Wale ambao wana stress ya umri kwenda huku hawana chochote, tukutane hapa

Wale ambao wana stress ya umri kwenda huku hawana chochote, tukutane hapa

Epuka hiyo roho ya kujilinganisha na wengine kwa sababu kila mtu ana safari yake.

Mimi nina ma classmates wana majumba mpaka Dubai na Amerika lakini nami niko kivyangu napambana. Wengine ni vigogo huko serikalini wanajichotea tu mahela wamejenga mahekalu kila kona hapa mjini na wanasukuma ma Vogue. Na mimi hata Corolla ya mchongo sina. Na umri umeenda sana!

Ukijilinganisha na watu utapata msongo wa mawazo kwa maana lazima kutakuwa na watu wanaokuzidi tena mbali mno.

Na ajabu tukijilinganisha na wengine kamwe huwa hatujilinganishi na wengi tuliowazidi (ukiachilia mbali wenzetu wengi waliotangulia mbele ya haki). Huwa naona ni kama vile huwa tunamkosea Mungu kwa kukosa shukrani kwa kutufikisha hata hii hatua tuliyofikia...

Kama ni lazima kujilinganisha basi kufanyike kwa lengo la kujipatia motisha tu wa kupambana na si vinginevyo.

Una afya nzuri. Una gari. Unajenga...Una kazi...Bado uko kwenye 40s.

God has been good to you and you are blessed. Just keep hustling [emoji1545]
Wewe kugombea ubunge misungwi si unaogopa wachawi,
 
Nakumbuka nilihitimu chuo nikiwa umri mdogo tu wa miaka 24 kasoro miezi kadhaa. Kwa enzi zile za JK sikuwa na shida sana ya kupata ajira kwahiyo nilianza ajira kwenye sekta binafsi siku chache tu baada ya mtihani wa mwisho chuo ilikuwa Julai.

Pia tangu nikiwa chuo nilikuwa nikijishughulisha sana na madili ya town kwahiyo kiukweli haikuwa shida kupata sehemu ya kujishikiza. Ile ajira niliifanya nikiwa na malengo ya kuja kujiajiri muda sio mrefu.

Wakati naanza kazi nikasema ndani ya miaka mitano lazima niwe na masters, nyumba nzuri, gari na ule mwaka wa sita naoa. Kwa hesabu za haraka ilikuwa nikiwa na miaka 29 niwe nimefikia hizo ndoto.

Kiukweli kwenye ile miaka mitano nilikutana na dhoruba nyingi sana ikiwemo kufeli karibu kila kitu nilichojaribu kwenye biashara kwasababu ajira niliacha ndani ya mwaka mmoja na nusu.

Nakumbuka kwenye hiyo miaka mitano nilipata admission ya kusoma Masters UDSM ila changamoto ikawa ada. Kuhusu nyumba na gari nilikubaliana na ukweli kwamba haiwezekani. Nikaona nitazame suala la mke. Huko pia nilifeli.

Wakati naelekea kutimiza miaka 30 ndo angalau ramani zikaanza kunyooka. Gari nikanunua nikiwa na 33yrs. Nyumba bado haijaisha.

Kimsingi nakaribia 40 ila hakuna uhalisia wa zile ndoto zangu za wakati ninatoka chuo. Kwa wananchi wengi wanaona niko poa ila binafsi naona muda unazidi kuchanja mbuga na ndoto za kushika kibunda zikiwa bado kutekelezeka.

Ninawashauri wote wenye changamoto ya umri kwenda huku hawajafikia malengo wazidi kupambana. Mbona Babu wa Loliondo alitoboa akiwa kikongwe?
Mtu upo hai halafu unasema huna chochote, wewe ni timamu kweli ?

Unafikiri hiyo pumzi ya uhai ni jambo dogo
 
Aisee pole sana na hiyo ndio dunia.
Sema nimekuja kugundua kwamba malengo watu tunatofautiana sana pia mitazamo jinsi tunavyoya pima maisha ndio maana wengine wanapokuona umepiga hatua wewe unajiona bado sanaaaaaa.

Binafs stress za umri pia zinanitafuna sana na kama isingekua huyu Mungu inawezekana ningetafuta ushirikina.
Kwangu kuwa na nyumba wala gari sioni kama ni hatua kivile.Nina nyumba ya kisasa tu na kagari pia nina watoto wa4 wanasoma wa kwanza anaingia form 1 mwakani na yoote haya yote nikiwa ndio nafunga 33 years.

Ila kwangu ndoto kubwa inayonifanya nijione kama nimechelewa sana ni ku establish buznes empire..hilo tu na kwa umri huu wa 33 najina kama nishazeeka tayat japo najitia moyo kwamba Mungu atanisaidia tuu...Kikubwa ni kuomba baraka na mkono wa Mungu utusaidie tusikate tamaa na kujikinai
Jf bana[emoji1787]
 
Haina shida, nakuelewa sana na kiufupi ni wakati sahihi wa kuwa hivyo na hata zaidi. Ni vile tu wengine 40+ hata nusu ya hapo bado.
Ujue kinachonitafuna sana mimi ni ile hali ambayo tumekua tukiishi nayo wengi kwamba mtu anakua na pesa kwa vipindi flan tuuu..mfano kwa mfanya kazi ni kile kipindi. Ha mishahara...katika harakat zangu za ujasiriamali kuna kipindi mtu unafulia balaa buzness zinakua sio za uhakika kila kitu kinasuasua mpaka inafika hatua elfu 20 inakua adimu 😂😂😂sasa maisha haya ndio naonava ufala kwann mtu usifike hatua unakua na pesa anytime uko full.??
 
Unamiliki gari na nyumba bado una-complain,,,we jamaa hemu piga goti chini daily mshukuru Mungu.
Kikubwa na cha kushukuru hapo ni hao watoto wanne aliowapata mapema,gari ni nini??? Si combo cha usafiri tu hajasema ni gari gani kuna gari nyingi tu zinauzwa milio 10,au nane hata tano...
 
Back
Top Bottom