Wale tuliomaliza darasa la 7 mwaka 2000 kurudi nyuma tujikumbushe ilivyokua siku matokeo ya la 7 yanatangazwa

Aisee......
 
Elimu ya 2000 kurudi nyuma ilikuwa tough sana. Yani darasa lenye wanafunzi 45 wanachaguliwa wawili au watatu tu na hapo umekaza ile ile.
Siku hizi shule za CCM, mtu mpaka anamaliza std 7 hata jina lake kulisoma ni shida lakini nae anafaulu.
Wanapigwa kijiko siku ya paper.
 
😲😲😲😲 ivi humu kumbe kuna wengine wanajitoaga ufahamu afu Ni watu wazimaaa🙆🙆🙆🙆,huo mwaka hata shule ya msingi sijaanza.
 
Ilikua heshima sana kufaulu kipindi hicho...Wilaya nzima shule ya sekondari ni moja tu,ukifaulu unafahamika...mitihani ilikua 3 tu na inafanyika siku 1.
 
Hakika mkuu mie nilihitimu la 7 mwaka 1995 Hali ilikuwa mbaya Sana.
 
Hakika mkuu mie nilihitimu la 7 mwaka 1995 Hali ilikuwa mbaya Sana.
Nchi ilikuwa maskini kinoma ndugu yangu. Hizo ndo enzi kwenda Mwanza kutokea Arusha mnalala njiani. Dar - Mtwara ni safari ya wiki nyakati za mvua. Umaskini ulikuwa umekithiri.
 
Kilikua kipindi cha hovyo sana, tushukuru sana utandawazi
 
Kipindi hicho kulikuwa na kufaulu na kutofaulu. Miaka hii kuna kuchaguliwa na kutochaguliwa!
 
Sahihisho, Tambaza ilikuwa A level tu kuanzia mwaka 1996.
 
Nyakati ngumu sana miaka hiyo,mock unapasua vibaya National unapigwa chini nadhani ndo kipindi cha biashara ya majina waliofaulu inaangaliwa status ya familia ikoje nani aende nani asiende,ile ilikua sio kufaulu bali uchaguliwe unafaulu na hauchaguliwi
 
Shule za vijijin alikuwa anafaulu moja au wawili
Sio kufaulu ni kuchaguliwa,unafaulu kufika wastani lakini hauchaguliwi kulingana na mahitaji ya shule ni chache wanaangalia waliozidi wastani zaidi,ndomana class seven wa miaka hiyo ana compete na four wa miaka hii
 
1994 tulichaguliwa wawili shule yetu. ila ckwenda kusoma nikatorokea Nairobi.
 
Hongera Alumni mwenzangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…