Mkuu hoja hii ndio inayonidhoofisha, lakini ni kweli kwamba shule hizo za boarding hazina watoto, na je wote wamekuwa na tabia mbaya ama kupoteza 'bond'na wazazi wao?Nashauri mtoto anatakiwa kwenda boarding kuanzia form 1, chekechea hadi anapomaliza darasa la 7 anahitaji malezi ya wazazi wake. Atapata wapi upendo wa wazazi kama tangu anaanza shule yeye yupo boarding?
Mkuu una hoja ya msingi nitaitafakari zaidi, kimsingi nikiangalia hata tabia za watoto wa hizi shule za umma ambao wanashinda na wazazi bado zinasikitisha kbs!Kama unampeleka boarding hakikisha hiyo shule ina waalimu wa malezi ya watoto waliosomea na kubobea, hutojuta.
Akipata shule nzuri ya boarding ni bora kuliko akae nyumbani wakati wazazi wenyewe mnaondoka nyumbani saa 11 asubuhi na kurudi saa 5 za usiku.
Ni bora aende boarding atapata elimu bora na extra curricular activities kuliko kukaa nyumbani na house girl wakiangalia tamthilia za bongo movie.
Lipi ni jema sasa mkuu, apate elimu hii ya jua kali ili kulinda ukaribu wa mzazi na mtoto na malezi bora au aende akapate elimu itakayonjenga vizuri kuyakabili mazingira yake.Mkuu huku ni kumyima mtoto malezi angali bado mdogo na hili hupunguza ukaribu kati ya mzazi na mtoto.
Angalau angekuwa kidato cha Kwanza na kama kuna ulazima shule ya msingi basi yawe madarasa ya juu kuanzia darasa la 5 mpaka la 7.
Mkuu hoja hii ndio inayonidhoofisha, lakini ni kweli kwamba shule hizo za boarding hazina watoto, na je wote wamekuwa na tabia mbaya ama kupoteza 'bond'na wazazi wao?
Mkuu hebu fikiria tatizo la kimazingira, wazazi ambao wanaishi mbali na huduma ya hizi shule tunazoamini zinatoa elimu bora, je watoto wao wasipate fursa kabisa ya kunufaika na elimu hiyo kwa sababu za kimalezi?Mi huwa nashangaaga sana wazazi kupata ujasiri kuwapeleka watoto zao wadogo shule za boarding.Kipindi cha utoto ndo kizuri kumjua mwanao na kuanza kumfundisha taratibu za kimaisha pamoja na kumgombeza akikosea. Mtoto wako umesema ni wa kike,ebu fikilia kapata hedhi(period) yupo shule,anaweza kupata emotional support anayohitaji ambayo kama angekuwa nyumbani mama ake au hata wanawake wa family wangeweza kumsaidia, sasa unataka kazi hii ufanyiwe na wengine.Mtoto wako atakosa home life,Bullying na abuse ni uwezekano,pia kuna hisia kuwa kawa abandoned na wazazi hizi huwasumbua wakiwa wakubwa.
Mkuu numbisa ni kweli nilikuwa na fikra flani lkn kuomba ushauri ni muhimu ili tuweze kupima maamuzi yetu kupitia uzoefu wa wengine. Ninachokifanya ni kuangalia mizania kati ya hasara ya kimalezi na faida kwa mtoto.Kwa majibu yako hapo juu inaonekana tayari una solution basi tu kutuchora wananzengo. Peleka tu boarding si utalia wewe na mkeo sie washika vidumu na mifagio hayatuhusu