Wale tuliokulia kwenye familia za kishua tukutane hapa

Wale tuliokulia kwenye familia za kishua tukutane hapa

Mimi najuta sababu nimeharibiwa future yangu na huu upuuzi .

Nimekulia dasalam sehemu ya ushuani hasa zama hizo za baba wa taifa , nikasoma nje baada ya mzee kupelekwa huko nje .

Nikala kitabu mpaka nikapata proffession yangu huku mzee akiwa bado yuko ofisini .

Tukazaliwa wawili mimi na sister yangu sikujua kupika wala kufua sio mimi tu hata dada yangu .

Nikalelewa kizungu ujinga ukanijaa nikahitimu masomo nikala kazi mapema sana hapa bongo , ushenzi ukaanza pale kazini nilipokutana na majungu nikawa mtu wa kufyumu na kupotezea namaanisha nimeacha kazi mara sita ya saba haitotokea maana mzee ashatangulia mbele za haki nikijiroga yatanikuta [emoji3]

Nilianza kunywa pombe nikiwa na miaka kumi na nne , leo hii pombe imenighalimu sana yaani kwasasa nimepelekwa vijijini sana kisa pombe kuzidi kazini mpaka nhamishiwa vijijini kama adhabu .

Mzee hakunijenga kama mwanaume ili niweze kuendeleza mali zake , kadanja kamuacha bi mkubwa naye bi mkubwa baadae kadanja hivi navyoongea sina mali ya mzee niliyorithi zaidi ya elimu tu na gari lake la kitambo na nyumba hiyo ya ushuani (nayo sister naona kama vile ataiuza alafu mimi aniteme maana naye mtata tu )

Ukiniuliza hata sielewi maana mama alisema sijui ni nini basi nimeishia tu kuwaona ujombani wakiwa na maisha bora baada ya mama kufa hivyo najua walichukua kila kitu .

Sina maisha ya kuungaunga ila sasa nawaza ningeandaliwa misingi ya kuwa mwanaume kweli basi hata leo ningekuwa na mali nyingi ila ndiyo hivyo nimebaki kupaangalia nyumbani tu kama mgeni maana hata kwa kwenda sijui ni wapi ujombani au kwa akina baba maana mimi siwaelewi na wao hawanielewi sababu wazazi hawakuwa na ukaribu na ndugu zao kabla ya kifo yaani ule ukaribu wa sisi labda kamsalimie bibi mara uncle hayo hayakuwepo

Sijui kufua wala kupika na umri huu wa sitini kasoro .
Ngono nimeanza kufanya na miaka kumi na mshua alikuwa anajua ila anaishia kusema be care .

Oyaa ngoma nimepona tu kwa vile wazungu wengi ngoma hawana sio kama hapa kwetu .

Nilileta ukishua vijijini kwa watu nikaozeshwa ndoa ya mkeka [emoji3] na sasa niko na mwanamke ila ukiniuliza niliwahi kuwaza kuoa sijui hata kama hilo wazo liliwahi nijia .

Naishi kwa akili za mwanamke maana yeye ameyajua madhaifu yangu hivyo kadi ya benki na mahitaji ya kiume yote utoa yeye baada ya kuninyang'anya kadi ya benki baada ya kunishtaki kwa wakubwa .

Kutokuwekewa misingi ya maisha halisi yalivyo kumenifanya baada ya mzee kufariki nijichanganye sana na jamii ya watoto wa uswazi yaani Keko , Tandika , Temeke , Mwananyamala , Mburahati huniambii chochote na hunidanganyi chochote .

Sijaambulia maarifa ya maisha zaidi walinifunza kuvuta bangi na mwisho wakawa machawa wangu ila sasa nilishawatema .

Nakunywa pombe mpaka sijielewi na kuacha nawaza japo sio leo [emoji848]

Ni nyumba tu iliyoko huko ushuani ndiyo natamba nayo kuwa hapa ndiyo kwetu ila ushua wa kwetu changanya na uzungu basi nilikuwa kama mbwa wa kisasa aliyekosa matunzo baada ya wazee kutangulia .

Nachofurahia kazi ninayoifanya naipenda japo kabla sijalewa nikilewa wewe pita kule .

Nipende kuwaasa wazazi na walezi , uwe na hela usiwe na hela pambana sana umlee mtoto katika mazingira ambayo yanaendana na jamii itakayomzunguka wewe ukiwepo na usipokuwepo .

Uzungu ukizidi mtoto unamuharibu leo ukiwepo na kesho usipokuwepo .

Nawasalimu wanangu wa nguvu advocate Pascal Mayalla , kaka mkubwa GENTAMYCINE , mkubwa mdukuzi bila kumsahau mwamba Abiola
Wao ni wao thanx bro ,dah imenigusa sana,kikubwa usikate tamaa na usikubali watoto wako wapite njia yako,pole sana mkuu
 
Huyo huwa ni mbishi mbishi kila thread, pia naonaga kakaa kishari shari.

Inanituma kupata picha yake kama vile maza mmoja mwenye sura mbovu kweli kweli, pia napata picha ni kama vile aliolewa na kuachika au hakuwah kubahatika kuolewa kabisa, hana mtoto (tasa).

Naenda mbele zaidi namuona kama vile ni mmama ambae kwenye ukoo wake haelewan karibia na 90% ya ndugu zake, sababu tu ni mawazo yake mwenyewe kujiona hahitaj kuhusiana na mtu ili aishi, pia wazo la mwanamke kujiamini na kuweza lilikita kwake nguzo.

Mwisho namuona kama mmama ambae sometime anajutia lifestyle yake, anaweza kukaa ndani akaliaaa halaf roho inamwambia badilika kidogo uishi na watu, ile akijaribu tu kubadilika anajikuta anashindwa na kuharibu zaidi maana ashazoea.


Hii hutokea hata Jf hujiapiza ya kuwa sitakaa nikoment Jf tena ila ndo hivyo anajikuta yupo mkiwa inabid aongee na watu asiowaona wala kuwajua, katika yote hayo stress na tabia zake za kuwavuruga anajikuta zinamwandama.

Nimechora picha tu wadau
Umemaliza kuchora picha yako?

Haya sasa rudi kwenye mada.

Watoto wa kishua hawana fikra za kuchora kijinga hiyo. Unaobesha ushua na wewe ni tofauti kama nyuki na nzi.
 
Kuna jamaa yangu mmja hivi alifiwa na baba yake...
2 huyu jamaa alipata matatizo kidogo ki afya yaliyomfanya akae hospal kwa muda mrefu
Baadae huyu jamaa yangu mzee wake alifariki ,kutokana na aina ya familia ile ilivyokua inaendeshwa ..naweza kusema baada ya yule baba kufariki ile familia iliyumba kidodo +watoto wengi+ wanasoma shule za ghali
Hivyo huyu jamaa yangu alichukuliwa akaenda kuishi na jamaa mmja ambae ana kampuni zake binafsi
Kwa iringa yule jamaa anaishi kule wanapokaa matajili wengi wa mkoa + wafanyakazi wengi wa serikali
Of corse jamaa ana hela na pia mke wake ni manager wa shilika moja mjini hapo hivyo unaweza pata picha ya familia hiyo
Kwasababu hata hapo nyumbani kwake ni pazuri sana (ushua mwingi)

Kwa bahati mbaya pc yangu ilipata shida kidogo kwenye hard disc ,hivyo nkawa nahitaji kumpa aniangalizie shida ni nini sababu jamaa anazijua vyema
Nkaelekezwa hadi nyumba ilipo nkafika akanipokea

Haoo tukaingia ndani ya gate ...pale nje palikua na eneo la kukaa pana kama kivuli hivi pemben ya parking
Nkakaa pale nkamuambia yeye aingie ndani aendelee tu na kuitazama me nko hapo nna msubili(nlikua nachezea simu yangu wakati huo)
Baada kama ya dk 20-25 hivi jamaa akatoka akasema kuna namna anafanya hivyo twende ndani tukakae huko ... coz Hata hivyo pc ilikua na passwords

Nlisita kidogo kwenda ila nkainuka tukaanza kupanda ngazi kuingia
Nkavua mibuti yangu (napenda sana boots) tukaanza safari ya kukatisha sebule kubwa kama darasa kuitafuta korido tuzame chumbani
Mwenzangu yuko mbele me nko nyuma yake kama siafu[emoji28][emoji28] paapu !!! Tukakutana na mama mjengo kordoni akaniangaliia nmevaa shat kubwa kubwa hiv na cape akaona nini hili[emoji848][emoji848]
Akauliza mnaenda wap?
Wakati jamaa anaanza kujibu tu yule mama
ALINISHIKA BEGA NA KUNISUKUMA AKINITAKA NITOKE NJE!![emoji21][emoji21][emoji21]
Hi ni moment mbaya iliyojihifadhi kwenye akili yangu
Hua najiuliza sana alinionaje? Au alinitafsiri vipi yote anajua yeye
Nlipofika nje nkamtext jamaa anipe tu pc yangu niondoke
Japo ilikua kwenye progression ya kufanya mchakato wa window ila nliamuru aizime niondoke pale
Nkainuka na kuondoka huku sina raha

Wewe mke wa E....E kelphin nakumbuka dhalau uliyonionesha
Kwa hakika ya bidii yangu najua ntafiki Na pengine hata kukuzidi mafanikio yangu
Ila kamwe siwezi kumfanyia yoyote kama wewe ulivyo fanya kwangu
Nmekusamehe.

Ilikua 2019!
 
Back
Top Bottom