Wale tuliowahi kuishiwa nauli katika mishemishe tukutane hapa tuelezee tulifanyaje tukapata nauli

Wale tuliowahi kuishiwa nauli katika mishemishe tukutane hapa tuelezee tulifanyaje tukapata nauli

Kategele

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2017
Posts
1,086
Reaction score
2,533
Ni mida ya jioni nashuka kwenye boti ya Azam kutoka bongo Islamic state (Zanzibar).

Mfukoni nimebakiwa na Shilingi mia tano huku Safari yangu inabidi nielekee Mbezi Kimara, simu imezima chaji lakini pia safari yangu toka Bongo Islamic state ikiwa ni ya shida maana nilienda kiutafutaji huko Zenji nimefika Zenji ikawa magumashi nikaamua kugeuza dsm baada ya kukosa mishe na sehemu ya kukaa.

Niliposhuka kwenye boti nikatembea mpaka mnazi mmoja huku nawaza nafikaje Mbezi.

Basi nikasimama pale Mnazi najiuliza hapa nimuombe nani daah nikakumbuka katika mishemishe zangu mjini hapa nilishwahi kutana na watu mbalimbali wamepungukiwa nauli na unakuta yupo smart kimuonekano anakuomba umuongezee nauli nikawa nafikiri Ni matapeli.

Leo nami nikasema hamna namna hapa nimueleze mtu yeyote anisaidie japo elfu moja ili niongezee nauli.

Basi nikamuona kijana anaongea na simu pale baada ya kumaliza nikamface nikamweleze shida yangu mshikaji akazama mfukoni akanipatia elfu moja nilimshukuru sana yule kijana hakika umeniokoa Mungu akubariki sana.

Hakika watu wema bado wapo kijana umenisaidia sana.​
 
Mkaka uliyenisaidia nauli kutoka mbez hadi kibaha Jah akubariki sana na akuongezee mafanikio zaidi. Sitasahau ile siku wallah hadi nafukiwa chini. Acha tyuuuh [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Ilishawahi kunikuta hiyo nimepanda basi nauli 700 Mbezi-Kibaha,nimefika mlangoni konda anachukua hela, kujisachi mfukoni nikakumbuka pochi nimeacha kwenye suruali nyingine, ikabidi nizuge kuna jamaa yuko chini ana hela zangu, ile kushuka ikawa kama bahati kuna jamaa namjua anakatiza, nikamuelezea akanipa buku mbili, ila inafikirisha sana hiyo situation, akili huwa inafanya kazi kwa kiwango cha juu sana kutafuta solution ili kukwepa aibu.
 
Niliishiwa nauli Tabora, nikaenda asubuhi stand, nikamwambia conductor kuwa Sina nauli ila itatumwa baada ya muda mfupi, nikawa nayeyusha yeyusha Hadi tukafika Dodoma Mwisho wa Safari, nikasepa zangu
Ilishawahi kunikuta hiyo nimepanda basi nauli 700 Mbezi-Kibaha nimefika mlangoni konda anachukua hela,kujisachi mfukoni nikakumbuka pochi nimeacha kwenye suruali nyingine,ikabidi nizuge kuna jamaa yuko chini ana hela zangu,ile kushuka ikawa kama bahati kuna jamaa namjua anakatiza nikamuelezea akanipa buku mbili,ila inafikirisha sana hiyo situation,akili huwa inafanya kazi kwa kiwango cha juu sana kutafuta solution ili kukwepa aibu...
 
Umekula nauli wenzako wote wanaondoka, umebaki na wajinga wenzako hostel nzima mpo kuzuga tu ooh na issue hapa Sikh mbili hizi nadhani kesho kutwa taondoka inafika hiyo siku upo tu,

Unapambana uku na kule unapata nusu nauli kwakua unatoka bukoba unaenda dar na nauli uliyonayo inaishia singida unamua liwalo na liwe unakata ticket ya bukoba to singida safari inaanza mkifika singida ushuki, unabana, kutoka singida to dar wewe in maombi tu konda asikumbuke Mara mpo Dodoma unashukuru, Mara morogoro unasema asante mungu Mara mbezi mwisho unasema ubarikiwe yawe Mara ubungo unasema amen

Ni mapito ila yametujenga sana tena sana
 
Nili print kutoka Kariakoo mpaka Kinondoni Studio.

Ilikua ni utoto, hela niliimaliza kununulia mazaga huku naona kabisa ikiwa inaisha, sababu nilikua mdogo na sijawahi kupata shida yoyote ya kiuchumi, basi nilihisi mtoto mdogo hawezi kua na shida popote wakubwa wakamuacha..

Yani niliamini tuu wakiniona natembea kwa mguu wataniuliza halafu nikiwaambia nitapata msaada...kuomba niliona aibu sana, lakini pia inahitaji timing la sivyo nita aibika zaidi.

Shaaabash, labda wakubwa wa peponi.

Nikaenda kwenye duka la Anko (ilikua nikienda na bimkubwa hua tunapitia hivyo nikawa napafahamu) kufika kashafunga maana ilikua 12 jioni,
Nikaenda kwa rafiki yake mzee, kufika napo chenga.

Sasa hapa ndio utoto ukaanza kunitoka,

Kumbuka hapo kinachonitesa eti ni Sh 100 ya nauli ya mwanafunzi, na kilichonipeleka k.koo ni kwenda mchikichini kununua notes na mazaga mengine ya shule

Hela iliyobaki ndio nikaitumia kipuuzi.

Kuomba nako nahisi aibuuu,

Kwa ufupi Nikakanyaga raba, Mbaya zaidi njiani nikakutana na vibaka wakapita na yale mazaga yote ambayo ndio yaliyonifanya ni nitembee (ilikua nguo na viatu) halafu wakaniachia yale mahitaji yaliyonipeleka Kariakoo(vitabu, daftari n.k) tena walitaka wapite na begi lote ila sijui wakashauriana nini, basi mmoja akaniita halafu akanirushia begi maana nilishaakimbia.

Kwa ufupi nilikaribishwa ukubwani kwa Tanzania Shilling Mia moja( 100).
 
Mkaka uliyenisaidia nauli kutoka Mbezi hadi Kibaha Jah akubariki sana na akuongezee mafanikio zaidi. Sitasahau ile siku wallah hadi nafukiwa chini. Acha tyuuuh [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
Ina Mana hakukuomba namba ya simu? Huyo jamaa ana walakini
 
Nimetoka Dar nimeahidiwa tumiwa nauli, nikazama Darlux la Arusha nikamwambia Konda mpaka Chalinze nauli fresh!

Kibaha hola, naanza tetemeka, sina vocha sina kitu, wala message, aliyeahidi kimya, nikashushwa chalinze, nikatafuta mahali nikakaa!

Nimekaa mpaka saa 12 sijawa, sijanywa sina Vocha’s sina kitu, akatokea Mzee akanambia Kijana Nimekuona toka asubuhi shida nini?

Nikamweleza, akanambia chukua bag twende, kudadadeki, kanipeleka Guest kalipa 25,000/- nikaanza ogopa, akanipa cash 40,000/- akanambia Safari njema kesho!

Kaondoka, nikasema hapa yaweza kuwa msala siamini amini, cha kwanza nikahama Chumba, cha pili nikaenda tafuta chakula!

Sikuwahi mwona tena yule Mzee mpaka Leo wala hakurudi!
 
SHINYANGA TO KIGOMA kwa mguu hii sitaisahau, pia tanga to dar mpaka dar to msumbiji. hizo sitazisahau, nikipata muda nitaleta uzi.
 
SHINYANGA TO KIGOMA kwa mguu hii sitaisahau, pia tanga to dar mpaka dar to msumbiji. hizo sitazisahau, nikipata muda nitaleta uzi.
Mh, mkuu unafaa kuwa msimamizi mkuu wa mradi wa ujenzi ya reli ya standard gauge dar to mwanza. Peleka hii cv yako unapata kazi. Utapunguza cost za mafuta maana so kwa kukanyaga huko.
 
Back
Top Bottom