Wakuu wa JF, naomba dakika chache za muda wenu

Status
Not open for further replies.
Mtumie chochote kitu!
 
Umesema jambo la msingi mkuu, nimekupata. ๐Ÿ™ Nilifungua nafasi ya mawazo kwa sababu nilihitaji pia ushauri, siyo kwamba nimeacha kutafuta msaada wa mtaji. Ukweli ni kwamba bila mtaji ni vigumu kuanza, ndiyo maana bado nipo kwenye harakati za kutafuta namna ya kujikwamua. Nashukuru kila anayetoa ushauri na zaidi anayesaidia kwa kile alichonacho. Mungu awabariki wote.
 
Kwanza kabisa Mawazo255 kwa uandishi huu naamini sio mtu ambae ni Kukesha jf ukiomba msaada, at least labda kuna mahali ulifeli kimaisha (unaonekana ni mtu mzima kabisa)..

Pili ukishaomba msaada sehemu moja then ukarudi tena itaonesha una lako jambo... Mtu anaona sio shida tena, ni kawaida yako

Si semi hufai kupata msaada Hapana, naongea human nature. They see repeating the sema thing as behavior..

Ushauri: kama una watu wa karibu wenye uwezo tafuta mmoja kaa nae mweleze shida zako, hasa hao unasema unawategemea kwa sasa, you need someone to keep you disciplined and online people hawawezi.

Acha kuomba sana pesa mtandaoni ni kujidhaalilisha maana si wata tuma kwenye namba pia, hata kama utaumia jina la mtu mwingine bado the issue persists, na kingine unajiskiaje kuwa katika situation hii?..
 
Nimekuelewa sana mkuu, na kwa kweli ushauri wako nimeupokea kwa moyo mmoja. Sina nia ya kuifanya kuomba msaada kuwa maisha yangu, wala kujenga mazoea hayo. Nimepitia kipindi kigumu na ndiyo maana nimefikia hatua hii. Sasa ninachotafuta zaidi ni namna ya kujisimamisha na kuwa na kipato changu, si kuendelea kuomba. Asante kwa kunikumbusha kwa ukweli na heshima. ๐Ÿ™
 
Sasa wewe mkuu umejuaje kama huyo mtu ana vinasaba na kijijini. Kama alizaliwa mjini na familia yao ipo mjini, kijijini ataenda kufanya nini?
 
Na wale vilema na wagonjwa watasemaje?
 
Nilikuona kule uzi wa kubet majuzi umesema "Najua Vingi KTK Betting Ila Mnakazaaa Kunisaidia Mtaji .... An"
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ Mkuu, ulivyoniona kwenye ule uzi wa betting usifikirie mimi ni mbet. Nilikuwa nimeingia tu kwenye mjadala na kuchangia nilichokuwa najua kuhusu betting. Mimi nilichokuwa naomba ni msaada wa mtaji wa kuanzisha biashara, sio mtaji wa kubet. ๐Ÿ™
 
Kuna harufu ya utapeli๐Ÿ˜‚
Ni kweli mkuu, naelewa kabisa kwa nini unaona hivyo. Ila mimi sina nia ya kutapeli mtu wala kumdanganya yeyote. Nimeomba msaada kwa uwazi kutokana na hali ninayopitia, na yeyote ambaye hana imani nami ni sawa kabisa, simlazimishi. ๐Ÿ™
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ