Wale tuliowahi kucheza chandimu tukutane hapa tujuane

Wale tuliowahi kucheza chandimu tukutane hapa tujuane

Nilikua naiambia team yangu nzima wapande mbele halafu huku nyuma waniachie mimi tu,

Nilikua natembeza buti,mpaka forward za team pinzani zilikua zinarudi nyuma kuungana na mabeki wao.
Kumbe na ulikuwa na guu la hivyo😁
 

Attachments

  • zumbekhan_20251225_1.jpg
    zumbekhan_20251225_1.jpg
    100 KB · Views: 15
Nilikuwa zidane wa kitaa bila ya mimi watu hawachezi.. nishakula sana mikwaju kisa chandimu.
Kuna moja hiyo, watu wamekuja kunitorosha madrassa, chama liko robo fainali, zawadi mchele na kuku chama lishakufa goli 2, watu mbona walikuja madrassa wakasingizia wameagizwa toka home, nahitajika mara 1, aisee natoka wana wananiambia breki uwanjani, chama lishaloa chuma 2..
Nafika navua kanzu, nabaki na bukta tunachomoa chuma 2, kisha ya 3 napachika mwenyewe...
Sasa mimba haina siri.. tunarudi mtaani shangwe nyingi, full kuimba nini, kunitania, siri ikavuja mie ndio shujaa wa leo, na wale makomqndo vipensi, wazee wa CIA waliokuja kunichomoa pale, wakamwaga siri walivyonipata, alooh, taarifa zikafikq home, usiku ule nikachezea sana mikwaju, kesho yake napo madrassa taarifa zimemfikia ostadhi nako nikala mikwaju.. 😂🤣
🤣🤣🤣🤣
 
Chandimu namkumbuka mwanangu rama mniga sijui hata yuko wapi.. fundi sana wa boli mguu wa kushoto, mudi mafua fundi mnooo, anacheza huko kamasi zinamtoka wakati mwingine nae sina taarifa zake.. doto kifyeke(apumzike kwa amani) peter mambwa, huyu nilisikia aliuwawa sina hakika.. sefu, zama golikipa mama yake alikuwa anauza sambusa tamu saaana, hilo chama mie funga kazi hapo..
Kurasini shimo la udongo hiyo...
Kila kiwanja tunatimba
 
Kitu pekee nilikosa ni nguvu za kupiga mashuti, sikuwa mpigaji mashuti makali ila mabeki chamoto walikuwa wanakiona, timu sana, kimbiza mnoo, ni mwendo wa kuondoka na kijiji tu
 
Shule ya msingi tulikuwa tunachanga 100 kila timu afu kinapigwa timu itayoshinda inabeba pesa

Ule ulikuwa sio mpira ni vita ile ilikuwa hakuna timu inakubali kupoteza 100 yao kirahisi aisee pira linapigwa mpaka mda mwingine ugomvi unatokea
 
Nakumbuka nilipiga ndole mguu wa mwenzangu kidole gumba kikapinda kulalia juu nilipiga kelele za maumivu.

Mwamba mmoja akaja kakishika vuta kwa nguvu kikarudi sehemu yake sio poa
Mi nakumbuka jamaa mmoja alinifanyia uhuni kwa kunirushia jiwe fulani lenye umbo kama la mpira. Aliniambia Mpira huo akarusha, mimi nakipokea kama lilivyokuja, kilichotokea usikiulize.
 
Back
Top Bottom