Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi ni mkulima tu na mkazi wa muda mrefu hapa Dodoma.Duh,umejibu Kama msemaji wa jiji la Dodoma..vyema
Hongera mkuu,umepatendea haki.Mimi ni mkulima tu na mkazi wa muda mrefu hapa Dodoma.
Vipi mbona Kama kisukari kimepanda?are u ok?Mbaba nimekuzalia Bwana ako au
Basically hali ya hewa kwa kipindi Fulani cha mwaka sio nzuri sana!! Pia ilikuwa hakuna umuhimu sana kwenye dunia ya Mtandao kuwarundika na kuweka wizara zote sehemu moja!! Kwa mawazo ya walio wengi ingependeza wizara ziwe kama ifuatavyo; Hazina DSM, uvuvi Mwanza, Utalii Arusha, Uchukuzi DSM, Misitu Morogoro, Madini Geita, Tamisemi mama LA mawizara Dodoma, Elimu Dodoma, Muungano na Mambo ya nje DSM
Dodoma hii hii ninayoijua??Dodoma ni shida.Serikali wanaibrand lakini wanachemka.Yaani ni sawa na lile kabila,wenyewe ni kuomba tu kila kukicha.Hawajishughulishi kazi ni kuomba.
Hela zinazojengwa mawizara zingefanya kazi nyengine.Wizara zishakuwepo na sio nje ya nchi bali ni nchini hapahapa.Kuanza kugongomoa miradi ya ujenzi wa mawizara
katika mji mkame na usiojibrand.
Yote kwa yote,Dodoma sio aisee, japo tunapenda tuione tunapoifikiria lakini tumechemka.Wakazi mtuvumilie tu, mji wenu ni changamoto.
Duuuh inaonekana hampajui dodoma. Nikupe mtihani tu mdogo tafuta picha ya nkukhungu walau hata wiki hii. Anzia four ways halafu njoo ulinganishe hiyo nkukhungu hiyo kimara yako kama bunyonkwa au hata kimara mwisho marufuku kuweka flyover weka mitaa yenye nyumba tuNkhuhungu
Duuh utadhan dar es salaam imejengwa na wandengereko na wazaramo. Kwa habari yako wakazi wengi wa dodoma mjini sio wagogo. Pia ni nadra sana kusikia watu wakiongea kigogo hadharanDodoma hii hii ninayoijua??
Jua la Dar na Dodoma lipi kali? Lipi linalowaka mapema asubuhi?Lile jua ni balaa linawaka mapema asubuhi kali, ardhi ina magadi ya kutosha, serikali iliyokuwa ya kizalendo haiwezi kuendelea kumwaga mabilioni ya shilingi jangwani.
Sent using Jamii Forums mobile app
Miaka 26 iliyopita kulikuwa Hamna Daladala??????Hii mada inaonesha kumbe watu wengi bado wana mtazamo hasi dhidi ya mji wa Dodoma.
Binafsi mara ya kwanza nimefika Dodoma miaka 26 iliyopita. Kweli wakati huo maisha yalikuwa magumu sana kuishi Dodoma kwa sababu zifuatazo;
Mosi, mji ulikuwa ni mfinyu mno, ulikuwa unaweza kutumia dk zisizozidi 40 ukatembea mji mzima.
Kipindi hicho hata daladala hazikuwepo.
Pili, maji yalikuwa ya shida sana kiasi kwamba tulilazimika kufukua makorongoni kutafuta maji. Hali hiyo ilichangia sana kuwepo kwa magonjwa mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa macho, kipindupindu, homa ya matumbo n.k.
Tatu, sehemu kubwa ya mji ulikuwa ni jangwa hali iliyopelekea kuwa na hali mbaya ya hewa hasa kipindi cha kuanzia mwezi Mei hadi Julai.
Nne, mzunguko wa fedha ulikuwa mdogo kutokana na kukosekana kwa shughuli za uzalishaji mali.
Kuanzia mwaka 2018 hali imekuwa tofauti. Changamoto nilizozibainisha hapo juu sasa zimefanyiwa kazi. Mji umekuwa sana na miundombinu ya kisasa imewekwa.
Dodoma kwa sasa hakuna nyumba iliyokamilika yenye kuhitaji wapangapi ikakosa wapangaji tena kwa bei nzuri ukilinganisha na bei katika miji mingine ya nchi yetu.
Hata suala la usafiri sasa hivi limeboreshwa sana. Kwa upande wa usafiri wa anga, zamani ili kupanda ndege mfano kwenda Dar au kokote ilikubidi ukodi ndege nzima ambapo nakumbuka mwaka 2011 tulikuwa na na shida ya haraka kwenda Arusha ili ilibidi tukodi ndege nzima kwa Tshs 6,000,000/ kutoka shirika la ndege la MAF. Sasa hivi Dodoma kupitia mashirika ya ATCL na PRECISION karibu kila siku kuna safari za kwenda miji yote muhimu kutokea Dodoma tena kwa bei nafuu.
Dada hivi kupitia mpango kabambe wa kuendeleza mji wa Dodoma inatarajiwa kuanzishwa usafiri wa treni za mjini (commuter) utakaounganisha maeneo yote muhimu kuanzia Ikulu, mji wa kiserikali, uwanja wa ndege Msalata, stendi ya mkoa na mjini kati.
Pia sasa hivi serikali inaendelea na ujenzi wa majengo 24 ya ghorofa 6 ya wizara mbalimbali katika mji wa kiserikali Mtumba sambamba na ujenzi wa barabara za lami katika mji huo na maeneo mengine.
Jambo pekee linalohitaji kufanyiwa kazi na mamlaka za jiji na wakazi ni kuhakikisha tunaongeza kasi ya upandaji miti na kuitunza iliyopo kwani kupitia miti hiyo sasa hivi hali ya hewa na mandhari ya mji ni ya kuvutia tofauti na zamani. Pia mradi wa kuchukua maji ziwa Victoria na kuyaleta Dodoma ukitekelezwa kama serikali ilivyoahidi mji utakuwa wenye kuvutia zaidi kwani maji ya ziwa Victoria ni baridi kupita haya tunayoyatumia sasa.
Fursa za uwekezaji katika mji huu ni nyingi kuanzia nyumba za makazi, shule za binafsi, viwanda vya kukamua/ kusindika/ kukoboa mazao kama zabibu, alizeti, mahindi, mchele, ubuyu n.k. Pia kutokana na uwepo wa vyuo vingi kuku na mayai vinahitajika sana.
Dodoma sio pa kusimuliwa, fika mwenyewe ujionee na uwekeze kabla hujachelewa kwani miaka mitano ijayo hata Gaborone Botswana itakuwa imepitwa.
Hapajui Mkuhungu(Nkuhungu) huyo...anaongea tu...Tena miongoni mwa mitaa iliyoendelea mapema ni hapo Nkuhungu.Duuuh inaonekana hampajui dodoma. Nikupe mtihani tu mdogo tafuta picha ya nkukhungu walau hata wiki hii. Anzia four ways halafu njoo ulinganishe hiyo nkukhungu hiyo kimara yako kama bunyonkwa au hata kimara mwisho marufuku kuweka flyover weka mitaa yenye nyumba tu
ila dodoma kusema ukweli bado sana bora hata singida imechangamka na kuna deals kuliko dodoma wagogo sijui wana shida ganimji wa jangwa Dom,
mkuu unafananisha nkuhungu na kimara kweli? ha ha ha ha ha ha we jamaa kuwa serious basi labda ungesema chanika hukoHapajui Mkuhungu(Nkuhungu) huyo...anaongea tu...Tena miongoni mwa mitaa iliyoendelea mapema ni hapo Nkuhungu.
Kwani Maendeleo ya tehama Tanzania bado hayajafika ?Huo utakuwa ujinga wa Hali juu sana,mutu ana shida wizara ya Afya ,mfano wako ,hiyo iwe morogoro,akifika hapo anaambiwa tunahitanji hiki kutoka wizara ya elimu,Sasa wizara hiyo iwe kagera-bukoba huko,huoni kama ni usumbufu wajinga sana huo,nilishawahi kuomba uhamisho kutoka Kwa katibu mkuu(wizara fulani-siitaji),nikaambiwa nenda Kwa katibu mkuu tamisemi,Sasa fikiria Mmoja awe mtwara na mwingine awe kigoma na wewe uwe umetokea mara usumbufu unaoupata ukoje?,vitu vingine mfikiri kabla ya kutoa comment,wizara ukizitawanya hivyo raia na maskini ndo wataumia,ukifika hapa unaambiwa nenda wizara fulani kwanza,Sasa hapo ziwe mbalimbali utakufa na shida yako
Mkuu, uko serious unafananisha Dodoma na Singida?ila dodoma kusema ukweli bado sana bora hata singida imechangamka na kuna deals kuliko dodoma wagogo sijui wana shida gani
Kimara imechangamka,Biashara nyingi...mkuu unafananisha nkuhungu na kimara kweli? ha ha ha ha ha ha we jamaa kuwa serious basi labda ungesema chanika huko
Dodoma na singida[emoji848] Serious??ila dodoma kusema ukweli bado sana bora hata singida imechangamka na kuna deals kuliko dodoma wagogo sijui wana shida gani