Epuka hiyo roho ya kujilinganisha na wengine kwa sababu kila mtu ana safari yake.
Mimi nina ma classmates wana majumba mpaka Dubai na Amerika lakini nami niko kivyangu napambana. Wengine ni vigogo huko serikalini wanajichotea tu mahela wamejenga mahekalu kila kona hapa mjini na wanasukuma ma Vogue. Na mimi hata Corolla ya mchongo sina. Na umri umeenda sana!
Ukijilinganisha na watu utapata msongo wa mawazo kwa maana lazima kutakuwa na watu wanaokuzidi tena mbali mno.
Na ajabu tukijilinganisha na wengine kamwe huwa hatujilinganishi na wengi tuliowazidi (ukiachilia mbali wenzetu wengi waliotangulia mbele ya haki). Huwa naona ni kama vile huwa tunamkosea Mungu kwa kukosa shukrani kwa kutufikisha hata hii hatua tuliyofikia...
Kama ni lazima kujilinganisha basi kufanyike kwa lengo la kujipatia motisha tu wa kupambana na si vinginevyo.
Una afya nzuri. Una gari. Unajenga...Una kazi...Bado uko kwenye 40s.
God has been good to you and you are blessed. Just keep hustling [emoji1545]