Wale tuliokulia kwenye familia za kishua tukutane hapa

Wale tuliokulia kwenye familia za kishua tukutane hapa

sasa, sisi wenzio ambao sio wa kishua, baada ya kupambana na shule na maisha, tumefanikiwa kupiga shule hadi tukafika majuu. kule, hizo burger ni garbage foods. yaani vyakula wanavyokula masikini vinavyonenepesha sana miili. ndio maana hata bei yake ni ndogo. na wewe hapo unaona ulikuwa mjanjaaa?
Mimi kiukweli maisha yako hayanihusu, alafu sijui kwanini maskini tuna hasira na gubu 🥹😂
 
Mimi najuta sababu nimeharibiwa future yangu na huu upuuzi .

Nimekulia dasalam sehemu ya ushuani hasa zama hizo za baba wa taifa , nikasoma nje baada ya mzee kupelekwa huko nje .

Nikala kitabu mpaka nikapata proffession yangu huku mzee akiwa bado yuko ofisini .

Tukazaliwa wawili mimi na sister yangu sikujua kupika wala kufua sio mimi tu hata dada yangu .

Nikalelewa kizungu ujinga ukanijaa nikahitimu masomo nikala kazi mapema sana hapa bongo , ushenzi ukaanza pale kazini nilipokutana na majungu nikawa mtu wa kufyumu na kupotezea namaanisha nimeacha kazi mara sita ya saba haitotokea maana mzee ashatangulia mbele za haki nikijiroga yatanikuta [emoji3]

Nilianza kunywa pombe nikiwa na miaka kumi na nne , leo hii pombe imenighalimu sana yaani kwasasa nimepelekwa vijijini sana kisa pombe kuzidi kazini mpaka nhamishiwa vijijini kama adhabu .

Mzee hakunijenga kama mwanaume ili niweze kuendeleza mali zake , kadanja kamuacha bi mkubwa naye bi mkubwa baadae kadanja hivi navyoongea sina mali ya mzee niliyorithi zaidi ya elimu tu na gari lake la kitambo na nyumba hiyo ya ushuani (nayo sister naona kama vile ataiuza alafu mimi aniteme maana naye mtata tu )

Ukiniuliza hata sielewi maana mama alisema sijui ni nini basi nimeishia tu kuwaona ujombani wakiwa na maisha bora baada ya mama kufa hivyo najua walichukua kila kitu .

Sina maisha ya kuungaunga ila sasa nawaza ningeandaliwa misingi ya kuwa mwanaume kweli basi hata leo ningekuwa na mali nyingi ila ndiyo hivyo nimebaki kupaangalia nyumbani tu kama mgeni maana hata kwa kwenda sijui ni wapi ujombani au kwa akina baba maana mimi siwaelewi na wao hawanielewi sababu wazazi hawakuwa na ukaribu na ndugu zao kabla ya kifo yaani ule ukaribu wa sisi labda kamsalimie bibi mara uncle hayo hayakuwepo

Sijui kufua wala kupika na umri huu wa sitini kasoro .
Ngono nimeanza kufanya na miaka kumi na mshua alikuwa anajua ila anaishia kusema be care .

Oyaa ngoma nimepona tu kwa vile wazungu wengi ngoma hawana sio kama hapa kwetu .

Nilileta ukishua vijijini kwa watu nikaozeshwa ndoa ya mkeka [emoji3] na sasa niko na mwanamke ila ukiniuliza niliwahi kuwaza kuoa sijui hata kama hilo wazo liliwahi nijia .

Naishi kwa akili za mwanamke maana yeye ameyajua madhaifu yangu hivyo kadi ya benki na mahitaji ya kiume yote utoa yeye baada ya kuninyang'anya kadi ya benki baada ya kunishtaki kwa wakubwa .

Kutokuwekewa misingi ya maisha halisi yalivyo kumenifanya baada ya mzee kufariki nijichanganye sana na jamii ya watoto wa uswazi yaani Keko , Tandika , Temeke , Mwananyamala , Mburahati huniambii chochote na hunidanganyi chochote .

Sijaambulia maarifa ya maisha zaidi walinifunza kuvuta bangi na mwisho wakawa machawa wangu ila sasa nilishawatema .

Nakunywa pombe mpaka sijielewi na kuacha nawaza japo sio leo [emoji848]

Ni nyumba tu iliyoko huko ushuani ndiyo natamba nayo kuwa hapa ndiyo kwetu ila ushua wa kwetu changanya na uzungu basi nilikuwa kama mbwa wa kisasa aliyekosa matunzo baada ya wazee kutangulia .

Nachofurahia kazi ninayoifanya naipenda japo kabla sijalewa nikilewa wewe pita kule .

Nipende kuwaasa wazazi na walezi , uwe na hela usiwe na hela pambana sana umlee mtoto katika mazingira ambayo yanaendana na jamii itakayomzunguka wewe ukiwepo na usipokuwepo .

Uzungu ukizidi mtoto unamuharibu leo ukiwepo na kesho usipokuwepo .

Nawasalimu wanangu wa nguvu advocate Pascal Mayalla , kaka mkubwa GENTAMYCINE , mkubwa mdukuzi bila kumsahau mwamba Abiola
Ukiacha kuwekewa misingi pia wewe mwenyewe ulizingua KIBURI ndio kimekuangusha
 
Acha
Maisha ya kishua ni yapi hapa bongo ya kuendesha hizi mitumba ya magari ya mjapani, au kuweka ligate la chuma la kusukuma, kuishi kwenye hizi nyumba zisio kua na Ac ndani, chakula chenyewe ndo nafaka hizi sembe Michele makande.....kusema ukweli sioni maisha ya ajabu hapa Tz, hapa TZ, Africa is the same na Africans are the same, isipo kua tunapishana tu mitizamo na vipao mbele, wote ni masikini tu but with varying degree of poverty, hamna mtu mwenye maisha ya kishua isipo kua ufisadi na showoff za kijinga.
Acha WIVU mzee ,wenzako Wana uwezo WA kula kuku wa kienyeji mara 10 kati ya 30, za mwezi ata kama ni nafaka je wabongo wengi wanaeza kufanya ivyo
 
Kama umenitumia sms inbox sijakujibu usiwaze nitakujib muda wowote

Nina sms nying sana najib Moja baada ya nyingine kiusahihi sitaki nijibu kwa haraka nisije kuonekana nalinga.

Kwa wale mnaotaka msaada wa kipesa nitapima kulingana na maelezo ya mtu wengine ni wagonjwa wamelazwa hao lazima tuwape kipaumbele, lakin kama unadanganya utajua mwenyewe.

Pia wale mnaotaka connection muwe wapole nitatekeleza matakwa yenu kwa uzuri unaositahil

Nitatoa msaada kadri ninavyoguswa

Ukisema kiasi furan ukaona nimetoa nusu ushukru pia, siyo kuongeza malalamiko na shida zingine. Ahsante
 
Haya sasa,

Kwa upande wangu mm nimebahatika kuzaliwa na kukulia kwenye familia ya KISHUA haswaa, nyumba,magari na chakula Cha Kila aina tena Kila siku.

Changamoto ya kuishi kwnye familia ya KISHUA ni kukosa muda Wa kuwa marafiki, pia ukitoka nje ya geti Kila mtu anakushangaa, marafiki wengi wa Kila aina wengine wezi wanakuibia vitu kama mipira nk, wazazi kukuona mtoto hata kama umekuwa, nimeogeshwa na Mama na wadada wa kazi Hadi namalizia la Saba.

View attachment 2503537
Hivi kwanini watoto wa kishua kama ni wanaume wanakuwa useless na wanawake wana sura ngumu kama baba zao? Yaani haki ya Mungu sijapata ona mtoto wa kishua mzuri maishani mwangu.
 
Zingatia acha pombe, nazani hata mkeo anaumia ila anakuvumilia tu kwa vile Hana la kufanya.

Tunza heshima yako na ya familia yako pia, usiruhusu historia yako mbaya ijirudie tena kwa kizazi kipya
Nakuelewa sana bro .
Hakika unahitaji nibadilike na wish sana ila sasa pombe ndugu yangu nitaanza kuiacha taratibu maana kwa haraka haraka sitaweza

Ni kweli shemeji yako ananivumilia tu kwa vile ananipenda vile nilivyo japo sasa umri wangu umeenda kiasi cha kuwa nahisi anawaza hata akiniacha ataenda wapi sasa zaidi atakuwa anajidharirisha .
 
Nakuelewa sana bro .
Hakika unahitaji nibadilike na wish sana ila sasa pombe ndugu yangu nitaanza kuiacha taratibu maana kwa haraka haraka sitaweza

Ni kweli shemeji yako ananivumilia tu kwa vile ananipenda vile nilivyo japo sasa umri wangu umeenda kiasi cha kuwa nahisi anawaza hata akiniacha ataenda wapi sasa zaidi atakuwa anajidharirisha .
Ndugu marehemu baba yangu alikuwa ana matumizi makubwa ya pombe, hivyo niliona athari zake. Ukiona tabu sana, basi ni pm namba yako tuwe tuna share hizo story zakoo na utaacha
 
Ngoja nikae kimya coz JF ukitaka uonekane kua ni mkweli basi jitangaze kua unapitia magumu na upo kwenye dhiki,kila mtu atakuonea huruma na kukuombea dua kisha kukutia moyo, sijui pambana utatoka tu,

Ukisema kua una good life, utasikia acha uongo,mtu mwenyewe upo kwa Shemeji yako unagombania remote na watoto wa Dada yako.

😀 😀
Sio jf tu, ni watanzania wote. Hawapendi kusikia a good side ya mtu. Wanapenda wasikie mm nimeteseka sana. Au ss wanawake hawapendi wasikie sijui mume wangu ananipenda utasikia ndoa mpya tu hiyo. I dont know why
 
Back
Top Bottom