JUAN MANUEL
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 7,808
- 16,972
Passport, ya kusafilia, NIDA,au kadi ya mpiga kuraWakuu baada kupambana hapa Tabora na kutokuona mwelekeo wowote maisha nimeamua niende Zanzibar. Sasa nimekuja hapa mnipe muongozo jinsi ya kuingia Zanzibar nataka niende huko nikatafute KAZI ZA UJENZI. Pesa niliyonayo Kwasasa niliyosevu ya kunifikisha huko kutoka Tabora na matumizi mengineyo nitakapokuwa natafuta kazi ni laki 1 na nusu tu(Sina pesa nyingine). Tafadhari ushauri wenu wakuu.
UONGO MTUPU ETI WAZANZIBAR WANA ROHO NZURI(Blueprint)
Kuingia Zanzibar
Unahitaji kuwa na kitambulisho , NIDA vote ID , reseni n.k
Sehemu pakufikia , Kama wewe ni muislam Ila hauna pakufikia jitahidi upande boti ya Ahsubui then ukifika tafuta msikiti wowote kuanzia hapo forodhani waambie hilo swala lako.
Kuwa hauna pakulala Ila unafatilia fursa katika miradi ya ujenzi.
Hawa jamaa wanajiita wazanzibari wana roho nzuri Sana hawana ubaguzi wowote .
Kuhusu kula
Kulala ukifika Zanzibar usiwaze kale kanchi kamebarikiwa watu wakarimu na wenye UPENDO .
Jitahidi uwe na maadili zile tabia za kibongo za kugoneka na kupombeka hawazifagilii so wakikusoma Una hizo mambo wataanza kukuchukulia poa poa na kuua reputation yako.
Kutoboa na kufanikiwa -hii muachie Mungu wewe weka juhudi tu .
All the best Nigga.
Kweli Zanzibar kutoboa ni ngumu lakini kama anataka kwenda kutafuta Milioni moja au mbili ili arudi Tanganyika afanye biashara Adobe hapo sawa, Zanzibar mji wa kichawi sana ule Mifumo imeshkwa na watu wawili watatu tofauti na Tanganyika. uku Tanganyika mimi ninaweza kwenda nje ya nchi nikaagiza Sukari na Ngano na Sabuni hakuna shida ila Zanzibar upati hiyo ruhusa kwasababu hiyo biasharaku kuna mfanya biashara mkubwa anaifanya kwa hiyo wewe unazuiliwa. Mfano MO Dewji analeta Mafuta ya kula anakua peke yake tu mtu mwingine akitaka kuagiza ananyimwa Kibali.Zanzibar pagumu sana kutoboa.
Kwa nini usiingie hapo Dodoma au Dar tu ukapambane?
Tsh 200- mpaka utakapo fika kikomo cha mfuko wako! au umekosea ni mia mbili au elfu 21)Nauli hii unayo.
2)Vitambulisho kati ya hivi :
(a) Nida
(b) Mpiga kura
(c)Barua ya utambulisho kama hauna a na b
Kazi ni ngumu kupata ila shughuli za kufanya zipo na zinapatikana zaidi mashambani huko ndiko ujenzi wa mahotel hufanyika na unaendelea kufanyika!
Ukifika tembelea maeneo haya kama unatafuta vibarua na siyo kazi:
1)Nungwi
2)Paje
3)Kiwengwa
4)Mjini
5)Pemba
Malipo
a)Fundi:Tsh 30000-50000 kwa siku
b)Kibarua :Tsh 15000-20000 kwa siku
Malazi:
Chumba: Tsh 30000-100000 kwa mwezi.
Chakula:
Tsh 200- mpaka utakapo fika kikomo cha mfuko wako!
Hii ni kwa uzoefu wangu!
Wakuu baada kupambana hapa Tabora na kutokuona mwelekeo wowote maisha nimeamua niende Zanzibar. Sasa nimekuja hapa mnipe muongozo jinsi ya kuingia Zanzibar nataka niende huko nikatafute KAZI ZA UJENZI. Pesa niliyonayo Kwasasa niliyosevu ya kunifikisha huko kutoka Tabora na matumizi mengineyo nitakapokuwa natafuta kazi ni laki 1 na nusu tu(Sina pesa nyingine). Tafadhari ushauri wenu wakuu.m
m pia nataka mwongozo asanteee!
Sijakosea, kuanzia shilingi mia mbili (200) na kuendelea unaanza kupata chochote tumboni. Andazi, kisheti, kachori, katilesi, chai,uji n.k huanzia bei hiyo!Tsh 200- mpaka utakapo fika kikomo cha mfuko wako!
Dom, Dar pia zinajengwa, kwa steel fixing kazi naamini zipo maeneo hayo pia.Steel fixer mkuu.
Zingatia Zanzibar ni Nchi.Wakuu baada kupambana hapa Tabora na kutokuona mwelekeo wowote maisha nimeamua niende Zanzibar. Sasa nimekuja hapa mnipe muongozo jinsi ya kuingia Zanzibar nataka niende huko nikatafute KAZI ZA UJENZI. Pesa niliyonayo Kwasasa niliyosevu ya kunifikisha huko kutoka Tabora na matumizi mengineyo nitakapokuwa natafuta kazi ni laki 1 na nusu tu(Sina pesa nyingine). Tafadhari ushauri wenu wakuu.
Ndoto ya Kila Mtanganyika Kwa hivi Sasa ni kuingia Zanzibar hali hii isipodhibitiwa sijui hali ya Zanzibar itakuwaje baada miaka 10
Wenye dhamana waliangalie hili Kwa jicho la tatu kisiwa kinazama