Dialogist
JF-Expert Member
- Apr 14, 2014
- 1,167
- 1,872
Wakuu Salaam,
Leo asubuhi nikiwa jijini Dar es Salaam nimepanda gari (daladala) za kutoka Mbagala Charambe kwenda Mbezi Magufuli Bus Stand, ili nichukue Nyehunge ya Kurudi kwangu Nyamisati, na ndipo nikaona kitu cha kunishangaza kidogo, sio sana.
Nilijikuta ndani ya daladala tuliyopanda kwa kugombania na nikiwa nimeshikilia bomba ili nisianguke, huku tumebanana kama nyanya kwenye matenga, na konda akitulazimisha kupeana mgongo, basi jirani na mimi kwa mfumo huo huo wa kushikilia bomba, kulikua na wadada warembo sana, wawili wa kichina. Ni purely Chinese, ila kidogo wanaongea kiswahili. Kilichonishangaza ni namna hao wadada walivyojichanganya nasi kuanzia ndani ya aina hiyo ya usafiri, lugha yetu na hata mavazi walivaa vitenge vya kushona.
Tashtwiti yangu ipo hapo, hivi hamuoni kwamba kwa uwepo wa wachina wengi kiasi hiki Tanzania (Africa) haitasababisha bara letu kua koloni la wachina, kuanzia kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni kwa miaka michache mbele?
Zingatia, kuna thread ya mshana hapa alizungumzia ujio wa wachina 300k, pia zingatia wameanza kujichanganya mitaani na vijijini na kuzaana na wabongo...
Je hii sio strategic plan ya hawa jamaa kwa miongo kadhaa mbele wakaja sema Bara la Africa ndio asili yao?? Je hamuoni kwamba miaka 50+ mbele ukasikia (ukizaliwa upya) Rais wa Malawi ni Xui Cheng Ping au Rais wa Kenya ni Zhengo Dong Feng? Mara Waziri Mkuu wa Tanganyika miaka hiyo akawa Bing Yen Zhong?
Wakuu hili mnaliona? Au tuachane nayo tu!!!