Nimemaliza STD Seven mwaka 1997 kwenye shule mojawapo wilaya ya Kinondoni. Siku matokeo yametoka tumekwenda wilayani na marafiki zangu tumekuta watu wameshajaa kwenye ubao wa matangazo hata nafasi hakuna.
Kuna dogo mmoja namfahamu alitangulia ile kuniona tu akaniambia "Mwamba umepasua Azaboy umekwenda" akimaanisha Azania Sekondari. Aisee sikuamini nilipambana kwenye ule umati hadi nikaona jina langu, nilifurahi sana.
Kuna mwenzetu mmoja tulikuwa nae ametafuta jina halioni na alikuwa kipanga darasani, alitafuta jina lake hadi alikata tamaa. Kumbe kachaguliwa Mzumbe vipaji pekee kiakili, kuja kuona jina alishangilia kama Mwehu.
Kipinid kila Dar es salaam ilikuwa na shule za sekondari za serikali chache sana.
1. Azania- wavulana tupu
2. Jangwani- wasichana tupu
3. Kisutu- wasichana tupu
4. Zanaki- wasichana tupu
5. Forodhani- Mchanganyiko
6. Kibasira- Mchanganyiko
7. Kambangwa- Mchanganyiko.
8. Pugu
NB! Tambaza ilikuwa ni A-level tu (kuanzia mwaka 1994)
Pata picha Dar nzima wanafunzi wanagombania nafasi kwenye hizo shule ushindani wake ulikuwaje.
Asilimia kubwa tulitegemea Tuition ili kufaulu bila hivyo ni ngumu kutoboa.
Tuition maarufu za wanafunzi wa shule ya msingi wilaya ya kinondoni kipindi kile zilikuwa;
1. MT Zungu- Sinza,
2. Dani - Mburahati,
3. Boniface Ibunga- Mabibo.