Wale tuliowahi kuishiwa nauli katika mishemishe tukutane hapa tuelezee tulifanyaje tukapata nauli

Wale tuliowahi kuishiwa nauli katika mishemishe tukutane hapa tuelezee tulifanyaje tukapata nauli

Nili print kutoka Kariakoo mpaka Kinondoni Studio...

Ilikua ni utoto, hela niliimaliza kununulia mazaga huku naona kabisa ikiwa inaisha, sababu nilikua mdogo na sijawahi kupata shida yoyote ya kiuchumi, basi nilihisi mtoto mdogo hawezi kua na shida popote wakubwa wakamuacha......
Yani niliamini tuu wakiniona natembea kwa mguu wataniuliza halafu nikiwaambia nitapata msaada...kuomba niliona aibu sana, lakini pia inahitaji timing la sivyo nita aibika zaidi.

Shaaabash, labda wakubwa wa peponi.....

Nikaenda kwenye duka la Anko (ilikua nikienda na bimkubwa hua tunapitia hivyo nikawa napafahamu) kufika kashafunga maana ilikua 12 jioni,
Nikaenda kwa rafiki yake mzee, kufika napo chenga....

Sasa hapa ndio utoto ukaanza kunitoka,

Kumbuka hapo kinachonitesa eti ni Sh 100 ya nauli ya mwanafunzi, na kilichonipeleka k.koo ni kwenda mchikichini kununua notes na mazaga mengine ya shule,
Hela iliyobaki ndio nikaitumia kipuuzi...

Kuomba nako nahisi aibuuu,

Kwa ufupi Nikakanyaga raba, Mbaya zaidi njiani nikakutana na vibaka wakapita na yale mazaga yote ambayo ndio yaliyonifanya ni nitembee (ilikua nguo na viatu) halafu wakaniachia yale mahitaji yaliyonipeleka Kariakoo(vitabu, daftari n.k) tena walitaka wapite na begi lote ila sijui wakashauriana nini, basi mmoja akaniita halafu akanirushia begi maana nilishaakimbia.

Kwa ufupi nilikaribishwa ukubwani kwa Tanzania Shilling Mia moja( 100)..
Sasa kariakoo na kinondoni ndo umetembea nini,hapo wala hutakiwi kupanda bus
 
Duuuu, kuna siku nilienda mjini Singida kutokea Iramba kutoa picha za watu nikaishiwa hela ilinilazimu kumpigia dadangu kumuomba anisaidie buku tano ilikuwa fedheha saaana

Ila huyo ni ndugu yako mkuu, she got your back. Hakuna tatizo hapo.
 
mimi nimesaidia wengi sana hizi nauli sijui kuombwa hela ya kula hawaesabiki huwa najisemea moyoni kama wananitapeli potelea mbali najua wanashida anyway kuna siku mama mmoja yuko smart kweli nakiete pharmacy pale ananiambia hajala na hana nauli nikampa elfu kumi
Usijali hata kama wanatapeli ww fungi lako kwa Muumba halipungui kwani unatoa kwa lengo la kuondoa shida ya mwanadamu mwenzako. Mungu akuzifishie
 
Ni mida ya jioni nashuka kwenye boti ya Azam kutoka bongo Islamic state (Zanzibar).​

Mfukoni nimebakiwa na Shilingi mia tano huku Safari yangu inabidi nielekee Mbezi Kimara, simu imezima chaji lakini pia safari yangu toka Bongo Islamic state ikiwa ni ya shida maana nilienda kiutafutaji huko Zenji nimefika Zenji ikawa magumashi nikaamua kugeuza dsm baada ya kukosa mishe na sehemu ya kukaa.​

Niliposhuka kwenye boti nikatembea mpaka mnazi mmoja huku nawaza nafikaje mbezi.​

Basi nikasimama pale mnazi najiuliza hapa nimuombe nani daah nikakumbuka katika mishemishe zangu mjini hapa nilishwahi kutana na watu mbalimbali wamepungukiwa nauli na unakuta yupo smart kimuonekano anakuomba umuongezee nauli nikawa nafikiri Ni matapeli.​

Leo nami nikasema hamna namna hapa nimueleze mtu yeyote anisaidie japo elfu moja ili niongezee nauli.​

Basi nikamuona kijana anaongea na simu pale baada ya kumaliza nikamface nikamweleze shida yangu mshikaji akazama mfukoni akanipatia elfu moja nilimshukuru sana yule kijana hakika umeniokoa Mungu akubariki sana.​

Hakika watu wema bado wapo kijana umenisaidia sana.​
Nawapenda sana wanaume maishani mwangu mmebalikiwa na mungu toka mbinguni katika pita pita zangu niliishiw nauli Mara nyingi nikapew nauli na wanaume kwa wakati tofauti bila kuombwa chochote kwenye mwili wangu wala no nilisaidiwa tu na bado naendelea kusaidiwa na wanaume
 
Sina nyingine tumia mbinu za kimedani.
Anza kuhubiri kwenye gari, ukifika sehemu uendayo shuka. Awadai nauli watumishi
 
Nimetoka Dar nimeahidiwa tumiwa nauli, nikazama Darlux la Arusha nikamwambia Konda mpaka Chalinze nauli fresh!

Kibaha hola, naanza tetemeka, sina vocha sina kitu, wala message, aliyeahidi kimya, nikashushwa chalinze, nikatafuta mahali nikakaa!

Nimekaa mpaka saa 12 sijawa, sijanywa sina Vocha’s sina kitu, akatokea Mzee akanambia Kijana Nimekuona toka asubuhi shida nini?

Nikamweleza, akanambia chukua bag twende, kudadadeki, kanipeleka Guest kalipa 25,000/- nikaanza ogopa, akanipa cash 40,000/- akanambia Safari njema kesho!

Kaondoka, nikasema hapa yaweza kuwa msala siamini amini, cha kwanza nikahama Chumba, cha pili nikaenda tafuta chakula!

Sikuwahi mwona tena yule Mzee mpaka Leo wala hakurudi!
Ungeliwa kibogaa yaheee
 
Tatizo Kuna matapeli pia,Kuna kipindi Niko mwanza nikakutana na jamaa anganiingila kwa gia kwamba amepungukiwa nauli na anataka kuwai interview yeye Ni mlizi,sikua vizuri Ila Nika sema mpaka mtu amekuface kweli anauitaji,nilikua na buku tano Nika mpa buku mbili....baada ya wiki nikakutana namtu huyo huyo na sound hizo hizo asee nilitamani kimdai
 
Kipindi nasoma shule mojaa mwanga huko milimani....sinakala naulii mzee nilishuka Hadi mwanga mjini kwa miguu
 
Nina mikasa mitatu ya ukata iliyowahi kunikumba hadi hivi niandikapo. Nitawashirikisha mkasa mmoja leo na mikasa mingine miwili nitaitoa siku za usoni:

Mwaka ulikuwa 1976 wakati huo TRC ikiwa chombo muhimu sana cha usafiri kwenda Bara, wakati huo usafiri wa mabasi ukiwa unaendeshwa na Serikali kupitia kampuni ya mabasi ya Taifa yaani KAMATA. Mzazi wangu aliamua kunihamisha kutoka shule sekodari ya kutwa hapa Dar, kwenda shule moja maarufu ya bweni iliyoko wilaya ya Iramba. Mzee alinikatia tiketi ya treni hadi Itigi. sikumbuki nauli wakati huo ilikuwa kiasi gani, ila alinikabidhi tiketi na pesa ya njiani kitu kama shillingi hamsini hivi.... sikumbuki vizuri!. Treni wakati huo zilikuwa zikiondoka saa 9 na kufika Itigi kesho yake saa saba mchana.... Tulifika Itigi saa sita na nusu mchana.

Enzi hizo, ukishuka kwenye treni unakuta mabasi ya KINANDA yanasubiri abiria wanaoshuka kwenye treni kwenda Singida, enzi hizo barabara ni vumbi tupu. Tulifika Singida saa kumi na moja jioni na kulazimika kutafuta nyumba ya wageni pale stendi ya wakati huo, na kununua kabisa tiketi ya kwenda Kinampanda kesho yake asubuhi kwa basi lililoitwa IRADECO wakati huo.

Kesho yake asubuhi sana baada ya kufugua kinywa nikapanda basi kuelekea Kinampanda, sikuwa na pesa nyingi mfukoni, nikitegemea mambo yatanyooka tu huko huko shuleni!!.. Kufika nikaripoti kwa mkuu wa shule wakati huo Mwalimu Msemembo, baada ya kusoma barua kutoka kwa katibu mkuu wa wizara ya elimu pamoja na cheti cha uhamisho kutoka Mzizima Secondari School, mkuu akaanza kulalamika kuwa shule ina wanafunzi wengi, mara hakuna nafasi bwenini ... Akagoma kupokea vyeti vyangu!. Kwa bahati akaingia mwalimu mmoja kijana hivi, akaniangalia nami nikamuwahi kwa "shikamoo"... mkuu akataka kumshirikisha huyu mwalimu ili akazie uamuzi wake, badala yake yule mwalimu kijana akaropoka kuwa kuna vitanda viko wazi kwenye mabweni. Mkuu wa shule mara akabadilisha gia juu kwa juu kwa kuwa sikuwa na godoro ... Nikarudishwa nyumbani ili nirudi na godoro la kulalia maana ndio utaratibu wa hapo shule.

Mkuu bila hata kuniuliza kama nina pesa ya kutosha akaniamuru nirudi na basi lililonileta maana linapita tena saa saba mchana kurudi Singida. Nikafanya hivyo nakurejea tena kwenye nyumba ya wageni "Pongezi Guest House" na kulala hapo hadi kesho yake nilipopanda basi kuelekea Itigi kungojea treni yoyote itakayotangulia kufika, wakati huo pesa yote niliyokuwa nayo ilikuwa imekwisha. Siku hiyo ilitangulia kufika treni ya kwenda Tabora tena ikiwa imechelewa sana na imejaa hadi watu wananing'inia kwenye ngazi... Nilisafiri kwenye ngazi hadi usiku ulipoingia bila kuwa na tiketi hadi Tabora bila kulipa, siku hiyo mkaguzi wa tiketi "TT" hakuweza kabisa kupita kukagua tiketi sababu ya nyomi.... Ikawa faida kwangu.. Baada ya kufika Tabora nikawa napanga namna ya kuendelea na safari tena ya masaa 12 kwenye treni hiyo bila kuwa na pesa wala tiketi.

Katika kupitapita kwenye mabehewa, nikamkuta mchungaji wa kanisa letu huko kwetu, akanitambua!!.. Akaniita, baada ya kusalimiana nae na kufahamu nimetoka wapi, akaniuliza kwa nini siko na mzee wangu maana yuko daraja la pili vyumba vya kulala? ... Nikamjibu kuwa mimi nimepandia pale Tabora hivyo nitamtafuta.. Baada ya kuachana na mchungaji, nikamfuata mzee, nikamhadithia kilichotokea bila kuficha! Akaninunulia tiketi ya daraja la tatu ..... Safari ikaendelea Ha ha ha 😂 😂
 
Nimetoka Dar nimeahidiwa tumiwa nauli, nikazama Darlux la Arusha nikamwambia Konda mpaka Chalinze nauli fresh!

Kibaha hola, naanza tetemeka, sina vocha sina kitu, wala message, aliyeahidi kimya, nikashushwa chalinze, nikatafuta mahali nikakaa!

Nimekaa mpaka saa 12 sijawa, sijanywa sina Vocha’s sina kitu, akatokea Mzee akanambia Kijana Nimekuona toka asubuhi shida nini?

Nikamweleza, akanambia chukua bag twende, kudadadeki, kanipeleka Guest kalipa 25,000/- nikaanza ogopa, akanipa cash 40,000/- akanambia Safari njema kesho!

Kaondoka, nikasema hapa yaweza kuwa msala siamini amini, cha kwanza nikahama Chumba, cha pili nikaenda tafuta chakula!

Sikuwahi mwona tena yule Mzee mpaka Leo wala hakurudi!
Malaika wanaexist
 
Hao wanakuwaga malaika hao[emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom