Mkuu hebu fikiria tatizo la kimazingira, wazazi ambao wanaishi mbali na huduma ya hizi shule tunazoamini zinatoa elimu bora, je watoto wao wasipate fursa kabisa ya kunufaika na elimu hiyo kwa sababu za kimalezi?
Elimu na malezi ni vitu viwili tofauti!
Unataka kumpa elimu, umesahau kuna malezi, na malezi bora huanza na msingi bora.
Sisi tulisoma shule za kawaida yet, tunaongea kingereza. Unatamani mwanao asome shule muitane daddy, mummy!
Ongeeni naye hiyo lugha nyumbani! Mbona wahindi, wahaya, wanyakyusa, wahehe, wasukuma e.t.c watoto wao hawasomi shule zenye lugha yao lakini lugha zao wanazimudu??
English siyo kipimo cha mafanikio maishani, ni lugha tu!
Mfundishane home, nakukatalia siyo sahihi kumpeleka mtoto, nursery boarding, hapati faida yoyote!
Vinaishia kuwa vichafu, vinaonewa, na kujua mambo mengi yaliyo nje ya age group.
Tuache kasumba ya kuamini English ni kipimo cha mafanikio.
Everyday is Saturday................................
😎