Declaration of interest, mimi ni mwanaume ambaye kila mwaka naweza kumnunulia mwanamke wangu Gari la kuanzia 50mil, mwanamke ni viumbe wa ajabu
Katika vitu nasema nimewahi kukosea maishani mwangu ni kuishi na huyu mwanamke niliyezaa nae, hakuna amani kabisa kwenye maisha yangu kila siku ya Mungu, amani yangu inakuja nikilala usingizi na wakati mwingine nakunywa dawa au pombe kali sana ili nilale, au nitafute Mwanamke wa Burudani.
Kama uko kwenye uchumba, umezaa na mtu ikakubidi umuoe, usioe ndoa ya Kanisani wala msikitini, utaratibu wa kubariki ndoa ndio jambo bora kwenye masuala ya dini.
Ukisikia mwanaume anaacha nyumba, mali zote anamuachia mwanamke ili asihangaike na watoto huwa akosei kabisa, nimewahi kupanga niharibu namba zangu zote za simu, niwapige stop ndugu zangu nihame nyumbani nimuachie kila kitu alafu nianze maisha upya.
Ukipata mke mbaya, hutawahi upate amani hadi unakufa.