Wale ambao tunaishi na watoto wa watu na hatujapeleka hata 100 ya mahari tukutane huku

Kama utoi mahali wanachukua mtoto wao eeeh itakuaje hapo..!?
Haya ni mambo ambayo unafanya kwa koo zilizoendelea ambazo zinaelewa haya mambo.

Point ya ķuacha kutoa mahari ni kumtambua mwanamke kama mtu, si chombo, si bidhaa, mtu mwenye utu wake.

Na kama familia yake inaelewa hayo, haiwezi kumfanya bidhaa, haiwezi kulazimisha ulipe ili kuwa naye.

Inabidi uijue familia kabla ya kuoa. Ukiwa hujafanya hiyo homework, una tatizo kubwa zaidi ya mahari.
 
Kwa mwanamke gani wa kumfanyia hayo? Hawa hawa akina Sikitu? 😀

Utakuja shangaa na roho yako ukikuta boda boda anamtia.
 
Kwa mwanamke gani wa kumfanyia hayo? Hawa hawa akina Sikitu? [emoji3]

Utakuja shangaa na roho yako ukikuta boda boda anamtia.

Mkuu mimi ninapokaa hakuna hayo majina yanayojirudia. Ukisikia "Daladala" au "bodaboda", ujue matatizo matupu hapo.

Hapo ushafanya homework yako, haya mambo si ya kumfanyia mtu ovyo ovyo.

La sivyo utakuwa na tatizo kubwa kuliko mahari.

Kuna cousin wangu mmoja alikuwa anasema mambo yanayotatuliwa kwa pesa si matatizo, ni gharama tu.

Matatizo halisi hayatatuliwi kwa pesa tu.
 
Vipi kuhusu wale ambao hawajapima DNA na hivyo wanalea watoto wa watu pasipo ridhaa ya baba zao?
 
Haya mambo yaachwe kama yalivyo tu. Lipa million 1-2 inatosha sana usije onekana umechukua mtoto wao kihuni.
 
Kutunza ilikuwa unakuta kitu sealed. Wazazi wenyewe hawa wa sasa hawawezi tunza watoto. Wanawake unaoa breki pumbuz
 
Mahari ni heshima kwa mwanamke wa kiafrika mahari ni utamaduni wetu, mahari ni halalisho la ndoa ya kimila, mahari ni mapenzi mahari ni kitambulisho cha kijana kuweza kumtunza mke husika mahari........ Tutolewe mahari aisee msilete ujuaji
Mahari si heshima kwa mwanamke.

Mahari ni kumuondolea heshima mwanamke.

Unamuwekea bei mwanamke kwamba huyu thamani yake ni sawa na ng'ombe ishirini.

Na hapo mwanamme anapata sauti kwamba amemnunua mwanamke kwa ng'ombe ishirini.

Sasa wewe unakubali kumuweka mwanamke awe sawa na ng'ombe ishirini?
 
Mi ni mwanamke niko tayari kuuzwa kwa mujibu wa mtizamo wako,
 
Haya mambo yaachwe kama yalivyo tu. Lipa million 1-2 inatosha sana usije onekana umechukua mtoto wao kihuni.

Kwanza kabisa mahari hupangi wewe unayeoa, hivyo usiweke figure.

Ukioa sehemu ambazo wanaendekeza tamaduni za kijima sawa.

Lakini, hapo unaweza kabisa kuwa na tatizo kubwa zaidi ya mahari.

Unaweza kuwa na tatizo kwamba umeoa ukoo unaoendekeza mila za kijima.
 
Mahari pia ni sehemu ya interview kwa.mwanaume kumpima kama ana uwrzo.ea kulisha na kutunza huyo mwanamke.kuna makabila mengine lazima uhojiwe kazi unayofanya ya kukuingizia kipato hawaki mtoto wO aolewe.na mzururaji.mtu ambaye kipato chake.tu hana cha kueleweka

Mtu kushindwa kulipa mahari ni dalili ya waxi.kuwa ana pepo la umaskini ja sio.vizuri kuoza mtoto kwa mtu mwenye pepo la umaskini
Mahari inamtbulisha mtu.kuwa uwezo upo wa kutunza huyo mke
 
Unavyopenda ligi sasa, we tuache tutolewe mahari we ukioa usitoe full stop
Kwani wapi nimekukataza?

Naanzaje kukukataza mtu hata sikujui?

Huwezi kujadili hoja kidhahania tu kwamba hili jambo ni zuri au baya, kwa sababu hizi na hizi, bila ya ku catch feelings na kuona kwamba nakufanyia personal attack wewe kama mtu binafsi?

You as a person are not that important to me. Sikujui.

Point ya mjadala ni kuelimishana kifalsafa, kimantiki, kidhahania, si kufanya personal attack kwako.

Inaonekana hujaelewa point hii.
 
🤩🤩Uwe na wakati mzuri
 
Hoja nzima ya kwamba mwanamme ndiye analisha na kutunza mwanamke imepitwa na wakati.

Hayo ni maisha ya kijima.

Mnaishi katika ulimwengu uliopitwa na wakati unaomfanya mwanamke hana akili, ni mtu wa kulishwa na kutunzwa tu na mwanamme.

Pia, kupinga kulipa mahari si kushindwa kulipa mahari. Kuna watu wanapinga kwa minajili ya kifalsafa.
 
Hoja nzima ya kwamba mwanamme ndiye analisha na kutunza mwanamke imepitwa na wakati.

Mnaishi katika ulimwengu uliopitwa na wakati unaomfanya mwanamke hana akili, ni mtu wa kulishwa na kutunzwa tu na mwanamme.
Biblia ndio inaagiza hivyo

Kazi ya Mume kutunxa mke na familia
Biblia haipitwi na wakati hata siku moja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…