MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Nakumbuka nilihitimu chuo nikiwa umri mdogo tu wa miaka 24 kasoro miezi kadhaa. Kwa enzi zile za JK sikuwa na shida sana ya kupata ajira kwahiyo nilianza ajira kwenye sekta binafsi siku chache tu baada ya mtihani wa mwisho chuo ilikuwa Julai.
Pia tangu nikiwa chuo nilikuwa nikijishughulisha sana na madili ya town kwahiyo kiukweli haikuwa shida kupata sehemu ya kujishikiza. Ile ajira niliifanya nikiwa na malengo ya kuja kujiajiri muda sio mrefu.
Wakati naanza kazi nikasema ndani ya miaka mitano lazima niwe na masters, nyumba nzuri, gari na ule mwaka wa sita naoa. Kwa hesabu za haraka ilikuwa nikiwa na miaka 29 niwe nimefikia hizo ndoto.
Kiukweli kwenye ile miaka mitano nilikutana na dhoruba nyingi sana ikiwemo kufeli karibu kila kitu nilichojaribu kwenye biashara kwasababu ajira niliacha ndani ya mwaka mmoja na nusu.
Nakumbuka kwenye hiyo miaka mitano nilipata admission ya kusoma Masters UDSM ila changamoto ikawa ada. Kuhusu nyumba na gari nilikubaliana na ukweli kwamba haiwezekani. Nikaona nitazame suala la mke. Huko pia nilifeli.
Wakati naelekea kutimiza miaka 30 ndo angalau ramani zikaanza kunyooka. Gari nikanunua nikiwa na 33yrs ambalo sikukaa nalo sana nikauza. Nyumba bado haijaisha.
Kimsingi nakaribia 40 ila hakuna uhalisia wa zile ndoto zangu za wakati ninatoka chuo. Kwa wananchi wengi wanaona niko poa ila binafsi naona muda unazidi kuchanja mbuga na ndoto za kushika kibunda zikiwa bado kutekelezeka.
Ninawashauri wote wenye changamoto ya umri kwenda huku hawajafikia malengo wazidi kupambana. Mbona Babu wa Loliondo alitoboa akiwa kikongwe?