joseph1989
JF-Expert Member
- May 4, 2014
- 17,420
- 35,765
Kuna demu mmoja aliniacha kipindi na maliza chuo nikaamua kumbembeleza nikajaribu mpaka kwa dada yake na ndiye alikuwa demu wa kwanza mtaani.Kuna wale ambao tuliachana na ma-Ex zetu na kuwafanya marafiki na kuishi nao vyema kwa kubadilishana nao Ideas tofauti za maisha
Na kuna wale ambao tuliachana nao kwa Visa, Usaliti, Chuki, Fumanizi,chuki ,uhasama na Ugomvi mkubwa kifupi ni makando kando tele
Mimi ninaye mmoja , nadhani katika ma-Ex wangu yule sikuthubutu hata kusoma dua njema ihusike kwa namna yoyote kumpatia heri katika maisha yake mpaka siku tunaonana.
Ilipita muda kidogo kama mwaka mmoja ndipo tukakutana tena hii ni baada ya kufungiana Vioo
Niseme ukweli wakati namsalimia Bidada yule,ambaye mwanzo alikuwa miongoni mwa wanawake maridhawa sana kitabia na kimuonekano , nadhani ujana maji ya moto ndiyo ulotuchemshia na kuliunguza tunda tamu la mahusiano yetu.
Binti yule wakati ule nlipomwona
Dalili pekee iliyonifanya nijue kuwa mtu huyo ni Mwanamke ni Furushi la matiti lilikuwa bila mpangilio wowote uwezao kuvutia macho MWANAUME.
Alikongoroka tofauti na uzuri wa mwanzo wakati tupo pamoja kuanzia hapo nikaanza kumuombea kwa Mungu japo arudi katika hali yake ya mwanzo.
Toka hapo SIKUBAHATIKA kumtia tena machoni mpaka keshokutwa
VIPI WEWE ULIMWONA KATIKA HALI IPI EX WAKO KWA MARA YA KWANZA???
Kila tukionana nikimsalimia hataki nikaona isiwe tabu tukapoteza kama miaka mitano, akawa kabadilika na kakonda sana nikamsalia labda nikazani kabadilika lkn wapi, sasa kuna siku tukakutana stationary, nikamwita nikamwambia hivi kwa nini nikusalimia huitikii mpaka tunanuniana akawa anaona aibu huku kainamisha sura, nikamwambia pamoja tumeachana, ila sisi ni binadamu tusijenge uadui kuna siku tutahitajiana kwani mama yake na mama yangu ni marafiki nika mwacha aendelee na mambo yake.
Ila mpaka sasa bado yupo vilevile na sasa hivi ana mtoto, halafu mdogo wake ni rafiki yangu sana na tunataniana sana ,basi huwaga na muacha aendelee na minuno yake ila mpaka sana sijaiona sababu ya kununa kwani kila mtu ana issues zake.