Wale mliokimbilia kujenga Dodoma poleni sana

Nakukumbusha tu hakuna mji duniani serikari imewekeza pekee ikaishinda majiji ya biashara. Mfano Beijing haijaishinda Shanghai, Abuja hajaishinda Lagos, Cape town na Johansburg hivyo hio ni ndoto ya alinacha.
Hapo hatushindanishi, bali tunaweza distribution angalau... sio kila mshamba wa nchii hii lazima akaishi Dsm, acha na washamba wengine wakaishi majiji yanayoifuatia Dsm.
 
Achana nae huyu msukuma wa sangamwalugeshi kaja mjini kwa lift ya treni!Dodoma aliiona pale relini tu
 
Tatizo mmeingia dar juzi ndo mnapiga kelele. Hivyo viwanja unavyonunua kwa square meter kibada wenzio tulinunua kama mashamba tena kwa kubembelezwa miaka ya 2003. Tembeni muelimike. Nyie kaeni na dar yenu mtakuja shtuka wenzenu washakuwa mabilionea
[emoji2962][emoji2962][emoji849][emoji849]
 
Nyie endeleeni kupoteza muda na dodoma, mkija dar hakuna plot mtakayo weza ishika.. sqm 1 ni elfu 45 hadi elfu 50. Kiwanja cha sqm buku uwe na kuanzia milioni 45 na kuendelea, hiyo dodoma haiwez kukua kama ilivyo pewa promo
Wa kuja mna taabu![emoji23][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]daah!mnashoboka na Dar wakati watu wazawa hatuna habarii!pole sana
 
Tatizo mmeingia dar juzi ndo mnapiga kelele. Hivyo viwanja unavyonunua kwa square meter kibada wenzio tulinunua kama mashamba tena kwa kubembelezwa miaka ya 2003. Tembeni muelimike. Nyie kaeni na dar yenu mtakuja shtuka wenzenu washakuwa mabilionea
Tena mapori hata lami hawana!!wanajionaa wajaanja!!!
 
Dodoma ya sasa sio ya zamani, nimepita last week nikakaa siku 2 aisee imebadilika sana, Dodoma imejengeka kwa kiasi kikubwa.. JPM alifanya kazi sana kuiboresha Dom

Siku hizi mpaka kuna Shopping Mall πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Ila tatizo la Dom ikifika saa 4 usiku unaweza kusema ni saa 8 usiku, gari za kuhesabu πŸ˜‚πŸ˜‚ sio kama Daslamu au Mwanza.

Dodoma imepanuka sana ukilinganisha na zamani.

Promo za Serikali ya 4 imeisadia Dodoma kupanuka na watu kuhamia huko.
 

Unadanganya watu. Haya unayosema umetunga asilimia 100
 
Watu wamejenga wenyewe then unasema mwendazake ndo kaboresha acha ujinga wewe n jitihada za watu binafsi wala sio yeye
 
elewa swali kwanza
Naona unalikimbia swali...Jibu ni kuwa; mwekezaji mkubwa wa majengo makubwa hapo Dar es Salaam alikuwa ni serikali; na mashirika makubwa ambayo yanamilikwa na serikali (NHC, PPF, NSSF(PSSSF) etc). Hao wote sasa hawatofanya tena uwekezaji hapo Dar; na badala yake wanawekeza Dodoma. Hivyo ni kuwa Dar es Salaam ya leo, itaendelea kubaki hivyo hivyo kwa miaka 5-10 ijayo. Labda kama nyinyi watu mmoja mmoja kama wewe; mtawekeza kwa vijumba vyenu vya chumba kimoja na choo nje; kule MBAGALA MAJI MATITU na BUZA KWA MPALANGE. Sasa sijui kama hizo nyumba za chumba kimoja na choo nje zitaibadili hii sura ya Dar es Salaam ya sasa?? Hapo utajijibu mwenyewe. Kwa Dodoma mambo yatakuwa ni tofauti, maana uwekezaji mkubwa wa serikali umepelekwa kwa makusudi huko (strategically). Hivyo muonekano wa Dodoma utakuwa tofauti kabisa. Hahihitaji PhD ya UDOM kujua hayo; jaribu tu ku-visualize kwa akili ya kawaida, utaona ukweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…