Mbona unafoka sana bwashee? Mngetumia usomi wenu kuwaelimisha watu wasiangaike na degree wasomee ujuzi ndio unalipa dunia ya leo.
Kuna mtu ana kozi ya certificate ya miezi minne tu analipwa mshahara wa dollar 50 kwa saa, kwa masaa 10 anakunja dollar 500 kwa siku, huyu ni form leavel aliyejiongeza kozi ya miezi minne mpaka 6 kwenye machine oparating.
Tatizo la wasomi wa Bongo kama mna bifu na watu waliokosa fursa ya kupata elimu ya juu, lakini bado wanao mlango wa kutokea na kuingiza pesa kuliko degree holder.
Mimi kwa exposure niliyonayo leo natamani ningekuwa fundi seremala kuliko taaluma niliyosomea ni ujinga mtupu, shida nyingine wenye taaluma ya useremala hawana connection nilizonazo mimi.
Haya mkuu unayosema ndio mawazo ya ujengaji sasa nasio mtu adharau taaluma za watu kisa baadhi ya watu wanaomzunguka hawana ajira.
Mimi degree yangu ni ya Mechanical Engineering, lakini ni mebase sana kwenye maintenance na ndio imenisaidia kunifikisha hapa nilipo.
Baada ya kumaliza chuo niligundua mapungufu niliyonayo kwenye taaluma yangu nikaenda kujifunza ufundi wa magari garage baada ya miezi 7 ya msoto nikapata kazi kwenye kiwanda Cha muhindi, lakini ajira niliyopata ilitokana na vyeti pamoja na uzoefu huo wa garage, nilipoenda pale niliajiriwa kama Mechanical Engineer lkn kiuhalisia nilikua nafanya kazi nyingi za ufundi hasa kwenye IMB, injection machine,petty machine, pneumatic machine, homogenizer, printing machine, pamoja na labeling machine, kuzifanyia maintenance nikawa kama fundi mkuu pale. Bila vyeti nisingepata nafasi hio Kwa muhindi.
Baada yahapo nilikaa mwaka mmoja nikapata kazi SBL kama maintenance engineer nikawa nafanya kazi vizuri hata miezi 7 haikuisha nikaja hapa nilipo mpaka Sasa na napata mshahara mzuri tu unanzia mil 3 na laki kadhaa. Lakini pia Kuna pesa nje ya mshahara ambazo Kwa mwezi zinaniwezesha kuishi, na nafanya taaluma yangu vizuri na vyeti vya degree ndio vilinifikisha hapa.
Ingawa niliziba mapengo pale penye mapungufu Kwa kujiongeza kutafuta uzoefu wakutumia mikono.
Lakini nimeshuhudia jamaa yangu mmoja akiwa CHEMISTRY IN CHARGE mahala fulani, kafanya kazi miaka sita kaacha na Sasa hivi yupo kwenye useremala ana workshop yake kubwa hapa mjini. Lakini asingeweza pata mtaji kama asingeanza kuajiriwa ili kupata mtaji wakumuwezesha kununua machine mablimbali za kufanyia kazi zake Kwa Sasa.
Kuna jamaa zangu pia nikama brothers walikua wanafanya kazi TBS baada yakupata mtaji wameacha kazi na walianzisha kampuni ambayo Ina kama miaka 5 Kwa Sasa lkn turnover Kwa mwezi nizaid ya mil 100.
Kwahio siwezi dharau elimu suala la msingi mimuhusika mwenyewe anajiongeza vipi kwenye elimu aliyonyo.
Kuna jamaa yangu pia kasoma chemistry alikua anauza madawa(anasambaza kwenye hospital )lkn Sasa hivi kaingia kwenye uzalishaji wa Tambi lishe na anakiwanda chake Wazo ingawa kimeanza operate mwaka huu lkn anapiga hatua nzuri.
Kwahio ni namna ya muhusika mwenyewe kuifanya elimu iwe na manufaa kwake.
Kiufupi elimu hasa degree ni ufunguo wakufungua mageti mengi, lkn baada yakufungua Sasa ndio uliowakuta pale wanatazama huyu aliefungua ndio tunaemuhitaji?. Kama huna vyeti na unaufundi pekee hapa bongo utalipwa kama kibarua mpaka kufa kwako, hutokuja kugusa hata mshahara wa mil 1.
Kwanza waajiri wengi wanaangalia kama unajua kuongea kingereza vizuri na una vyeti vya bachelor, hii inawsaidia Kwenye ukaguzi pindi serikali inapoenda kuwafanyia audition juu ya waajiriwa walionao.
Sasa Kwa mtu alieishia veta ningumu mno kuongea kingereza nahata vyeti huna nani atakaekujari na Akulipe vizuri?, Utaendelea kua fundi mzuri mwenye maslahi duni.
Lakini ukiwa na degree na ukawa waijua kazi yako vizuri kwanza unjiamini, lugha waongea vizuri unapata maslahi mazuri na unaheshimika. Hata unapoanzisha kampuni Yako iwe ya taaluma Yako au nje ya taaluma yako unakua uko vizuri na unjiamini Kwa kile unachokifanya tofauti na watu wengi ambao hawajafika huko.
Assalamu Alleykum.