Me I'm turning 28 kitu pekee nachomilikini hizi dreads zangu nilizofuga kwa miaka kadhaa.
Nikizikata nikauza kwa urefu wake napata laki 7.
Nikimuomba mzee aniongeze laki tatu nipate milioni naenda kulima matikiti.
Nitapanda mbegu za matikiti ambapo kwa heka moja nitapata miche 444.
Nikichukua miche 444 mara 5 kwakuwa kila mche utatoa matikiti hadi matano napata matikiti angalau 2000 kwa heka moja!
Nikiuza tikiti moja 2000 kwa matikiti 2000 napata 4000000 ndani ya miezi mitatu tu, imagine heka mbili!
Shamba nitapata la kukodi kwa laki moja tu huko Kibaha.
Mbegu nitanunua kwa bei nafuu hata laki haifiki.
Nitaajiri kibarua mmoja asafishe shamba na kupanda mbegu kwa 2000 tu kwa siku.
Pesa inayobaki nakodi mashine ya kumwagilia,
dawa ya kuulia wadudu hata elfu 20 haifiki,
pesa ya mtu wa kuangalia shamba,
Na kibarua wa kuvuna.
Haya nikilima misimu miwili tu najikuta nina 8M ndani ya miezi sita!
Yajayo yanafurahisha ngoja niende saluni!