Wale tuliomaliza darasa la 7 mwaka 2000 kurudi nyuma tujikumbushe ilivyokua siku matokeo ya la 7 yanatangazwa

Kuna mtu matokeo yalitoka akaona jina lake limetoka wilayani ila kesho yake majina yamekuja kubandikwa kwenye kata yao halipo. Ilikuwa kilio. Bahati nzuri mjomba wake akamfadhili kwenda private school.
 
Hivi matokeo ya miaka ya nyuma yanaweza patikana online kweli . Maana page za necta kuna miaka hakuna
 
We ni Getman Mwandemele nini?!!!!
Uliwakuta kina Kunambi, Kachingwe Kaselenge (r.i.p), Kadelya na Mwampaja?!!!!!
 
Sisi wa early 80s tuna comment wapi?
 
Second Selection iliniokoa .2000-Kahama .Wilaya nzima shule ya Sekondari ya serikali ilikuwa moja na mbili za private.Vijana wawili tu darasa letu ndio walienda shule za bweni nje ya mkoa .Mmoja marehemu ,mwingine anazurula tu Ulaya.Si haba na mimi nakula sahani moja na mashehe huku mkoani.
 
Ulimalia 99?
 

Daah mkuu hali ilikuwa inatisha. Mimi kti ya darasa lote tulichaguliwa wanne tuu. Alafu matokeo yanatolewa wilayani na sisi kijijini ni umbali wa 20 kms. Tuliletewa matokeo na mwalimu alioyeenda mjini. Kipindi hicho nikikatiza pale kijini nilikuwa naheshimiwa na kila mtu yaani ilikuwa vibe fulani mtaani ilikuwa gumzo. Nakumbuka siku ya kwenda form 1 wenzangu tuliokuwa darasa moja ambao ni majirani walikuja kuniaga siku naenda shule wakaniletea zawadi kila mmoja alinipa penseli kalamu na daftari. Kati yetu wanne wawili waliiishia form 2 wakaacha shule. tukabaki wawili. form four mwenzangu akafeli alikuwa mtu wa mishe mishe flani hivi wazazi wake walikuwa watumishi so dogo akawa anajiona matawi ya juu hajali sana kusoma. Mimi nikapata div 1, nikasonga form 5 na hatimaye chuo.
 
Hongera sana. Kiukweli ilikuwa ni huzuni kubwa sana kwa wale wanaokuwa hawajachaguliwa... mimi ninaamini kuna watu wangepata nafasi ya kuendelea wangekuwa wasomi wakubwa nchini. Ndo maana huwa nakwepa sana mambo ya kukutana kwenye party za watu mliowahi kusoma pamoja kwa sababu kwa wale ambao hawakuweza kuendelea mbele na bahati mbaya maisha pia yamewapiga inakuwa kama mnawanyanyapaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…