Hii mada ni nzuri sana.Kwa upande wangu naona ni vyema sana kumshukuru Mungu kwa vile alivyokujalia na kutokujilinganisha na jirani yako.Muda mwingine unaweza dhani jirani yako unayemuona maybe anamiliki v8,range na mengineyo ana maisha mazuri lkn ukute anajitibu kansa,Figo inamsumbua au gonjwa ambalo hata uambiwe mbadilishane maisha hutaweza kustahimili anachopitia.Tunamkosea Mungu mara nyingi maana fikiria unasema mbn jirani yupo vizuri kumbe jirani yako ana share yake ya matatizo kwenye hii dunia.Wengine hujui utajiri wameutoa wapi maybe waliiba,kutoa kafara,kulala na mama au watoto zao.Wapendwa kuna mengi sana tusiyoyajua kwenye hii dunia ni vyema sana kumshukuru Mungu alichokujali maana mara nyingi hatujui lolote kuhusu tunalolitamani