Ni mida ya jioni nashuka kwenye boti ya Azam kutoka bongo Islamic state (Zanzibar).
Mfukoni nimebakiwa na Shilingi mia tano huku Safari yangu inabidi nielekee Mbezi Kimara, simu imezima chaji lakini pia safari yangu toka Bongo Islamic state ikiwa ni ya shida maana nilienda kiutafutaji huko Zenji nimefika Zenji ikawa magumashi nikaamua kugeuza dsm baada ya kukosa mishe na sehemu ya kukaa.
Niliposhuka kwenye boti nikatembea mpaka mnazi mmoja huku nawaza nafikaje mbezi.
Basi nikasimama pale mnazi najiuliza hapa nimuombe nani daah nikakumbuka katika mishemishe zangu mjini hapa nilishwahi kutana na watu mbalimbali wamepungukiwa nauli na unakuta yupo smart kimuonekano anakuomba umuongezee nauli nikawa nafikiri Ni matapeli.
Leo nami nikasema hamna namna hapa nimueleze mtu yeyote anisaidie japo elfu moja ili niongezee nauli.
Basi nikamuona kijana anaongea na simu pale baada ya kumaliza nikamface nikamweleze shida yangu mshikaji akazama mfukoni akanipatia elfu moja nilimshukuru sana yule kijana hakika umeniokoa Mungu akubariki sana.
Hakika watu wema bado wapo kijana umenisaidia sana.