Wakuu wa Kaya, hivi tatizo ni mshahara mdogo au matumizi mabaya ya fedha?

Wakuu wa Kaya, hivi tatizo ni mshahara mdogo au matumizi mabaya ya fedha?

Wakuu wa KAYA hivi mbona Hadi nae muona ana mshahara mzuri nae analalamika mshahara mdogo hautoshi hivi tatizo nini haswa?
Mshahara mdogo?
Matumizi mabaya ya fedha?
Au kuto kuwekeza?
 
1. Mfumuko wa bei
2. Utegemezi (Familia zetu za Kitanzania zilizo nyingi). Huyo unayemuona ana mshahara mkubwa inawezekana nyuma yake ana chain ya watoto wa ndugu anaowasaidia.

3. Matumizi mabaya ya fedha.
4. Kutegemea chanzo kimoja cha fedha.

Ila hayo mawili ya juu ndo muhimu sana.
 
Mshahara mdogo yes
Majukumu mengi yes

Ila kubwa ni nidhamu ya unachopata na kutegemea one source of income .
 
tatizo ni kulenga pakubwa kulikoni kinachopatikana. kuepuka kadhia hii angalau uishi kulingana na kipato chako. mathalani kama una kipato cha milioni moja usitamani kuishi kama yule wa milioni kumi.

jingine ni kutafuta zaidi ikiwemo uwekezaji wa kina. sema ulimwengu huu wa tamaa kila mmoja hujiona hana kipato wala kufanikiwa eti kwa kuwa tu hana gari kali na nyumba.

sisi wa zama za kati za mawe, kuanza kuwasha moto kwa kupekecha vijiti, na kufuga mbwa na mbuzi ilikuwa ni kipato na mafanikio vilevile!
 
Back
Top Bottom