Pre GE2025 Wakuu wa shule kumchangia fedha ya kuchukua fomu ya Urais Rais Samia 2025, hiki ni "kituko" cha kufungia mwaka

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kama mdau wa Elimu na maendeleo ya kijamii, taarifa za wakuu wa shule kumchangia Mama Samia fedha za kuchukua fomu ya Urais kabla ya mchakato husika kuanza linaleta ukakasi na maswali mengi juu ya uwezo wa kupambanua mambo wa hawa viongozi walioaminiwa kusimamia elimu ya watoto wetu.

Je, kiongozi wa umma anaruhusiwa kuonyesha msimamo wake wa kisiasa hadharani?

Je, wamejuaje kama Rais Samia atagombea 2025?

Je, wana uhakika gani chama chake kitampitisha?

Kulikuwa na haraka gani kufikia hili azimio kipindi hiki ambacho hata mchakato haujaanza?

Tuamini kuwa hili nalo ni sehemu ya kujipendekeza? Kama ni kujipendekeza, wanawezaje kupandikiza ujasiri na kujiamini kwa walimu wanaowasimamia na watoto wetu? View attachment 2847719
Nchi yetu ujinga mwingi Sana. Yaani Jamaa wamepiga pesa za shule na hakuna wa kuwafuatilia wanaona ili tuendelee kuzipiga tumpiganie yuleyule dhaifu . Wajinga wakubwa Hawa. Vichwa kama kapu la mama.
 
Ndio japokwa kuchelewa ,sasa mwezi wa 12 wanapewa za mwezi wa10[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]🪑
Zinakuwa hata hazinogi kabisa.

Enzi nasoma shule(Primary/Secondary) nilikuwa nawaona Walimu ni watu wenye maisha mazuri ila sasa naona tofauti sijui kwanini.

Kule kijijini Walimu walikuwa wanaheshimika sana na jamii yote
 
Wanapewa mkuu, wa sekondari na waratibu elimu kata 250,000/= wakuu wa shule za msingi 200,000/= nadhani na maafisa watendaji kata kila mwezi inaingia kwenye mifuko yao kutoka hazina
Sio mbaya, ila inatakiwa waamke wadai maslahi yao
 
Hii ni kutafuta kumjengea uhalali bi hadija ambaye kimsingi anatakiwa kumaliza muhula wake wa pili mwaka 2025, nasikitika kwamba uchawa kwenye taifa hili umeshakuwa donda ndugu.
 
Tatizo lipo kwa uongozi wa TAHOSSA sidhani kama walimu wakuu wote wameridhia.Hawa walimu wakuu wa shule zote za msingi na sekondari za Serikali na Private . Uongozi wa TAHOSSA unajua gharama ya fomu ya urais itauzwa bei gani au wanataka Maokoto yatakayobaki wajinufaishe
 
Kama mdau wa Elimu na maendeleo ya kijamii, taarifa za wakuu wa shule kumchangia Mama Samia fedha za kuchukua fomu ya Urais kabla ya mchakato husika kuanza linaleta ukakasi na maswali mengi juu ya uwezo wa kupambanua mambo wa hawa viongozi walioaminiwa kusimamia elimu ya watoto wetu.

Je, kiongozi wa umma anaruhusiwa kuonyesha msimamo wake wa kisiasa hadharani?

Je, wamejuaje kama Rais Samia atagombea 2025?

Je, wana uhakika gani chama chake kitampitisha?

Kulikuwa na haraka gani kufikia hili azimio kipindi hiki ambacho hata mchakato haujaanza?

Tuamini kuwa hili nalo ni sehemu ya kujipendekeza? Kama ni kujipendekeza, wanawezaje kupandikiza ujasiri na kujiamini kwa walimu wanaowasimamia na watoto wetu? View attachment 2847719
Watawachangia na nyie machadema Wala msiwaze 😁😁
 
Ndio maana kazi yao inadharauriwa na ina laana ya kiuchumi

Wengi wakijitahidi kujenga nyumba ya milioni 40 hadi 50 kwa kipindi cha miaka ishirini basi wanaridhika

Magari yao ni mengi ni ya mwaka 1998-2005

Mpwayungu was right
 
Kama mdau wa Elimu na maendeleo ya kijamii, taarifa za wakuu wa shule kumchangia Mama Samia fedha za kuchukua fomu ya Urais kabla ya mchakato husika kuanza linaleta ukakasi na maswali mengi juu ya uwezo wa kupambanua mambo wa hawa viongozi walioaminiwa kusimamia elimu ya watoto wetu.

Je, kiongozi wa umma anaruhusiwa kuonyesha msimamo wake wa kisiasa hadharani?

Je, wamejuaje kama Rais Samia atagombea 2025?

Je, wana uhakika gani chama chake kitampitisha?

Kulikuwa na haraka gani kufikia hili azimio kipindi hiki ambacho hata mchakato haujaanza?

Tuamini kuwa hili nalo ni sehemu ya kujipendekeza? Kama ni kujipendekeza, wanawezaje kupandikiza ujasiri na kujiamini kwa walimu wanaowasimamia na watoto wetu? View attachment 2847719

Nadhani Walimu nao wanahaki ya msingi kama raia wa kawaida kuonyesha Mahaba na Mapenzi wa Rais Wao

Nimechagua kuwa POSITIVE
 
Back
Top Bottom