Wale tuliosoma Makongo Secondary School tukutane hapa

Wale tuliosoma Makongo Secondary School tukutane hapa

Enzi hizo bila kufikisha wastani 41 huingii kidato kinachofuata mnajikuta hadi fomu four mnabaki 200 kutoka wanafunzi 1000 mlioanza fomu one...ilikuwa hatariiiii
 
Enzi form 3H1, 3H2, 4H1 na 4h2 hao walikuwa ni vipanga ADDITIONAL MATHEMATICS kama kilaza husogei kabisaaaaa
 
Makong 2004~2006 jamaa yetu moja kama Hamed Sagule juzi kapatwa na tatizo. Ni moja wa wale wazee wasiojulikana waliopigwa risasi na mfanyabiashara wa Tarime Peter Zakaria. Yeye alipigwa ya mguuni.
 
Siyo kweli mie nimemaliza F4 1994 kulikuwa hakunA hata nafasi ya kuvuta bangi na tulikuwa tunajisomea shule ya msingi makurumula,acha uongo toto lako miaka hiyo lilikuwa vutaji toka nyumbani kwako,Makongo hukuweza kuilinganisha na Jitegemee kwa nidhamu miaka ile
Heshima yako Ndugu Makongo ya mwaka 1994 ilikua bora sana katika kila nyanja nidhamu na matokeo huyo Mdau mtoto wake alikua mtoto wa mama ndiyo maana alishindwa kusoma pale.
 
Inasemekana mlikuwa mnavuliwa sana kaptula pale Makongo ni kweli? Nilisikia Story za pale nikasema sipeleki mdogo wangu pale.
 
Makongo High School...Elimu ni Ulinzi
 
Major Mayebe....kuna siku huyu afande alikua ana watafuta watoro,kuna jamaa aka ruka senyenge huku nyuma karibu na nyambizi kwenda mbuyu wa kota,afande mayebe hakupata tabu alishika alama ya viatu vya jamaa aka muacha msela aliruka kavu ya mbele asikamatwe.kesho yake Mayebe alipita kila darasa shart wanaume wote kuinua miguu juu kutazama alama ya viatu hadi alimpata jamaa akampa elfu kumi na uongoz wa skauti alionesha ukakamavu
hahaha [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Aisee Senkondo ndio yule jamaa wa misosi au...?. Huyu Afande Master nilimuacha na nyota 2 alikuwa mrembo lakini akikutia mkononi babake, hatari.

Kuna jamaa alikuwa anaitwa Issac tulikuwa nae bweni mshkaji alikuwa DAH acha nisiseme tu mtakuwa mmeshaelewa walengwa.

Ilikuwa ukipelekwa 1MP aisee ukirudi unaambiwa kabisa kapumzike bwenini usiingie class maana kipondo utakachopata pale acha tu.

Namkumbuka Salama Jabir na FILA yake aisee.
Senkondo huyo huyo wa MISOSI mikwara kibaooooo....Isaac alikuwa anaitwa Isack Peter alishiriki hadi miss khanga party kilimanjaro hotel pool side

Salama alikuwa anaforce basketball
 
Heshima yako Ndugu Makongo ya mwaka 1994 ilikua bora sana katika kila nyanja nidhamu na matokeo huyo Mdau mtoto wake alikua mtoto wa mama ndiyo maana alishindwa kusoma pale.
Nakumbuka kuna dogo mmoja wa kiarabu aliletwa na baba yake f1 akitaka dogo anyoke baada ya kishindikana kote ma alifuata mstari baada ya kukabidhiwa chacha na miraji,kila aking'aa kwao tu ni adhabu kwenda mbele,alinyooka!!
 
Senkondo huyo huyo wa MISOSI mikwara kibaooooo....

Hahahahah, Staff Surgion.

Isaac alikuwa anaitwa Isack Peter alishiriki hadi miss khanga party kilimanjaro hotel pool side

Hatari sana kiongozi jamaa tulikuwa room moja Bweni la Mkwawa unakumbuka kuna siku alishameza vidonge alitaka kujiua mkuu...?. Hahah.

Salama alikuwa anaforce basketball

Hahah, mzee wa kusaga na kukoboa. Lol.
 
Makongo enzi hizo ilikuwa kituo cha taaluma, sanaa na michezo...akina Marehemu Chifupa, Daz Nundaz, Bon Crewz akina Eazy Mchwampaka, Salama Jabir, Mishi Bomba, Irene Ngowi nk kwenye kikapu sasa akina Gwantwa, Mpoki, Salum Kaindu, Kapwapwa, Mwaipungu, Gunze, Mlekwa, Jacob nk ilikuwa kwere kisanga na nususu

Easy M alikuwa na mshkaji wake mmoja hivi anaitwa Muddy Machafuko alifungwa miaka 15 jela aisee ila ameshatoka tayari. Jamaa alikuwa mwembamba flani hivi black.
 
Duuuu huyo jamaa alikua hatari tupu ukimkuta kwenye 18 zake.
Kioindi chetu tulikuwa tunasoma na maafande akiwamo Afande Miraji siku moja wakakosea karatasi zao za matokeo zikaja na zetu darasani Miraji akiwa ameata sifuri mmoja wetu akachora sifuri na masikio kwenye karatasi ya matokeo ya Afande Miraji zikarudishwa kwa mwl wa hesabu,alikuja Afande Miraji na zigo la fimbo akasema "leo nitawachaoa bakora hadi mik***u yenu iwake moto iwe myekundu kama ya kicheche iwe inaoiga dimu kama taa ya indiketa ya gari"

Mazee tulikula bakora f4 "science" kudadeki tukasomba maji toka makulumla kujaza drum halijai kumbe limetobolewa
 
Easy M alikuwa na mshkaji wake mmoja hivi anaitwa Muddy Machafuko alifungwa miaka 15 jela aisee ila ameshatoka tayari. Jamaa alikuwa mwembamba flani hivi black.
Eeeh namsoma Muddy mzawa wa kawe jina lingine alikuwa anaitwa BABU WA CHIGA mweusiiiii na kigugumizi chake...

Pia kulikuwa na baharia mwingine ana buti kubwa akitembea inaanza buti mwili unafuatia alikuwa anajiita PEACEMAKER hhaaaa hhhaaaaa
 
Alikuweoo VAN DAME miaka yetu sijui yuko waoi now,makonda walikula nakozi sana kutoka kwa huyu jamaa waliootuzuia tusioande daladala
 
Back
Top Bottom