Wakuu, nishaurini kuhusu Shule ya bweni kwa mtoto wa nursery

Wakuu, nishaurini kuhusu Shule ya bweni kwa mtoto wa nursery

Mkuu naona hili jambo halijakubariki hata kidogo sawa pia na kwa wachangiaji wengi, niseme tu kwamba i do wish all the best for my kid na najaribu kufikiria njia iliyo sahihi ya yeye kuwa 'a strong lady in future' hivyo ninaona kukosa kwake elimu bora ktk hatua ya mwanzo inaweza pelekea asiwe mshindani mzuri hapo baadae, kama nilivyobainisha awali, option ya boarding imekuja tokana na kwamba mazingira yangu ya sasa hayana shule hizi za mchepuo wa Kiingereza ambazo ndio target yangu yangu.
English language, can be learnt, wherever! Why don't you nurture your daughter at home, to do things right, in a caring way? Remember, any short cut has a long cut.
 
Aisee.. mkuu, sikushauri.. nimesoma shule ya bweni primary. Angalau nilikua matured. Mtoto wa kike tofauti na wq kiume. Nilikua mdogo lakini jaman kilikua na vitoto vya babby class navyo. Roho inaumaje? Hapana aisee. Umbali woote ule dar to rombo tena boarding? Na chakula cha kawaida sana. Uzuri ama ubaya sisi wakubwa ndo kama tulikua responsible kusaidiana na matrons kuwaangalia. Kiwaohesha etc. Wazazi wetu walipokuja kujua haya walikasirika sana. Almanusra watuhamishe wote. Halaf kuna wengine wakawa na tabia mbovu. Neno kulawitiana nilikua hata silielewi maana yake. Nimekuja lijulia ukubwani tena advance. Boys walikua kina baadhi wana hivyo vimichezo. Kuna wengine walikua wanagukuzwa shule wanazotoka na hata oale kwetu walifukuzwa kwa kuwa walishabobea hiyo michezo. Wai wanaoma ni leisure kumbe ndo athari. Walitandikwa sana na ukafa huo mchezo kwakua masista waliamua kichachamaa. Kukatlkea tena librother linataka somea upadre kulawiti boys, likasemewa likafukuzwa. Hapa uzuri ni kwamba system ya shule ilikua imesimama vizuri. Je, shule unayotaka mpeleka iko vzr uongozi? Na saa zingine hao hao viongozi ndo wabaya. Naomba juniour abebe kidumu mfagio kwa sasa. Acha kutaka kumtesa mtoto. Acha kbs. Kwangu ni ukatili
 
Nursery ni mdogo sana jmn
Kaa nae nyumbani

Ana muda mrefu wa shule ya msingi atajifunza kiingereza mbeleni.,vichwa vya watoto ni vyepesi atashika tu hicho kiingereza hata kama atakutana nacho Sekondari
 
Mbona watu mashuhuri tu wamesoma shule hizi hizi za kidumu mfagio? Na mbona maisha yao yameenda vyema tu? Uzuri primary mbona akifikia age fulan unaweza muhamishia eng med tu?
Honestly... mimi iliniathiri sana. Nilikua bullied sana. Kijumla ilinifindisha kuamza kujitetea mapema sana. Nilijisikia kama mimi ndo niko kwaajili ya peke yangu. Moyo wangu uliingia baridi. Ilifikia stage wala sina mapenz na nyumban. Yaan athari ni nyingi mno. Hao hao unaamini ndo wakiangalizie mtoto ndo hao hao watakaomtorture. Na mtoto hana pa kujitetea. Mzazi ukiitwa ukasomewa kesi ha mwanao hata kama amesingiziwa huwez mtetea. Peleka kidumu mfagio. Sipendi kukumbuka maisha yale.
 
Mwandishi akusikilize sana wewe,pole kwa experience yako.
 
Naimani afya zenu ni njema kabisa wakuu, kuhusu mengineyo inshallah Allah atafanya wepesi.

Wakuu 'junior' wangu sasa amefikia umri wa kuanza shule, changamoto inayonikabili ni kuhusu upatikanaji wa shule hizi za mchepuo wa kimombo ktk mazingira niliyopo kwa sasa, huduma hiyo hamna.

Hivyo basi nimeazimia 'junior' akapambane na maisha ya boarding ktk umri huo! Je, athari za kimalezi kwa kumpeleka mtoto mdogo boarding school ni kubwa kuliko faida kama inavyoelezwa na wengi? Ukweli ukoje?

Ikumbukwe sina option zaidi ya hiyo vinginevyo basi 'junior' achukue kidumu na mfagio avuke barabara jambo ambalo sijaliafiki.

Karibuni wakuu mnipe mawazo yenu kwa mliowahi kumbana na situation hii, pia wenye uzoefu mbalimbali. (huyu 'junior ni binti).
Na wewe unaona sifa? Yaani unataka mtaani uwe unawaambia washikaji zako kwamba mtoto wako yuko Boarding?

Aisee Waafrica bahati mbaya mno

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Mi huwa nashangaaga sana wazazi kupata ujasiri kuwapeleka watoto zao wadogo shule za boarding.Kipindi cha utoto ndo kizuri kumjua mwanao na kuanza kumfundisha taratibu za kimaisha pamoja na kumgombeza akikosea. Mtoto wako umesema ni wa kike,ebu fikilia kapata hedhi(period) yupo shule,anaweza kupata emotional support anayohitaji ambayo kama angekuwa nyumbani mama ake au hata wanawake wa family wangeweza kumsaidia, sasa unataka kazi hii ufanyiwe na wengine.Mtoto wako atakosa home life,Bullying na abuse ni uwezekano,pia kuna hisia kuwa kawa abandoned na wazazi hizi huwasumbua wakiwa wakubwa.
Huwa wanafanya hivyo kama sehemu ya Show off mtaani, wengi huwa hilo ndo lengo lao

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu hebu fikiria tatizo la kimazingira, wazazi ambao wanaishi mbali na huduma ya hizi shule tunazoamini zinatoa elimu bora, je watoto wao wasipate fursa kabisa ya kunufaika na elimu hiyo kwa sababu za kimalezi?
Shule zipi?/Shule Bora nchi hii International School pekee, zingine hakuna kitu

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Lipi ni jema sasa mkuu, apate elimu hii ya jua kali ili kulinda ukaribu wa mzazi na mtoto na malezi bora au aende akapate elimu itakayonjenga vizuri kuyakabili mazingira yake.
Shule Bora ni International School tu, hizi sijui st nani ni wanaenda kusoma Kingereza tu hakuna kitu pale kwa sababu mwisho wa siku wanapimwa kwa paper ilio tungwa pale BMT

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Kama ambae nimepokea watoto wadogo kuja boarding wakiwa na 3 years nakushauri atleast kama ni ngumu sana kaa nae mpaka afike atleast la tatu. Inawezekana elimu huko ni ngumu ila kaa nae aweze hata kusema shida zake. Akiwa la tatu at least anaweza jisemea anauhitaji wa nini. 3 to 4 years bado ni Mdogo mno.
Hakuna cha atlest, mzazi anapaswa kuwa ba mtoto wake muda wote

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Naimani afya zenu ni njema kabisa wakuu, kuhusu mengineyo inshallah Allah atafanya wepesi.

Wakuu 'junior' wangu sasa amefikia umri wa kuanza shule, changamoto inayonikabili ni kuhusu upatikanaji wa shule hizi za mchepuo wa kimombo ktk mazingira niliyopo kwa sasa, huduma hiyo hamna.

Hivyo basi nimeazimia 'junior' akapambane na maisha ya boarding ktk umri huo! Je, athari za kimalezi kwa kumpeleka mtoto mdogo boarding school ni kubwa kuliko faida kama inavyoelezwa na wengi? Ukweli ukoje?

Ikumbukwe sina option zaidi ya hiyo vinginevyo basi 'junior' achukue kidumu na mfagio avuke barabara jambo ambalo sijaliafiki.

Karibuni wakuu mnipe mawazo yenu kwa mliowahi kumbana na situation hii, pia wenye uzoefu mbalimbali. (huyu 'junior ni binti).

Watoto wengi wanaharibika wakiwa shule za boarding.....Mpeleke mtoto boarding ambaye anajitambua .....kuanzia form v na kuendelea.
 
Hakuna shule kama hiyo Tanzania. Operators wa shule binafsi wanaajiri mbumbu ku- maximize profit. Wanaajiri matron wanaojua kufinya na kuchapa vitoto makofi.
Ipo shule moja Tosamaganga Iringa inaitwa Lyaramo ni shule ya masista ya boarding kuanzia nursery hadi darasa la saba, wapo vizuri sana kwa malezi.

NB: Shule hii inawafaa sana watoto wa kanisa la RC. Ingawa wanapokea dini zote.
 
Mimi nimesoma kidumu na fagio na ilikuwa mwendo wa kutembea distance tena Ili nijengea ufahamu na kujitegemea mapema, tofauti na watoto wa school bus kichwani empty set aisee hata vitu vidogo hawaviwezi kabisa,hata performance mbaya tu kuliko wa kidumu, na ndio maana sikuhizi watoto Hadi wanakua hawawezi kujitegemea kisa spoon feeding in everything.
Mkuu kisa babu alipasua maawe apate kokoto kwa nyundo haimaanishi ukatae kutumia crusher.

Mambo yamebadilika, kama mtu una uwezo mpeleke tu mtoto shule nzuri apande hiyo school bus tu. Ukiwa na uwezo usifanye maisha yawe magumu kwa watoto acha wasome huku ukwaandaa na mengine. Mfano wakirudi nyumbani umri ukiruhusu wafue uniform, zao weekend wapike, wasafishe vyumba vyao. Kama una boashara mfano duka unaweza likizo ukamwambia siku kadhaa akae dukani utamlipa na hiyo pesa atanunua vitu vya shule. Lengo ni kumjenga tu wa namna nyingine. Sidhani kama kusoma kwa kuhangaika ni sifa ila ni kutoafford. Walking 6km kwenda shule 6km kurudi si jambo zuri.
 
Ipo shule moja Tosamaganga Iringa inaitwa Lyaramo ni shule ya masista ya boarding kuanzia nursery hadi darasa la saba, wapo vizuri sana kwa malezi.

NB: Shule hii inawafaa sana watoto wa kanisa la RC. Ingawa wanapokea dini zote.
Mzazi ni mzazi tu, haijalishi iwe ya masister au nini ni ulimbukeni kuchukua mtoto wa Nursery ukampeleka boarding, inawezekana ikawa ni ukosefu wa akili pia.
 
Mkuu kisa babu alipasua maawe apate kokoto kwa nyundo haimaanishi ukatae kutumia crusher.

Mambo yamebadilika, kama mtu una uwezo mpeleke tu mtoto shule nzuri apande hiyo school bus tu. Ukiwa na uwezo usifanye maisha yawe magumu kwa watoto acha wasome huku ukwaandaa na mengine. Mfano wakirudi nyumbani umri ukiruhusu wafue uniform, zao weekend wapike, wasafishe vyumba vyao. Kama una boashara mfano duka unaweza likizo ukamwambia siku kadhaa akae dukani utamlipa na hiyo pesa atanunua vitu vya shule. Lengo ni kumjenga tu wa namna nyingine. Sidhani kama kusoma kwa kuhangaika ni sifa ila ni kutoafford. Walking 6km kwenda shule 6km kurudi si jambo zuri.
Sijafamya maisha magumu vyote ninavoeleza nimepitia na watoto wasoma hzo english medium na hakuna utofauti licha ya watoto kupata everything Ila ujinga wao ni mkubwa kuliko wa st kayumba, pia kutembea huwa ni mazoezi na inafanya akili ichangamke tofauti na Sasa watoto Kama kuku wa kisisasa Wana kila kitu Ila ni wabovu. Pia ka kwenu ni vilaza hata umpeleke english medium gani toto litakuwa tu kilaza kuliko umulemaze asijue vtu vya msingi Bora umfundishe kukomaa na azoee maisha ya kawaida.
So usiseme shule za kayumba ni ukale wakati zimetufikisha mahali na tumetimiza ndoto zetu. Usasa usiwe chaka la kukwepa responsibilities zetu kwa watoto
 
Back
Top Bottom