustler kwa maana kazi yoyote isiyotweza utu wangu napiga lengo kubwa ni kutoboa katika maisha kwa maana niweze kula vizuri, nisiwe na mawazo ya bill mbalimbali, nijenge bungalow lenye floor mbili na gari walau la 15mil huko ndio kutoboa ninakotarajia, huku kukisindikizwa na mirija mbalimbali ya pesa zikiwemo biashara na kazi ya uhakika ya kudumu

Wakuu, uwe umefanikiwa kisiasa, kielimu au kibiashara walau ukaweza kumiliki vitu nilivyotaja hapo juu au zaidi una nafasi ya kunishauri kijana wako, japo najua siwezi kupita njia sawa ulizopita wewe nikafanikiwa kama wewe ila walau ninaweza kuchanganya na zangu nikatoboa

Kumbuka ushauri huu ni kwa ajili yangu na ma-hustler wengine humu toa mbinu, njia na hata connection tupate kusaidika.

Usilete mzaha watu tupo serious karibu
Ki kazana na shule inavileta
 
Ahsante sana mkuu pitia comment #42 nimeeleza ninachikifanya
Sawa nimeona mkuu.
Bado kwenye ishu ya ubunifu uko nyuma ya muda halafu akili yako inawaza kupewa connection hii sio suluhisho ukishaanza kuomba connection maana yake ushafeli kwenye ishu ya ubunifu.
Anzisha mradi kisha watu waje kukuungisha hii ndio itakuwa connection.
Tumia hizo pesa unazopata kwenye kusajili laini kama mtaji ili uanzishe mradi ambao unaona unaendana na mazingira uliopo
 
Nitaanzishaje mradi kwa hela za kula mkuu kazi ninayofanya ni hand to mouth
 
Nitaanzishaje mradi kwa hela za kula mkuu kazi ninayofanya ni hand to mouth
Kwenye kuanzisha mradi haitegemei ukubwa wa pesa unayoipata bali inahusisha zaidi nia yako na uchungu wa kutimiza ndoto zako kutoka moyoni mwako mwenyewe usingoje hadi watu waje kukuhamasisha.
Labda ukipiga hesabu kwa mwezi unakusanya kiasi gani kwenye deal unazozifanya na kwa siku matumizi yako ni kiasi gani kisha nitakushauri cha kufanya
 
1. Epuka kukaa katika comfort zone
2. Punguza matarajio kutoka kwa watu hii itakusaidia pale ukianguka hutalaumu mtu bali utajifunza na kusonga mbele (weka matarajio makubwa kwenye akili zako na nguvu zako)
3. Punguza msururu wa wategemezi namaanisha jifunze kusema hapana au sina hata kama kipo, huu sio uchoyo bali ni discipline ya fedha.
4. Sio kila mchongo ni wa kupaparikia mwingine unaweza kukuzamisha(vipaumbele )namaanisha jifunze kutathmini kabla yakuingia mazima though kujaribu ndo kujifunza ila ingia kwa step.
5.kusali si lazima uwe na dini as long as unamwamini Mungu basi muombe akusaidie kwenye mishe zako na ukumbuke kutoa sadaka( sio lazima kanisani au msikitini hata ukiwanunulia maji watoto wa mtaani)
6. tengeneza vyanzo vingine vya mapato usitegemee kimoja, jaribu hata vile vidogo vidogo tu vinakupa walau 200 ya kusolve mambo madogo madogo.
PESA INAHITAJI MTU JASIRI NA MWENYE ROHO NGUMU. mimi mwenyewe sina hizo pesa maana nimeyashindwa mengi niliyoandika hapo juu.
KILA LA HERI MPAMBANAJI.
 
Kwenye kuanzisha mradi haitegemei ukubwa wa pesa unayoipata bali inahusisha zaidi nia yako na uchungu wa kutimiza ndoto zako kutoka moyoni mwako mwenyewe usingoje hadi watu waje kukuhamasisha.
Labda ukipiga hesabu kwa mwezi unakusanya kiasi gani kwenye deal unazozifanya na kwa siku matumizi yako ni kiasi gani kisha nitakushauri cha kufanya
It's just hand to mouth na wakati mwingine na madeni juu sikudanganyi ndio uhalisia imagine mfano leo hadi saizi sijapata mteja huo mwezi nasave vipi zaidi nitatumia nilichopata jana
 
Siamini kuhusu uchawi na uganga wa kichawi labda uganga wa kitabibu pia kuwa na nyumba, usafiri na biashara nahisi ni maisha ya mafanikio ya kawaida na sio utajiri mkubwa au unaonaje mkuu
Vizuri, hata mimi siamini ki hivyo.
Nilipata kazini sehemu, tena kazi ya mshahara mkubwa tu. Nikakaa kizembe. Kuna watu kazini wanaitamani kazi ila tukikutana tunacheka wote na wanasema" wewe jembe mwanetu, dah tunakukubali sana" Mimi hapo nakenua kweli kweli. Mara nikaanza kuumwa hiki mara kile. Mmoja akanipa mbinu ya kupata pesa nyingi, nikaingia mkenge then akanichoma. Kazi ikaisha hivyo kumbe kuna watu washafanya yao ili mimi nikubali maana mwanzoni nilikataa katu katu. Hapa na pale nafanya kazi zangu mwenyewe japo kila siku customers wanapungua kwa sababu niko nje ya game, NSSF hii hapa. Nikakaa kijinga vile vile eti naanzisha bishara na kufungua kakijiofisi kangu maana kabla ya hapo nilikuwa nafanyia nyumbani au kwa watu. Dadeki wahuni hawa hapa tena, anyway kifupi nilifirisika vibaya sana.
Sasa hivi mpaka niwe naamka usiku wa saa tisa nasali ndipo napigiwa simu ya kuitwa kufanya ambayo inaisha siku hiyo hiyo (yaani unamfanyia mtu kazi anakulipa na imeisha hiyo). Unakaa tena kama week kadhaa ukisali kila siku ndipo upigiwe tena simu.
Ndugu bila kuwa mshirikina au kuiba pesa nyingi hayo matamanio yako hutoboi. Biashara,uchawi, makazini huko nako, uchawi tu. Ndiyo maan sina matarajio ya kuwa tajiri kwa sababu sina imani nao nimeishia kupata hela ya kula na kulipa kodi. Kodi yenyewe sasa, kila siku nahama hama mpaka sasa niko huku ndani ndani ninapo pamudu.
NB: KUSHINDWA KWANGU SIYO KUSHINDWA KWAKO AU KWA WATU WENGINE.
 
It's just hand to mouth na wakati mwingine na madeni juu sikudanganyi ndio uhalisia imagine mfano leo hadi saizi sijapata mteja huo mwezi nasave vipi zaidi nitatumia nilichopata jana
Una umri gani mkuu na unaishi mkoa gani?
Mimi nina vijana wangu wanafanya biashara kama hiyo kuna ubunifu fulani wanaufanyaga kina kipindi huwa wanakusanya hadi 600,000 kwa mwezi
 
Back
Top Bottom