Wale ambao wana stress ya umri kwenda huku hawana chochote, tukutane hapa

Wale ambao wana stress ya umri kwenda huku hawana chochote, tukutane hapa

Nakumbuka nilihitimu chuo nikiwa umri mdogo tu wa miaka 24 kasoro miezi kadhaa. Kwa enzi zile za JK sikuwa na shida sana ya kupata ajira kwahiyo nilianza ajira kwenye sekta binafsi siku chache tu baada ya mtihani wa mwisho chuo ilikuwa Julai.

Pia tangu nikiwa chuo nilikuwa nikijishughulisha sana na madili ya town kwahiyo kiukweli haikuwa shida kupata sehemu ya kujishikiza. Ile ajira niliifanya nikiwa na malengo ya kuja kujiajiri muda sio mrefu.

Wakati naanza kazi nikasema ndani ya miaka mitano lazima niwe na masters, nyumba nzuri, gari na ule mwaka wa sita naoa. Kwa hesabu za haraka ilikuwa nikiwa na miaka 29 niwe nimefikia hizo ndoto.

Kiukweli kwenye ile miaka mitano nilikutana na dhoruba nyingi sana ikiwemo kufeli karibu kila kitu nilichojaribu kwenye biashara kwasababu ajira niliacha ndani ya mwaka mmoja na nusu.

Nakumbuka kwenye hiyo miaka mitano nilipata admission ya kusoma Masters UDSM ila changamoto ikawa ada. Kuhusu nyumba na gari nilikubaliana na ukweli kwamba haiwezekani. Nikaona nitazame suala la mke. Huko pia nilifeli.

Wakati naelekea kutimiza miaka 30 ndo angalau ramani zikaanza kunyooka. Gari nikanunua nikiwa na 33yrs ambalo sikukaa nalo sana nikauza. Nyumba bado haijaisha.

Kimsingi nakaribia 40 ila hakuna uhalisia wa zile ndoto zangu za wakati ninatoka chuo. Kwa wananchi wengi wanaona niko poa ila binafsi naona muda unazidi kuchanja mbuga na ndoto za kushika kibunda zikiwa bado kutekelezeka.

Ninawashauri wote wenye changamoto ya umri kwenda huku hawajafikia malengo wazidi kupambana. Mbona Babu wa Loliondo alitoboa akiwa kikongwe?
Paragraph ya mwisho umeharibu sana...pesa za uzeeni za kingese sana, hazina vibe[emoji57]

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Kuhusu family honestly sina cha kusema brother..ila hayo mengine sasa...nimekaa juz namwambia shemej ako kwamba after 6 tutakua tunapaswa ku inject almost 10M kwa mwaka kwa ajili ya malipo ya ada tu kwa watoto hapo mengine weka kando..na hapo unasomesha vishule vya kawaida tu hiv... sasa imagine ndio na umri ushasogea na ishu hazielewi hapo liku ag 50..si unaweza ukajitundika?
😁😁😁
Uzuri wa hivi vitu, watoto watakua hadi utapofikia take off stage brother na utawapa hiyo life unayotaka (based na story ya faza). You are doing just good brother
 
hivi watu wanalsema nifanye hiki nifanye kile "nitoboe" " nitoke" sasa utoke uende wapi? upate hiki na kile then what???
mafanikio hupimwa na mtu mwenyewe binafsi, ukiona hapo ulipo sipo basi nenda unapotakiwa kuwepo! That's all
Tatizo tuna complicate sana maisha na kufanya yaonekane magumu mno!! Unakuta maisha ni ufukweni ila watu wanayafanya kama ni bahari kuu...
mi binafsi nikiwa na uwezo wa kula bila wasiwasi wa kufa njaa hapo nmefanikiwa sana tena mno. Mengine majaaliwa
 
Nakumbuka nilihitimu chuo nikiwa umri mdogo tu wa miaka 24 kasoro miezi kadhaa. Kwa enzi zile za JK sikuwa na shida sana ya kupata ajira kwahiyo nilianza ajira kwenye sekta binafsi siku chache tu baada ya mtihani wa mwisho chuo ilikuwa Julai.

Pia tangu nikiwa chuo nilikuwa nikijishughulisha sana na madili ya town kwahiyo kiukweli haikuwa shida kupata sehemu ya kujishikiza. Ile ajira niliifanya nikiwa na malengo ya kuja kujiajiri muda sio mrefu.

Wakati naanza kazi nikasema ndani ya miaka mitano lazima niwe na masters, nyumba nzuri, gari na ule mwaka wa sita naoa. Kwa hesabu za haraka ilikuwa nikiwa na miaka 29 niwe nimefikia hizo ndoto.

Kiukweli kwenye ile miaka mitano nilikutana na dhoruba nyingi sana ikiwemo kufeli karibu kila kitu nilichojaribu kwenye biashara kwasababu ajira niliacha ndani ya mwaka mmoja na nusu.

Nakumbuka kwenye hiyo miaka mitano nilipata admission ya kusoma Masters UDSM ila changamoto ikawa ada. Kuhusu nyumba na gari nilikubaliana na ukweli kwamba haiwezekani. Nikaona nitazame suala la mke. Huko pia nilifeli.

Wakati naelekea kutimiza miaka 30 ndo angalau ramani zikaanza kunyooka. Gari nikanunua nikiwa na 33yrs ambalo sikukaa nalo sana nikauza. Nyumba bado haijaisha.

Kimsingi nakaribia 40 ila hakuna uhalisia wa zile ndoto zangu za wakati ninatoka chuo. Kwa wananchi wengi wanaona niko poa ila binafsi naona muda unazidi kuchanja mbuga na ndoto za kushika kibunda zikiwa bado kutekelezeka.

Ninawashauri wote wenye changamoto ya umri kwenda huku hawajafikia malengo wazidi kupambana. Mbona Babu wa Loliondo alitoboa akiwa kikongwe?
Dunia haiko level ndivyo ilivyo
 
Kauli yangu siku zote hata kabla sijamaliza chuo

"Sitaki nianze kutafuta cha kufanya baada ya kustaafu kazi kama wengi niliowaona, nataka nijue dira ya maisha yangu toka mwanzo"

Hii kauli bado inanipa nguvu sanaa na nashukuru Mungu kila industry au skills set nilizotamani nizijue, nimezimaliza. Siishi tena maisha ya kusema ningejua ningefanya kitu flani au uwezo wangu flani ungenitoa HAPANA. Sina hiyo regret

I define my life and success in my own terms na kitu nachoogopa labda kifo tu 😁😁 lakini nikiwa hai. Lazma iwe

Najua kwa hii flow na phrases kuna watu washanijua.. Sijali lakini 😁🙏🏽
 
Epuka hiyo roho ya kujilinganisha na wengine kwa sababu kila mtu ana safari yake.

Mimi nina ma classmates wana majumba mpaka Dubai na Amerika lakini nami niko kivyangu napambana. Wengine ni vigogo huko serikalini wanajichotea tu mahela wamejenga mahekalu kila kona hapa mjini na wanasukuma ma Vogue. Na mimi hata Corolla ya mchongo sina. Na umri umeenda sana!

Ukijilinganisha na watu utapata msongo wa mawazo kwa maana lazima kutakuwa na watu wanaokuzidi tena mbali mno.

Na ajabu tukijilinganisha na wengine kamwe huwa hatujilinganishi na wengi tuliowazidi (ukiachilia mbali wenzetu wengi waliotangulia mbele ya haki). Huwa naona ni kama vile huwa tunamkosea Mungu kwa kukosa shukrani kwa kutufikisha hata hii hatua tuliyofikia...

Kama ni lazima kujilinganisha basi kufanyike kwa lengo la kujipatia motisha tu wa kupambana na si vinginevyo.

Una afya nzuri. Una gari. Unajenga...Una kazi...Bado uko kwenye 40s.

God has been good to you and you are blessed. Just keep hustling [emoji1545]
Umeandika points tupu mkuu
 
Ujue kinachonitafuna sana mimi ni ile hali ambayo tumekua tukiishi nayo wengi kwamba mtu anakua na pesa kwa vipindi flan tuuu..mfano kwa mfanya kazi ni kile kipindi. Ha mishahara...katika harakat zangu za ujasiriamali kuna kipindi mtu unafulia balaa buzness zinakua sio za uhakika kila kitu kinasuasua mpaka inafika hatua elfu 20 inakua adimu 😂😂😂sasa maisha haya ndio naonava ufala kwann mtu usifike hatua unakua na pesa anytime uko full.??
Financial freedom mkuu ni muhimu sana
 
[emoji120] Simba ..... Be blessed mkuu

Hili Jambo la kijinga sna mm Kuna jmaaa tumesoma nao Basi kila wakt wannitafuta kujua maendeleo yangu Niko Wapi nafanya nn yaani huwa sipendi jmaaa linakupigia tu na kukuambia fln Yuko HV Mara yule jamaa mwingine Ni head master Mara jamaa fln amenunua gar Sasa huyu jamaa najiuliza HV anadhani mm nitamuambia niniacho hiki au kile bas namuacha tu atiririke

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Wewe upo km mimi najiulizaga kwanini people wanapoteza muda kufuatilia life la watu wengine hasa bongo nakosa jibu kabisaaa sijui ni ujinga au ni nini isee!
 
Nyumba na magari nawaachia muyawaze😎
My biggest achievement kwangu ilikuwa na familia na Mungu alinijibu at the age of 28 nilikuwa tayari nimeolewa na watoto watatu nimemaliza kuzaa,
Mimi kwangu kitendo Cha kuwa na familia na kuzaa watoto wangu mapema kwangu ni mafanikio makubwa.
 
Masters pale udsm ilikuwa ada ya mwaka mzima sh ngapi!?

Wapo wastaafu kibao baada ya kustaafu ndo wanajenga bado sana mkuu pambana ..Nipo bro na hapa yuko 42 ndo kaanza masters mwaka huu nilishawahi kuongea nae alisema alikuwa na plan kibao na alikuwa vizuri kiuchumi ila alifirisika mpaka kurudi kuajiriwa ila gari anazo kama 3 sema pesa hana na hizo gari kazilinda maana ni mtumishi sasa amechukua mkopo...la sivyo angeziuza watoto 4 wapo msingi wote .
Ogopa sana mtu anaetumia sentence za "wapo watu..."
 
Back
Top Bottom