Wale waliofufuliwa walipata kusema nini huko walikokuwa?

Hiyo hukumu unayoongelea ambayo wafu wanaisubiri ataitoa nani? Unasema Yesu wa kweli alikuwa Muafrika na aliishi miaka 2000 iliyopita, sasa kwa nini hapo hapo umehitimisha ukisema huliamini jina Yesu?

Na baada ya hukumu, wakosefu na wasio wakosefu watakuwa sehemu moja au watatenganishwa? Kama watatenganishwa, sehemu watakayokuwa wakosefu itaitwaje? Pia, sehemu watakayoishi wasio wakosefu itaitwaje?

Je, kuna maisha ya milele baada ya hapo?
 
Hahaha..bwana mdogo una mambo kwel kwel..unaonekana huelew a wala b..mana unatapa tapa kwenye andiko lako.
Ebu tuambie umesema mtu akifa anaenda kusubiria siku ya hukumu..kwenye hiyo hukumu baada ya kuhukumiwa mtu huyoo anaenda wapi?
 
ni heri umeliona hilo mkuu
Utampingaje kwa hoja wakati yy mwenyewe hana hoja? Angetoa hoja kwanza yeye kisha tumpinge kwa hoja..jamaa amekuja na shutuma za kihistoria na picha za last sapaaaa tuu..hana analojua mana historia yenyeww kaunga unga
 
Mimi pia nimekuwa nikijiuliza swali hili.Hao kina Lazaro,Binti Yeiro na wengine waliofufuliwa si watupe siri za maisha ya huko baada ya kifo! Waliona nini huko?
Ujue yawezekana hao jamaa hawa kuwa wamekufa kweli bali walizimia tu.Sasa kwa kipindi kile kutofautisha kati ya aliyekufa mazima na aliyezimia yawezekana ilikuwa ngumu.

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Nimeweka kituo hapo uliposema Yesu wa Nazareth ni huyohuyo Issa bin Maryam. Huku historia inaonesha wazi mmoja alizaliwa kwenye holi ya ng'ombe na mwingine chini ya mtende huko mashariki ya kati.
Mzee yesu akuzaliwa kwenye holi ya ng'ombe boss b hakuna maandishi ya biblia yanasema yesu kazaliwa kwenye holi bali biblia inasema aliwekwa kwenye holi ya ng'ombe!! Wapi alizaliwa biblia haijua soma kwa moyo utajua
 
Nadhani Katika habari za Lazaro hapo kifo kimefananishwa na usingizi mzito
Hakuna kesi wala mashauri ndani ya kaburi
Lakini kabla hujazaliwa roho yako ilikuwa wapi?
Roho inarudi kule na siku ambayo utahitajika kwa ufufuo na hukumu au kiama ndiyo roho itarudishwa

Lakini kwa sasa wafu ni kama wako kwenye usingizi mzito usio na ndoto na hakuna kinachoendelea kwao mpaka siku hiyo itakapofika watarudishwa na kumbukumbu zao
 
Nashawishika kukuamini kwa kias flan.
Niulize hivi kweli binadam anaweza kukudhuru kiushirikina?
Je, unaweza kupata pesa kwa ushirikina? Achana na hiz story za freemason au wale wanaoenda kwa mganga wakapewa mashart ya kubana matumiz wakadhan dawa imefanya!
Kuna vitu vingi siviamin had nahis niko peke yang au ni mkorof wa kuamini. Ambacho sikiamini kihalali kabsa huwa ni biblia na quran
 
Hahahahaha wewe ni miongoni mwa wale mliokubali binadam wa kwanz alkuwa Nyani
 
Issa bin Mariam siyo Yesu, acha kueneza uongo.
 
kwan yesu akiwa mweusi inaondoa ukwel kuwa alikua nabii kutoka kwa Mungu?
 
kama tu haujui kabla ya kuzaliwa ulikua wap ? je utajuaje ukifa ukafufuka ulikua wap?msiende mbali kuuliza yalazaro jiulize wewe mwenyewe kabla haujazaliwa ulikua wap? na je huko kulikua na nn ? ukishindwa kutambua hilo jua haujajitambua wewe ni nan upo hapa kwa dhumuni gani na ukitoka hapa unaenda wap , juwa kua unaishi kama kipofu angali unaona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…