Wale ambao wana stress ya umri kwenda huku hawana chochote, tukutane hapa

Wale ambao wana stress ya umri kwenda huku hawana chochote, tukutane hapa

Nakumbuka nilihitimu chuo nikiwa umri mdogo tu wa miaka 24 kasoro miezi kadhaa. Kwa enzi zile za JK sikuwa na shida sana ya kupata ajira kwahiyo nilianza ajira kwenye sekta binafsi siku chache tu baada ya mtihani wa mwisho chuo ilikuwa Julai.

Pia tangu nikiwa chuo nilikuwa nikijishughulisha sana na madili ya town kwahiyo kiukweli haikuwa shida kupata sehemu ya kujishikiza. Ile ajira niliifanya nikiwa na malengo ya kuja kujiajiri muda sio mrefu.

Wakati naanza kazi nikasema ndani ya miaka mitano lazima niwe na masters, nyumba nzuri, gari na ule mwaka wa sita naoa. Kwa hesabu za haraka ilikuwa nikiwa na miaka 29 niwe nimefikia hizo ndoto.

Kiukweli kwenye ile miaka mitano nilikutana na dhoruba nyingi sana ikiwemo kufeli karibu kila kitu nilichojaribu kwenye biashara kwasababu ajira niliacha ndani ya mwaka mmoja na nusu.

Nakumbuka kwenye hiyo miaka mitano nilipata admission ya kusoma Masters UDSM ila changamoto ikawa ada. Kuhusu nyumba na gari nilikubaliana na ukweli kwamba haiwezekani. Nikaona nitazame suala la mke. Huko pia nilifeli.

Wakati naelekea kutimiza miaka 30 ndo angalau ramani zikaanza kunyooka. Gari nikanunua nikiwa na 33yrs ambalo sikukaa nalo sana nikauza. Nyumba bado haijaisha.

Kimsingi nakaribia 40 ila hakuna uhalisia wa zile ndoto zangu za wakati ninatoka chuo. Kwa wananchi wengi wanaona niko poa ila binafsi naona muda unazidi kuchanja mbuga na ndoto za kushika kibunda zikiwa bado kutekelezeka.

Ninawashauri wote wenye changamoto ya umri kwenda huku hawajafikia malengo wazidi kupambana. Mbona Babu wa Loliondo alitoboa akiwa kikongwe?
Natamani nifany Jambo lkn too late
 
Nyumba na magari nawaachia muyawaze😎
My biggest achievement kwangu ilikuwa na familia na Mungu alinijibu at the age of 28 nilikuwa tayari nimeolewa na watoto watatu nimemaliza kuzaa,
Mimi kwangu kitendo Cha kuwa na familia na kuzaa watoto wangu mapema kwangu ni mafanikio makubwa.
Mkuu una age gani kw sasa
 
Mm mpk kufika 2018 December Nina Kama milion 15 HV Ila baada ya hapo

Story IPO kwenye ule Uzi walio filisika ....

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Samahani mkuu imebidi nicheke japo siyo jambo la kuchekesha.

Bila shaka uko kwenye harakati za kuinuka tena. Cha muhimu ni kutokata tamaa tu na kama uzima upo mengine yote ni madogo.
 
39? Au maana 30's got no limit within 31-39.

Hupaswi kuhofu kusema ukweli. Mm Nina 41 Nina nyumba mbili Moja haijaisha ..Nina watoto kazi japo siipendi.

Kazi ninayoipenda naona kama siipendi japo natamani kitu ni Prestige tu. Hii kazi imaniudhi Sana. Nipo katika kuomba Allah niwe na maisha mazuri tu hizi kazi za tamaa zipite mbali.

Yaani I have dreams nadhani kuliko MTU yyt Yule
 
Epuka hiyo roho ya kujilinganisha na wengine kwa sababu kila mtu ana safari yake.

Mimi nina ma classmates wana majumba mpaka Dubai na Amerika lakini nami niko kivyangu napambana. Wengine ni vigogo huko serikalini wanajichotea tu mahela wamejenga mahekalu kila kona hapa mjini na wanasukuma ma Vogue. Na mimi hata Corolla ya mchongo sina. Na umri umeenda sana!

Ukijilinganisha na watu utapata msongo wa mawazo kwa maana lazima kutakuwa na watu wanaokuzidi tena mbali mno.

Na ajabu tukijilinganisha na wengine kamwe huwa hatujilinganishi na wengi tuliowazidi (ukiachilia mbali wenzetu wengi waliotangulia mbele ya haki). Huwa naona ni kama vile huwa tunamkosea Mungu kwa kukosa shukrani kwa kutufikisha hata hii hatua tuliyofikia...

Kama ni lazima kujilinganisha basi kufanyike kwa lengo la kujipatia motisha tu wa kupambana na si vinginevyo.

Una afya nzuri. Una gari. Unajenga...Una kazi...Bado uko kwenye 40s.

God has been good to you and you are blessed. Just keep hustling [emoji1545]
Mawaidha ya mzee wa 75+
Noted mkuu 😒🤛
 
Nyumba na magari nawaachia muyawaze😎
My biggest achievement kwangu ilikuwa na familia na Mungu alinijibu at the age of 28 nilikuwa tayari nimeolewa na watoto watatu nimemaliza kuzaa,
Mimi kwangu kitendo Cha kuwa na familia na kuzaa watoto wangu mapema kwangu ni mafanikio makubwa.
Exactly,
Watu wengi wana depression sababu ya kutaka maisha ambayo hata hawayahitaji kuwakamilishia furaha zao bali kufurahiwa, kupongezwa na kuonekana na watu wengine kuwa wamefanikiwa au ni watu wa maana sana. Mwisho wanapata walichokitafuta lakini bado hawapati furaha

Umebarikiwa sana kujua ni nini unachohitaji cha kwanza na kukipata 👏🏾👏🏾👏🏾🤷🏽‍♂️
 
Sasa kumbe watu mna magari na mapagale mnataka mpewe nini gunia la chawa? ndio mshukuru?

Shukuruni kwa mlivyonavyo na mna michongo

Kuna watu hapa 35 zinagonga hakuna ramani Wala mchongo wowote.

Asubuhi anatoka home hajui anaenda wapi.

Ukiona wewe umetoka home unajua unakoenda shukuru Sana.
Dah! Hapa mkuu umenigusa mimi kabisa yani. Mpaka sasahivi sielewi hatima ya maisha yangu itakuwaje, acha tu niishie hapa maana kuna wakati napata mawazo mabaya sana lakini kila nikiwafikiria wanangu roho inaniuma sana!

Kiukweli hii situation ya kuchelewa kwenye maisha ni mbaya. Acha nife kijerumani tu!
 
Kusoma sio kazi, kazi kubadirisha masomo kuwa pesa.😁
Watu wengi wapo depressed sio kwa sababu hawana pesa za kuwaendeshea maisha yao Ila kuendana na matarajio ya jamii zao. Mfano mzuri ni huo wa kutumia pesa kama kipimo cha thamani ya vitu vyote ikiwemo elimu

Ndio maana graduate asipopata pesa za kuishi life flani anajiona useless. Hii haipo sawa
 
Nakumbuka nilihitimu chuo nikiwa umri mdogo tu wa miaka 24 kasoro miezi kadhaa. Kwa enzi zile za JK sikuwa na shida sana ya kupata ajira kwahiyo nilianza ajira kwenye sekta binafsi siku chache tu baada ya mtihani wa mwisho chuo ilikuwa Julai.

Pia tangu nikiwa chuo nilikuwa nikijishughulisha sana na madili ya town kwahiyo kiukweli haikuwa shida kupata sehemu ya kujishikiza. Ile ajira niliifanya nikiwa na malengo ya kuja kujiajiri muda sio mrefu.

Wakati naanza kazi nikasema ndani ya miaka mitano lazima niwe na masters, nyumba nzuri, gari na ule mwaka wa sita naoa. Kwa hesabu za haraka ilikuwa nikiwa na miaka 29 niwe nimefikia hizo ndoto.

Kiukweli kwenye ile miaka mitano nilikutana na dhoruba nyingi sana ikiwemo kufeli karibu kila kitu nilichojaribu kwenye biashara kwasababu ajira niliacha ndani ya mwaka mmoja na nusu.

Nakumbuka kwenye hiyo miaka mitano nilipata admission ya kusoma Masters UDSM ila changamoto ikawa ada. Kuhusu nyumba na gari nilikubaliana na ukweli kwamba haiwezekani. Nikaona nitazame suala la mke. Huko pia nilifeli.

Wakati naelekea kutimiza miaka 30 ndo angalau ramani zikaanza kunyooka. Gari nikanunua nikiwa na 33yrs ambalo sikukaa nalo sana nikauza. Nyumba bado haijaisha.

Kimsingi nakaribia 40 ila hakuna uhalisia wa zile ndoto zangu za wakati ninatoka chuo. Kwa wananchi wengi wanaona niko poa ila binafsi naona muda unazidi kuchanja mbuga na ndoto za kushika kibunda zikiwa bado kutekelezeka.

Ninawashauri wote wenye changamoto ya umri kwenda huku hawajafikia malengo wazidi kupambana. Mbona Babu wa Loliondo alitoboa akiwa kikongwe?
Sio Babu tu wa Loliondo hata Joe Biden amepata u Rais akiwa na 78yrs wakati Joseph Kabila akaupata akiwa na 31 au Obama just 44 kama sikosei au Waziri Mkuu wa Sasa wa Uingereza.
 
Back
Top Bottom