Wale tuliowahi kuishiwa nauli katika mishemishe tukutane hapa tuelezee tulifanyaje tukapata nauli

Mwaka 2004 nimeenda mpwapwa dodoma kununua madini Fulani.

Sikufanikiwa kupata mzigo niliokusudia.

Nikaenda baa moja inaitwa HAFUNSI nikala Pombe mpaka saa nane.

Nikatoka HAFUNSI hotel ya msomali nadhani nikashuka kwenye baa Fulani zinapakana na mto mkubwa ila muda mwingi unakuwa umekauka.

Nikala Pombe mpaka saa kumi alfajiri nikachukua (ikoma ngiru) nikaenda kulitandika akaniibia milioni mbili na laki tatu.

Asubuhi nikaenda nbc bank nitoe hela nikaambiwa mpwapwa hakuna nbc mamaeeeee mfukoni Nina Mia tano ya kijani narudije daa?

Itaendelea.........

Ikoma ngiru ni noma wazee...!!!!
 
mimi ndo mana natembea na madini kama baharia[emoji23]maana muda wowote unafanya barter trade
niliporwaga mwaka fulani Coco bahati nzuri nikabaki na saa kali ,kwahiyo nikampa konda kwa exchange ya 300 kipindi icho aisee tangu mwaka huo nauli kwenye ziwa.
Next time tunaondoka na Hilo ziwa[emoji1787][emoji1787]
 
Nilipokuwa nasoma Mazengo sekondari ilikuwa ni lazima ulipe nauli shuleni siku unayofika!Yaani ile unalipa ada unalipa nauli!Nakumbuka nilikuwa nalipa 10400/= kama nauli ya treni kutoka Dodoma to kigoma!Term la kwanza likapita fresh tu,sasa kuanzia term la pili nilishakuwa mjanja nikadanganya kwa SBM(senior board master) kuwa nitabaki Dodoma ili nisilipe nauli!😁!Basi ikatiki na ile nauli nikafanyia starehe ikaisha!Hapo katikati nilikuwa nakusanya kutokana na poketi money ambayo nilikuwa natumiwa ili ifikie ile nauli ila kila mara najikuta nimeitafuna!Kimbembe kikafika tumefunga na natakiwa nisafiri!Nilitumia 12,000 ya kula njiani!Nikasema siwezi kukata tiketi nikateseka njiani na njaa!Basi bhana,nikazama kwenye gogo(treni) bila tiketi!Ilikuwa mishe sana kupita getini,ikabidi nijifanye namsaidia mama mmoja alikuwa na mizigo na watoto,yeye ndiye alionesha tiketi kadhaa huku mimi nikiwa busy na mizigo!Nikapenya!
Huko njiani ilikuwa tabu sana,mara nijifiche chini ya siti watu walizokaa nikimuona Cleaner au TT wakiwa wanakagua!Mpaka nafika kigoma ilikuwa balaa maana kuna wenzangu waliokuwa hawana tiketi walipigwa pingu na kushushwa vituo vilivyofata na kukabidhiwi kwa polisi!
Siwezi kusahau mihangaiko niliyoipata siku hiyo!
Nyingine nilishawahi kumsindikiza mtu ubungo kumbe nimevaa suruali ambayo siyo niliyokuwa nimevaa jana yake ambayo ndiyo ilikuwa na hela!Bahati mbaya hata simu niliacha charge nyumbani,nilikuwa nakaa kimara!Ile nimeagana na mgeni wangu naenda kupanda daladala hela hamna!
Sikutaka kusumbua watu maana ilikuwa asubuhi,ilibidi nifanye mazoezi ya kukimbia kutoka ubungo mpaka kimara mwisho!!!😁😁
 
Huwa najisikia faraja sana kusaidia random people at random circumstances
 
Juzi tu hapo kipindi cha covid 19 nimetoka mlowo,mbozi,songwe nakwenda hospital vwawa,mbozi,songwe nina kanauli tu buku kwenda nakurudi maana matibabu nilitegemea bima asa si nikasahau barakoa nafika hospitali huingii bila barakoa na mfukoni nina jero(mia tano) ya kurudia home! Barakoa yenyewe buku daah! Moto uliwaka nikamwomba muuzaji wa barakoa anifanyie kwa jero hakukubali nikijaribu ongea na mlinda mlango nae hanielewi nikakata shauri nirudi tu nyumbani sasa ile napiga hatua mbili tatu kurudi nyumbani wa barakoa akanionea huruma kanipa ya buku kwa jero hapo nikabaki mweupe mfukoni hospitali nikahudumiwa vizuri kimbembe kikabaki kurudi home ukizingatia niko smart ile kinoma si kwa mavazi tu hapana hata look mora kanijalia, swali likabaki kichwani nafikaje home sasa nikiwa najongea taratibu kuelekea uelekeo wa nyumbani miguu ikanogewa nikakanyaga mpaka home kaumbali karefu hatari nilifika nimechoka sio poa but problem was solved
 
Niliwahi kupitia kipindi kigumu ikanibidi nichague kipande gani nipande basi na kipande gani nitembee. Mfano Ada estate hadi maeneo ya posta mpya nilikuwa natembea, au ada estate hadi Mwenge, natembea, Mwenge hadi Kunduchi napanda basi.
Sijawahi kulazimika kumwambia yeyote kuwa sina nauli.
 
Hakukuomba papuchi aigegede
Mkaka uliyenisaidia nauli kutoka mbez hadi kibaha Jah akubariki sana na akuongezee mafanikio zaidi. Sitasahau ile siku wallah hadi nafukiwa chini. Acha tyuuuh [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Mwaka 2004 nimeenda mpwapwa dodoma kununua madini Fulani.

Sikufanikiwa kupata mzigo niliokusudia.

Nikaenda baa moja inaitwa HAFUNSI nikala Pombe mpaka saa nane.

Nikatoka HAFUNSI hotel ya msomali nadhani nikashuka kwenye baa Fulani zinapakana na mto mkubwa ila muda mwingi unakuwa umekauka.

Nikala Pombe mpaka saa kumi alfajiri nikachukua (ikoma ngiru) nikaenda kulitandika akaniibia milioni mbili na laki tatu.

Asubuhi nikaenda nbc bank nitoe hela nikaambiwa mpwapwa hakuna nbc mamaeeeee mfukoni Nina Mia tano ya kijani narudije daa?

Itaendelea.........

Ikoma ngiru ni noma wazee...!!!!
Du!! .. NBC benki ya kipuuzi sana hiyo, kuna mwaka mmoja pale Mwanza walinikatalia kuchukua pesa yangu mwenyewe wakidai taratibu zao zinaruhusu mtu kuchukua pesa kwenye tawi alikofungulia!!..... Amini usiamini, ilinilazimu kutembea siku tatu kutoka Mwanza hadi Kahama.😡
 
Ulitembea siku tatu????? Duuh mkuu ungeomba hata msaada uweke dhamani kitu
 
We acha tu mtu wangu, nilisimamisha roli moja la SHIRECU, kilometa chache kabla ya kufika Misungwi dereva alikuwa anapeleka mzigo wa pamba Shinyanga akadai haruhusiwi kubeba abiria, lakini alinisogeza hadi Misungwi akaniacha hapo.
 
1. Nilitembea kutoka Bondeni mpaka mabibo.

2. Nilitembea kutoka mbezi mwisho mpaka mbezi shule via goba. (Pia nilikuwa naumwa na nilikuwa na mzigo mzito)
3. Nilitembea kutoka lego mpaka mwenge kisha nikaenda mpaka ubungo via mawasiliano na kurudi tena lego. ( Nilifanya hivyo ili muda uende ili nikirudi nikute mtu niliyekuwa nimemuomba nauli awe ameshatoka kwenye semina alikiwa anahudhuria) Hata hivyo pesa aliyonipa haikutosha kunifikisha ninakokwenda hivo ikabidi nitembee kutoka lego mpaka mwenge ili nibalance nauli.

NB: Napenda sana kutembea, hivyo hata nikikosa nauli huwa siwazi sana. Labda kama kuna ishu ya fasta au ni route ndefu sana.
 
  • Thanks
Reactions: Auz
Kuna mdau mmoja humu nakumbuka baada ya kukosa nauli alijiongeza akapelekwa home na gari LA kuzibua vyoo, baada ya kuwapanga kwao choo kimejaa si unajua uswajilini vichochoro gari haingii.Mwana kawaonyesha jamaa home pale dakika mbili nakuja ndo kimoja washkaji kwenda kuulizia wanaambiwa hpa hakuna choo kilichojaa pia hii ni njia
[emoji3][emoji3][emoji3]
 
1. Nilitembea kutoka Bondeni mpaka mabibo.

2. Nilitembea kutoka mbezi mwisho mpaka mbezi shule via goba. (Pia nilikuwa naumwa na nilikuwa na mzigo mzito)
3. Nilitembea kutoka lego mpaka mwenge kisha nikaenda mpaka ubungo via mawasiliano na kurudi tena lego. ( Nilifanya hivyo ili muda uende ili nikirudi nikute mtu niliyekuwa nimemuomba nauli awe ameshatoka kwenye semina alikiwa anahudhuria) Hata hivyo pesa aliyonipa haikutosha kunifikisha ninakokwenda hivo ikabidi nitembee kutoka lego mpaka mwenge ili nibalance nauli.

NB: Napenda sana kutembea, hivyo hata nikikosa nauli huwa siwazi sana. Labda kama kuna ishu ya fasta au ni route ndefu sana.
Kutembea ni zoezi zuri.
 
Kipindi cha bodi ya mikopo tunaita TIRDO Kule msasani.Siku hiyo ilikuwa deadline ya kurudisha form nafika msasani na kutokujua tukaambiwa lazima ufungue account bank shilingi 20k kama sikosei.Sina simu nimekariri namba ya mdingi nikampigia hapatikani.Nikapanda daladala hadi posta pale azikiwe hapo nauli ikawa sina tena.Nikavuka pale crdb azikiwe nikajaza form na wanafunzi wenzangu walikuwa nyomi stress balaa saa nane mchana sina hata Mia.Form ya kufungua account inataka wadhamini watatu kila nikiwaomba wale wateja pale na hivyo hawakujui wanakataa na hela ya kufungua account sina.Muda umeenda saa tisa na nusu.

Mziki wa HESLB miaka ya 2006-7 usipime na kama huna division 1 kijana wa kiume hupati.

Mama mmoja akaniona nimekaa pale kituoni nalia mtoto wa kiume naona chuo basi tena akaniuliza nini mwanangu. Nikamuelezea akasema twende ofisini. Nikaenda nae hadi kule wizara ya afya pale IFM akanijazia form na wadhamini na copy za atm card zao akanipeleka hadi pale crdb holland house.Muda wa bank ulishaisha sema labda walikuwa wanamfahamu wakamfungulia mlango then nikaitwa na mimi.Nikafungua account.

Akampigia mzee mmoja akaja na pikipiki ya DFP.Mpeleke huyu kijana msasani akampa hela ya mafuta 10k na mi 10k cash.Nilimshukuru yule mama machozi yakinitoka.Nilifanikiwa kukusanya form.

Nilivyofika home nikamsimulia bi mkubwa.Kesho yake tukaenda shamba Mapinga tukavuna mananasi na mihogo. Jumatatu asubuhi tukaenda ofisini kwa yule maza wizara ya afya bi mkubwa akampa mihogo na mananasi na hela 50k.Yule mama alikataa hela akachukua mananasi na mihogo.

Hivi sasa kastaafu nadhani Mungu ampe maisha marefu ni family friend sasa.Mkopo nilipata chuo nilipata.
 
Nakumbuka ilikuwa msimu wa sikukuu ya Pasaka. Nikatoka home Kinondoni kwenda Dar Live Mbagala kushangaa shangaa. Nikaingia kwenye daladala la Mbagala. Konda katika kudai nauli nikajisachi kisha nikakumbuka niliacha kipochi chenye pesa juu ya meza jikoni nyumbani. Sema kuna kaka akajitolea kunilipia kumbe nae alikuwa anaelekea Dar Live.
Ikawa ni kampani yangu, akanilisha na kuninywesha kisha akanisindikiza kurudi nyumbani saa 9 usiku tuko chakari....
Usiulize kilichoendelea....

Ila kuna mdau hapo juu kasema, kama mwanamke ukitaka kusaidiwa mtafute mwanaume na kama ni mwanaume ukitaka kusaidiwa mtafute mwanamke.
Ila kuna wati wakaksi sana, badala ya kukusaidia, wanaanza kukushangaa ndani ya daladala.
 
Yale masihara ya vijana wa Riki boy hayakutokea kweli hapa?
 
Kipindi cha bodi ya mikopo tunaita TIRDO Kule msasani.Siku hiyo ilikuwa deadline ya kurudisha form nafika msasani na kutokujua tukaambiwa lazima ufungue account bank shilingi 20k kama sikosei.Sina simu nimekariri namba ya mdingi nikampigia hapatikani.Nikapanda daladala hadi posta pale azikiwe hapo nauli ikawa sina tena.Nikavuka pale crdb azikiwe nikajaza form na wanafunzi wenzangu walikuwa nyomi stress balaa saa nane mchana sina hata Mia.Form ya kufungua account inataka wadhamini watatu kila nikiwaomba wale wateja pale na hivyo hawakujui wanakataa na hela ya kufungua account sina.Muda umeenda saa tisa na nusu.

Mziki wa HESLB miaka ya 2006-7 usipime na kama huna division 1 kijana wa kiume hupati.

Mama mmoja akaniona nimekaa pale kituoni nalia mtoto wa kiume naona chuo basi tena akaniuliza nini mwanangu. Nikamuelezea akasema twende ofisini. Nikaenda nae hadi kule wizara ya afya pale IFM akanijazia form na wadhamini na copy za atm card zao akanipeleka hadi pale crdb holland house.Muda wa bank ulishaisha sema labda walikuwa wanamfahamu wakamfungulia mlango then nikaitwa na mimi.Nikafungua account.

Akampigia mzee mmoja akaja na pikipiki ya DFP.Mpeleke huyu kijana msasani akampa hela ya mafuta 10k na mi 10k cash.Nilimshukuru yule mama machozi yakinitoka.Nilifanikiwa kukusanya form.

Nilivyofika home nikamsimulia bi mkubwa.Kesho yake tukaenda shamba Mapinga tukavuna mananasi na mihogo. Jumatatu asubuhi tukaenda ofisini kwa yule maza wizara ya afya bi mkubwa akampa mihogo na mananasi na hela 50k.Yule mama alikataa hela akachukua mananasi na mihogo.

Hivi sasa kastaafu nadhani Mungu ampe maisha marefu ni family friend sasa.Mkopo nilipata chuo nilipata.
Nawewe usaidie wengine
 
Back
Top Bottom