Hello wakuu!,
Happy Sunday to everyone, karibuni kwa maoni yenu, je ni kweli ukiwa above 30yrs kuna possibility ya kutokuolewa kwa wadada? Sababu ni nini, kwani suala la ndoa linazingatia umri na si upendo baina yenu mnaotarajia kuwa wanandoa? Mliooa na kuolewa katika umri huo je kuna tofauti yoyote mnayoiona ? Maisha yanaendaje ?ushauri wenu ni upi kwa wengine?.
Kumekua na maneno ya kutishana mitaani na hata baadhi ya threads humu kwamba mdada ukiwa na 30s ndiyo basi tenaa, sometimes hupelekea wadada kuolewa tu na mtu yeyote hata wasiyempenda sababu tu ya kigezo hicho kwamba she's in her 30s na anahofia atakosa ndoa.
Zamani mtaani kwetu nilikua nikisikia wakisema aunt fulani hajaolewa hadi leo, wanamshangaa, naona sasa kibao kimegeuka nimekua huyo aunt pia aah[emoji23].
Karibuni na muwe na jpili njema...