Wale mliooa wake zenu wakiwa na zaidi ya miaka 30 na wadada mlioolewa mkiwa na zaidi ya miaka 30 pia, karibuni kwa maoni na uzoefu wenu

NDOA ni mpango wa MUNGU katika kujenga jamii ya wanadamu watakaoishi ndani ya misingi ya kutii na kuheshimu maagizo na matakwa ya ki'MUNGU hapa duniani.

Wanadamu tupo duniani kuishi ndani ya maelekezo ya MUNGU na kufuata miiko na makatazo yake. Kinyume chake ni kujenga jamii isiyo tii maagizo na mafunzo yake yeye muumbaa.

Ndoa hutakiwa kufanyika katika umri mdogo lengo likiwa ni vijana waweze kuishi ndani ya misingi ya imani na kuachana na mambo potofu ambayo miaka ya baadae hayatakuwa na tija wala faida katika maisha yao.

Mfumo wa maisha tunaoishi huwa inakinzana sana na mifumo sahihi ya kuishi na kufuata njia za MUNGU. Hii ni kuanzia namna tunakula, namna tunavaa, namna tunagawana majukumu ya kijinsia, malezi ya watoto, namna ya kufanya uongozi wa jamii na kadhalika. Hii imetokana na wanadamu kupotoka na kutoka nje ya mafunzo kila uchao.

Wataalamu wa falsafa wanakwambia ukiishi nje ya mafunzo ya MUNGU (Nature) then utatakiwa kujijengea mfumo wako wa kila kitu ili uweze kuwa salama na kuishi maisha yako hapa duniani bila madhara jambo ambalo haliwezekani.

Kwann haliwezekani ni kwasababu MUNGU ndie anaesimamia kila jambo katika maisha yetu tunapolala na tukiwa macho siku zote za uhai wetu. Hata wale unaowatumainia kukulinda wewe ( mabodyguard,askari jeshi,madaktari, dereva wa basi la mkoa,rubani wa ndege) nao wanamrejea MUNGU ili waweze kuifanya kazi yao vema.

Sasa jiulize wewe ni nani alikupa mamlaka ya kuamua nje ya maelekezo ya yule anaesimamia na mkuu wa yote.

Si maagizo ya MUNGU kuwa binti ukae na kusubiria upate masters ndipo useme nipo tayari kuolewa au kuanza maisha. kama ingekuwa hivyo basi katika maagizo ya vitabu vyake angesema "enyi wanaume wangoojeeni wachumba wenu wamalize masters ndipo muwaoe muanze familia"

Ndoa umri wake ni ule mchanga ukiwa bado mchanga wa dunia ndipo uingie kisha kumuomba MUNGU akuongoze uishi ndani ya ulinzi wake. La hasha kama haitawezekana basi tunza heshima yako ya mwili na roho hadi pale utakapomaliza shule huku ukimuomba kila uchao akupe ruhusa na ulinzi umalize masomo salama na uweze ingia ndoani,ila sote twajua hii ni ngumu mno na ndipo hapo tunapojidhihirisha kuwa hatupo tayari kwa yale tunayomwambia MUNGU atupe.

Kwa kumalizia niseme tu, maisha tunayoishi sasa si mpango wa MUNGU bali ni maono ya wanadamu na ndio maana yamejawa na hofu,vilio,masikitiko,maumivu,tamaa,chuki,wivu wa hasara,jazba na hasira pamoja na vingine vyote vinavyokinzana na upendo na amani.

Hii ni matokeo ya sisi wanadamu kwa viburi vyetu kumwambia MUNGU kuwa hatupo tayari kufuata maagizo yake bali tutafuata maono yetu.

Na ndio maana hata ukisoma hata utaona kuna wachangiaji wanacomment kwa kiburi tu kuwa "Ndio sio kitu cha lazima"." Zaa tu mtoto wako halafu ishi single" "utaolewa tu hata miaka 55" hizi na comment nyinginezo za aina hii ni taarifa ya namna gani kiburi cha mwanadamu kinaweza kukua akajiona yeye ana maamuzi hata kuamua kinyume na muumba sababu amefyatuka na maisha.

So kwasababu tumechagua kuishi bila kushika maagizo ya muumba basi tukubali kuwa tumechagua kuwa nje ya ulinzi wake. Tumekataa kuongozwa na mafunzo ya vitabu vyake tunataka kuongozwa na viburi,maono na tamaa za akili zetu bila yeye. Basi na tusilalamike haya yanayotukuta, usingle mother, ukahaba,udangaji, wazazi kubaka watoto wao, ukatili,mauwaji,ushoga,ufisadi,rushwa,kumomonyoka maadili, ubinafsi, usaliti wa mapenzi,etc.

Ni hayo tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahaaahaahaa[emoji1787][emoji1787][emoji38][emoji38]

Shemeji yupi? Uliyenae au?[emoji12][emoji12][emoji12][emoji1787][emoji1787]
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji1787][emoji1787][emoji1787] we jamaa huwa una mdomo sana
 
Ahaaaahaaaahaaahaaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji1732][emoji1732][emoji1732]

Kubabbbk kichambo heavy[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Tunaitwa SHANGAZI ila dunia[emoji24][emoji24][emoji29]

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Kuanzia miaka 30+ ni single mother tu.

NANI AKAOE LIZEE????
 
Fact!

Fact kabisaaaa
 
Nukuu "naona sasa kibao kimegeuka nimekua huyo aunt pia aah[emoji23]."

Mkuu bado hujaolewa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…