Wale tuliowahi kuishiwa nauli katika mishemishe tukutane hapa tuelezee tulifanyaje tukapata nauli

Wale tuliowahi kuishiwa nauli katika mishemishe tukutane hapa tuelezee tulifanyaje tukapata nauli

Acha tuu mimi ndo maana leo Mtu akiniomba hela kapungukiwa nauli NAMPA WALAHI....!! Yani kuna siku nimetoka zangu geto nawahi chuo gari imefika mbali kabisa najisearch sina hela alafu asubuhi makondakta wanazingua balaaa.. Ile nimeshuka konda kakomaa na mimi aisee ili bdi nimuombe mwana anilipie hakusita yani akanitolea acha aisee haya maisha penda kusaidia watu waliokatika hali ngumu kama unaweza ni Hazina kubwa na MUNGU ANAONAA AMINI MUNGU ANAONA ipo siku utatendewa wema sio sababu unastahili ila sababu ulishawahi kutenda wema..!!

Hars times teach us best lessons in life...
 
ile nimemaliza chuo mwaka mzima nipo home nimetuma sana maombi ya kupata seheemu tu ya kujishikiza

nilitrmbea Upanga hadi mbezi mwsho
siku moja napigiwa simu na taasis moja ya serikali kwa ajili ya kwenda kuchukua barua kwa ajili ya kujishikiza kama trainee niligurahi sana

nipo geto nikijichek ivi nina nauli tu ya kwenda nikasema ntaenda tu.
kweli nikaanza safari ya kuelekea upanga kweli nikapata barua nilifurah sana

ila msala nikurud nikaanza kuprint mdogomdogo tena nilikua nafuraha ya kupta sehem tu kujishkiza.

nimetoka upanga saa 7 mchana naingia mbezi mwisho saa 11 jion nimechoka baalaaa

daah nikikumbuka nafurah sana
 
Mkaka uliyenisaidia nauli kutoka mbez hadi kibaha Jah akubariki sana na akuongezee mafanikio zaidi. Sitasahau ile siku wallah hadi nafukiwa chini. Acha tyuuuh [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]

Kumbe unanikumbuka![emoji39]
 
Ni mida ya jioni nashuka kwenye boti ya Azam kutoka bongo Islamic state (Zanzibar).​

Mfukoni nimebakiwa na Shilingi mia tano huku Safari yangu inabidi nielekee Mbezi Kimara, simu imezima chaji lakini pia safari yangu toka Bongo Islamic state ikiwa ni ya shida maana nilienda kiutafutaji huko Zenji nimefika Zenji ikawa magumashi nikaamua kugeuza dsm baada ya kukosa mishe na sehemu ya kukaa.​

Niliposhuka kwenye boti nikatembea mpaka mnazi mmoja huku nawaza nafikaje mbezi.​

Basi nikasimama pale mnazi najiuliza hapa nimuombe nani daah nikakumbuka katika mishemishe zangu mjini hapa nilishwahi kutana na watu mbalimbali wamepungukiwa nauli na unakuta yupo smart kimuonekano anakuomba umuongezee nauli nikawa nafikiri Ni matapeli.​

Leo nami nikasema hamna namna hapa nimueleze mtu yeyote anisaidie japo elfu moja ili niongezee nauli.​

Basi nikamuona kijana anaongea na simu pale baada ya kumaliza nikamface nikamweleze shida yangu mshikaji akazama mfukoni akanipatia elfu moja nilimshukuru sana yule kijana hakika umeniokoa Mungu akubariki sana.​

Hakika watu wema bado wapo kijana umenisaidia sana.​
Nilisha tembea mwenge to tabataa segerea huo Ni mwendo wa masaa ma nne boda tu boda....
Pia mbagala rang3 mpka ubungo boda tu boda....
Mm niki kosa nauli huwa siogopi kujilipua kutembea...

Datc why mtu akinifuuata anaomba nauli bila iyana Mara zote huwa nawapatia...

Kama ushawai pewa msaada nam mtu mpka ukaogopa mfano nilikua na ingia kweny mtiani wa chuo SIKUA na calculator Nika mface jamaa mmoja nisie mjua akanipa calculator yake mpya nikataka kuweka bond kitu jamaa anasema wewe nenda utaniletea

Imagine mtu anakupaa imani ya namna hiyo....duu

Let's say good people are still alive
 
mimi nimesaidia wengi sana hizi nauli sijui kuombwa hela ya kula hawaesabiki huwa najisemea moyoni kama wananitapeli potelea mbali najua wanashida anyway kuna siku mama mmoja yuko smart kweli nakiete pharmacy pale ananiambia hajala na hana nauli nikampa elfu kumi

Jitahidi uendelee na moyo huo.
 
Kuna mdau mmoja humu nakumbuka baada ya kukosa nauli alijiongeza akapelekwa home na gari LA kuzibua vyoo, baada ya kuwapanga kwao choo kimejaa si unajua uswajilini vichochoro gari haingii.Mwana kawaonyesha jamaa home pale dakika mbili nakuja ndo kimoja washkaji kwenda kuulizia wanaambiwa hpa hakuna choo kilichojaa pia hii ni njia

Hii dhambi
 
Ilishawahi kunikuta hiyo nimepanda basi nauli 700 Mbezi-Kibaha,nimefika mlangoni konda anachukua hela, kujisachi mfukoni nikakumbuka pochi nimeacha kwenye suruali nyingine, ikabidi nizuge kuna jamaa yuko chini ana hela zangu, ile kushuka ikawa kama bahati kuna jamaa namjua anakatiza, nikamuelezea akanipa buku mbili, ila inafikirisha sana hiyo situation, akili huwa inafanya kazi kwa kiwango cha juu sana kutafuta solution ili kukwepa aibu...

Akili kama hiyo ukiitumia tafuta hela utafanikiwa sana
 
Ni mida ya jioni nashuka kwenye boti ya Azam kutoka bongo Islamic state (Zanzibar).​

Mfukoni nimebakiwa na Shilingi mia tano huku Safari yangu inabidi nielekee Mbezi Kimara, simu imezima chaji lakini pia safari yangu toka Bongo Islamic state ikiwa ni ya shida maana nilienda kiutafutaji huko Zenji nimefika Zenji ikawa magumashi nikaamua kugeuza dsm baada ya kukosa mishe na sehemu ya kukaa.​

Niliposhuka kwenye boti nikatembea mpaka mnazi mmoja huku nawaza nafikaje mbezi.​

Basi nikasimama pale mnazi najiuliza hapa nimuombe nani daah nikakumbuka katika mishemishe zangu mjini hapa nilishwahi kutana na watu mbalimbali wamepungukiwa nauli na unakuta yupo smart kimuonekano anakuomba umuongezee nauli nikawa nafikiri Ni matapeli.​

Leo nami nikasema hamna namna hapa nimueleze mtu yeyote anisaidie japo elfu moja ili niongezee nauli.​

Basi nikamuona kijana anaongea na simu pale baada ya kumaliza nikamface nikamweleze shida yangu mshikaji akazama mfukoni akanipatia elfu moja nilimshukuru sana yule kijana hakika umeniokoa Mungu akubariki sana.​

Hakika watu wema bado wapo kijana umenisaidia sana.​

asante kwa kushukuru, yule kijana aliyekupa ndio mimi sema leo nko na shida na teni sijala kabisa, naomba ulipe fadhila basi kidogo
 
Mimi hadi leo Mtu akiniomba nauli na nina helaa nitampaa Tuu...!! Huwa naelewa sana hii hali maana ishawahi kunikutaa na mtu alinipa toka siku hiyo nilijifunza kitu. Jana tu kuna mwanafunzi aliniomba nauli nikampa 1000 japo alihitaji 200..
 
Nimetoka Dar nimeahidiwa tumiwa nauli, nikazama Darlux la Arusha nikamwambia Konda mpaka Chalinze nauli fresh!

Kibaha hola, naanza tetemeka, sina vocha sina kitu, wala message, aliyeahidi kimya, nikashushwa chalinze, nikatafuta mahali nikakaa!

Nimekaa mpaka saa 12 sijawa, sijanywa sina Vocha’s sina kitu, akatokea Mzee akanambia Kijana Nimekuona toka asubuhi shida nini?

Nikamweleza, akanambia chukua bag twende, kudadadeki, kanipeleka Guest kalipa 25,000/- nikaanza ogopa, akanipa cash 40,000/- akanambia Safari njema kesho!

Kaondoka, nikasema hapa yaweza kuwa msala siamini amini, cha kwanza nikahama Chumba, cha pili nikaenda tafuta chakula!

Sikuwahi mwona tena yule Mzee mpaka Leo wala hakurudi!
Tenda wema uende zako. Hiyo ndio yenyewe. Siku moja ukikutana na mtu ana shida kama hiyo msaidie tu uende zako.
 
Siku moja nilitokea sehemu fulani twn nikashuka kimara,,,niunganishe gari nielekea nyumbani,,,kipindi hicho mabasi ni yakuungaunga sio kama usafiri wa sasa,,
Nimeshuka pale nikiwa na uhakika kwamba nina pesa zangu mfukoni,,
Nakumbuka kama nilitaka kununuwa kitu fulani wakati bado naendelea kusubiri usafiri ,,
Kujikaguwa mfukoni ,,,duu!!kumbe pochi sikumbuki niliangusha wapi..
Basi nilichanganyikiwa sn,,,tena kipindi hicho hata mambo ya pesa kwa miamala ya simu pia bado haijaanza,,,, nikajiuliza sasa nitafiikaje nyumbani?
tena bado ni mbali kutoka hapa?
now ni saa saba mchana,,tena jua ni kali sana,,kutembea kwa miguu hadi nyumbani ni kipengele.
Pale pale nikapata ujasiri wa kukumbuka maneno fulani ya Mzee wangu fulani aliwahi kuniambiya,,
Siku zote mwanamke husaidiwa na mwanaume,, na mwanaume husaidiwa na Mwanamke tena kwa urahisi sn kuliko mwanaume mwenzie..
Basi kipindi hicho nakumbuka wakati huo black Berry phones ndy zilikuwa zipo kwenye chat kubwa sn,,BlackBerry touch na BlackBerry bold.
Nikiwa na BlackBerry phones zangu mbili kali sana,,mkononi,,huku nanukia perfumes Kali sana aina ya kurous na joop.,
Nilimfata dada mmoja mrembo sana tu,,alikuwa kasimama pembeni yangu kidogo,,tulikuwa tukisubiri magari pamoja kituon,, Nikaanza kumsemesha semesha,, nikawa kama namtongoza hivi,,,baadae nikabadilisha mada,,nikamuuliza yule mrembo,
Hivi mm ukiniangalia unanionaje?
Yule mrembo akasema ,,,nakuona upo powa tu,,tena Simu zako nimezipenda sana,,umenunuwa wapi? Nimenunuwa South Africa nikamjibu yule mrembo,,
Nikamwambiya Mimi nina tatizo,, na sijuwi kama utanielewa,,,na kuniamini,,
Basi yule mrembo akaniangalia sana kwa makini ,,juu hadi chini,,
Niliruhusu anikaguwe ili dawa umuingie vzr mwilini..
Kisha nikamwambiya nimeangusha pochi na nahitaji kufika nyumbani,,nahitaji 300 tu nifike Mbezi ,,halafu kwngine nitatembea,,
Basi yule mrembo akaniangalia akanipa sh 1000 ,,,tena bila kujiuliza Mara 2.
Nikapokea,,ikawa bado tunazungumza mawili matatu ,,ikaja daladala tukaingia,,
Muda wa kutoa nauli nikamtolea nauli lakini aliikataa,,
Tukafika Mbezi,,tukapanda lingine na bado aligoma nisimlipie nauli,,
Baadae nilichukuwa mawasiliano yake ,,
Baadae tukaangukia ktk mapenzi,,
Hadi leo nikikumbuka ile issue ya nauli najiuliza bila yule mrembo sijuwi ningefikaje nyumbani..
 
Back
Top Bottom