Da Vinci XV
JF-Expert Member
- Dec 7, 2019
- 3,862
- 6,438
Wasaalaam
Katika dini hizi kuu (Abrahamic) hakuna pande yoyote inayokataa uwepo wa Mtoto wa Mariamu Yesu wa Nazareth , historia na hadithi za maisha za Yesu/Issa zipo katika upande wa Dini kuu mbili hizi Uislam na Ukristo.
Maelezo Juu ya Bwana huyu Katika pande hizo mbili yana kiwango chake yanachofanana na mambo mengine kadhaa wa kadhaa hayashabihiani.
Katika Uislam pia Yesu anatambulika kama Mtume wa Mwenyezimungu ambaye alipewa , neno kwa ajili ya kufikisha ujumbe kwa Waja wa huyo M/Mungu.
Tunajifunza juu ya bwana huyu kwenye Biblia,Qur'an kwenye Sayansi na Hata katika Historia juu ya Bwana huyu ambaye alipewa Ishara ambazo hata Manabii na mitume wengine Hawakupata (kuponya wagonjwa, kufufua wafu N.K)
ikumbukwe si Biblia tu iaminiyo juu ya Miujiza ya Bwana Yesu
Qur'an inadokeza pia,
2:87
Na hakika tulimpa Musa Kitabu na tukafuatisha baada yake Mitume wengine. Na tukampa Issa, mwana wa Mariamu, Ishara(miujiza) zilizo waziwazi, na tukamtia nguvu kwa Roho Takatifu. Basi kila walipo kufikieni Mitume kwa yale ambayo hayapendwi na nafsi zenu, mlijivuna; wengine mkawakanusha, na wengine mkawauwa.
Lakini kuwa na miujiza kwa wajumbe wa Mwenyezimungu ni jambo la kawaida ili waumini wapate kuamini kupitia kwayo.
Mlengo wa nyuzi hii ulijikita kwa Huyu bwana Yesu ambae alikuwa na Miujiza mikubwa na ya kipekee, na Hapa swali linajikita kwenye Hili la kufufua wafu.
Ni dhahiri Bwana Yesu hakufufua mfu mmoja , bali ni wengi sana lakini kipo kisa maarufu cha Lazaro , ambacho Injili ya Yohanna pekee imekielezea hichi kisa kwa Upana kidogo. Nami nitapenda nikitumie kisa hicho.
Yohana 11:41
Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia.
42
Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma.
43
Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje.
44
Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake.
Hapo anaelezewa Lazaro alipotolewa katika Wafu na Bwana Yesu
SWALI KUU HAPA NI KWAMBA
NINI MREJESHO WALIOKUJA NAO WAFU WALIOFUFULIWA , HUKO WALIKOKUWA?
Ukiachana na mafunzo tuyapatayo juu ya Uwepo wa M/Mungu na Kupitia miujiza kama hiyo.
Haijaandikwa katika histori hiyo kama ilivyoandikwa na mwandishi wa injili hiyo.
Ni wazi kwa mwandishi ilikuwa kwamba ni muhimu katika Histori hii.??
Histori inatuonyesha kwamba Wayahudi wengi walikuwa na mawazo tofauti juu ya ufufuo huo, Injili hii Iliandikwa yapata miaka sabini baada ya kupaa kwa Bwana Yesu.
Ufufuo wa Lazaro ni moja ya kielelezo cha mfululizo wa taarifa za kitheolojia. Katika histori hii Lazaro ndiye pekee ambaye hakusema, chochote.
Martha na Mariamu nduguze na Lazaro walipata kusema, Wayahudi nao walipata kuongea na Pia Yesu ameongea kuhusu Ufufu huo.
Lakini Lazaro ndiye aliyekaa kimya.
KAMA TUJUAVYO BWANA HAKUMFUFUA LAZARO PEKEE BALI WENGI AMBAO WENGINE HATUKUWAJUA
je ni vipi Mrejesho wa wafu hawa ,Walipata kusema nini? huko walikokuwa nini kiliwapata?? walijitambua?? au hawakujitambua?? Maisha ya Hali ya UFU yalikuwa vipi?
NB: Nyuzi hii haiko kwa Ajili ya kuleta mgongano wowote wa kiimani