Wale wenye BSc, BA na degree nyinginezo mnaendeleaje na hali? Matarajio yenu yametimia baada ya kutunukiwa degree hizo?

Wana jamvi kwema,

Leo nimeona niwajulie hali hawa ndugu zetu wenye BSc na BA na degree nyinginezo, vipi maisha yanaendaje baada ya kuhudhurishwa na kutunukiwa Shahada yako.

Vipi mategemeo uliyokuwa nayo, yame kuwa sawa na uhalisia huko duniani? Je, kati ya BSc na BA ipi imesaidia angalau kwenye kujikwamua nje ya ajira, yaani kujiajiri au kutumia ujuzi wako uliopata kutatua changamoto mbalimbali za maisha?

Asamaleko.
Kama unashea changamoto na hao jobless wewe nao ni walewale. Yaani, kama umeme ukikatwa mtaani na wewe unausubiria mpaka urudi ndo suluhu lake na wew.. au basi! Wasalimie kina mchengerwa
 
Ni kweli linawezekana lakini ni very very expensive. Hebu zingatia tangu JPM aanzishe habari za madawati Toshelevu mafanikio yamekuwaje hadi sasa. Mbona bado idadi ya madawati yanayotosheleza haijaweza kufikiwa/ haijakamilika? Hoja ya Elimu bure ipo kisiasa zaidi lakini katika uhalisia wake haipo elimu ya bure. Kwa mfano elimu bure haimaanishi mtoto ale chakula cha mchana shuleni kitakacholetwa na serikali.Hiyo haipo, bali ni lazima mzazi achangie ili mwane ale chakula mchana shuleni. Je, wazazi wenye watoto hapo shuleni wote ni wakulima?
Elimu bure haimaanishi mtoto akiugua akatibiwe bure huko hospitali(ipo tofauti kidogo sana kati ya shule za Day na zile za Boarding lakini at the end of the day Mzazi unawajibika kwa matibabu ya mwanao.
Yapo masuala muhimu ambatishi ambayo ni lazima yawepo ili kumwezesha mwanao aipate hiyo inayoitwa Elimu bure. Ni sharti mwanao aketi darasani (i.e awe na cha kukalia-dawati) ni lazima mwanao ale chakula ni lazima mwanao awekewe ulinzi kwa shule za bweni (mzazi achangie malipo ya mlinzi) n.k. n.k. Hakuna hicho kitu cha BURE 100%.
OK. Kwa sasa hivi Serikali imejitahidi kiasi kwamba walau kila Kata inayo shule ya Sekondari. Huko kwenye mashule ni mara nyingi tunasikia masomo fulani e.g. masomo ya sayansi na mathematics (Biology,Chemistry and Physics ) hayana waalimu i.e. watoto hawafundishwi ipasavyo kutokana na ukosefu wa waalimu. Lakini hapo hapo tunasikia waalimu waliohitimu vyuo, baadhi yao ktk.masomo hayo hayo yanayokosa waalimu, hawajaajiriwa na wala hakuna mpango unaoeleweka wa Serikali kuwaajiri. Kinachojitokeza ni wazazi kujipapasa au kujiongeza zaidi na kutafuta waalimu wa Tuition (ni gharama ya hiari hiyo ujue)
Kwa kifupi hicho kinachopigiwa upatu kwamba ni elimu bure, kimebaki kwenye makabrasha ya Serikali lakini in the real sense hakuna elimu bure kwa upande wa Mzazi. Ni sawa na kusema mzigo umetolewa kichwani na sasa upo mabegani.
Hapo usijidai eti umeutua mzigo. Badooo.
Ss hauoni kama serikali inafanya uzembe yaani walimu wanahitimu alafu kuna upungufu wa walimu mashuleni halafu la pili walimu wanashindwa kusimamia angalau kila mwanafunzi akapata C3 za muhimu kazi kusingizia mazingira mabovu ya shule
 
Haya ndio mawazo mazuri sasa, sio kisa kwao mtu kasoma kakosa ajira anataka aitoe elimu thamani kisa Kuna ndugu yake mwingine ana ahueni ya maisha kuliko waliosoma.
Hamna anaye itoa elimu thamani nimeuliza mnaendeleaje huko duniani, matarajio yametimia kwa kuwa matarajio yako ni ajira tuu ndio maana una panic ila kuwa watu wametoa positive feedback ya mambo, namna walivyo fanikiwa kupitia taaluma zao, wengine biashara na kadhalika.
 
Ss hauoni kama serikali inafanya uzembe yaani walimu wanahitimu alafu kuna upungufu wa walimu mashuleni halafu la pili walimu wanashindwa kusimamia angalau kila mwanafunzi akapata C3 za muhimu kazi kusingizia mazingira mabovu ya shule
Elimu imepungua ubora sana mpaka watu kusoma diploma wanataka D 4 au 5, kwamba imeonekana C ni kubwa sana ni wachache wanaweza kupata form four.
 
Hamna anayetoa elimu thamani nimeuliza mnaendeleaje huko duniani, matarajio yametimia kwa kuwa matarajio yako ni ajira tuu ndio maana una panic ila kuwa watu wametoa positive feedback ya mambo, namna walivyo fanikiwa kupitia taaluma zao, wengine biashara na kadhalika.
Mimi nimekujibu vizuri tu kua matarajio sijayafikia lakini angalau napata chochote kulingana na elimu yangu. Suala kufikia matarajio ni mtambuka huenda ukamuuliza hata GSM/MO/ROSTAM kama kwenye biashara zao wamefikia matarajio wakakujibu bado. Lakini hawezi dharau hatua walizopiga.

Inawezekana matarajio yangu nikuwa nakiwanda Cha bidhaa Fulani kulingana na elimu niliyosoma lkn Leo nikawa bado nipo kwenye ajira kuendelea kutafuta mtaji na maarifa lkn ukiniuliza matarajio yangu nimefikia ntakujibu bado, Sasa unapojibiwa bado unaona kama watu wote matarajio yao ni ajira.

Ndioo maana naamua nikujibu Kwa muktadha huo kama nihizo ajira tunazo Tena sehem ambapo vijana wengi wanatamani waajiriwe na tupo hapa Kwa elimu yetu hio ya degree wewe kwenye comments zako unazosema haina maana.
 
Mimi nimekujibu vizuri tu kua matarajioan sijayafikia lakini angalau napata chochote kulingana na elimu yangu. Suala kufikia matarajio ni mtambuka huenda ukamuuliza hata GSM/MO/ROSTAM kama kwenye biashara zao wamefikia matarajio wakakujibu bado. Lakini hawezi dharau hatua walizopiga.

Inawezekana matarajio yangu nikuwa nakiwanda Cha bidhaa Fulani kulingana na elimu niliyosoma lkn Leo nikawa bado nipo kwenye ajira kuendelea kutafuta mtaji na maarifa lkn ukiniuliza matarajio yangu nimefikia ntakujibu bado, Sasa unapojibiwa bado unaona kama watu wote matarajio yao ni ajira.

Ndioo maana naamua nikujibu Kwa muktadha huo kama nihizo ajira tunazo Tena sehem ambapo vijana wengi wanatamani waajiriwe na tupo hapa Kwa elimu yetu hio ya degree wewe kwenye comments zako unazosema haina maana.
Angalau sasa tuna ongea lugha moja. Hakuna sehemu nimesema elimu haina maana ila nime zungumzia umuhumu wa msomi kujikita kwenye shughuli nyingine za kawaida pia hasa kwa wale ambao hawaja pata ajira ya fani zao walizo somea.
 
Mbona unafoka sana bwashee? Mngetumia usomi wenu kuwaelimisha watu wasiangaike na degree wasomee ujuzi ndio unalipa dunia ya leo.

Kuna mtu ana kozi ya certificate ya miezi minne tu analipwa mshahara wa dollar 50 kwa saa, kwa masaa 10 anakunja dollar 500 kwa siku, huyu ni form leavel aliyejiongeza kozi ya miezi minne mpaka 6 kwenye machine oparating.

Tatizo la wasomi wa Bongo kama mna bifu na watu waliokosa fursa ya kupata elimu ya juu, lakini bado wanao mlango wa kutokea na kuingiza pesa kuliko degree holder.

Mimi kwa exposure niliyonayo leo natamani ningekuwa fundi seremala kuliko taaluma niliyosomea ni ujinga mtupu, shida nyingine wenye taaluma ya useremala hawana connection nilizonazo mimi.
Haya mkuu unayosema ndio mawazo ya ujengaji sasa nasio mtu adharau taaluma za watu kisa baadhi ya watu wanaomzunguka hawana ajira.

Mimi degree yangu ni ya Mechanical Engineering, lakini ni mebase sana kwenye maintenance na ndio imenisaidia kunifikisha hapa nilipo.

Baada ya kumaliza chuo niligundua mapungufu niliyonayo kwenye taaluma yangu nikaenda kujifunza ufundi wa magari garage baada ya miezi 7 ya msoto nikapata kazi kwenye kiwanda Cha muhindi, lakini ajira niliyopata ilitokana na vyeti pamoja na uzoefu huo wa garage, nilipoenda pale niliajiriwa kama Mechanical Engineer lkn kiuhalisia nilikua nafanya kazi nyingi za ufundi hasa kwenye IMB, injection machine,petty machine, pneumatic machine, homogenizer, printing machine, pamoja na labeling machine, kuzifanyia maintenance nikawa kama fundi mkuu pale. Bila vyeti nisingepata nafasi hio Kwa muhindi.

Baada yahapo nilikaa mwaka mmoja nikapata kazi SBL kama maintenance engineer nikawa nafanya kazi vizuri hata miezi 7 haikuisha nikaja hapa nilipo mpaka Sasa na napata mshahara mzuri tu unanzia mil 3 na laki kadhaa. Lakini pia Kuna pesa nje ya mshahara ambazo Kwa mwezi zinaniwezesha kuishi, na nafanya taaluma yangu vizuri na vyeti vya degree ndio vilinifikisha hapa.

Ingawa niliziba mapengo pale penye mapungufu Kwa kujiongeza kutafuta uzoefu wakutumia mikono.

Lakini nimeshuhudia jamaa yangu mmoja akiwa CHEMISTRY IN CHARGE mahala fulani, kafanya kazi miaka sita kaacha na Sasa hivi yupo kwenye useremala ana workshop yake kubwa hapa mjini. Lakini asingeweza pata mtaji kama asingeanza kuajiriwa ili kupata mtaji wakumuwezesha kununua machine mablimbali za kufanyia kazi zake Kwa Sasa.

Kuna jamaa zangu pia nikama brothers walikua wanafanya kazi TBS baada yakupata mtaji wameacha kazi na walianzisha kampuni ambayo Ina kama miaka 5 Kwa Sasa lkn turnover Kwa mwezi nizaid ya mil 100.

Kwahio siwezi dharau elimu suala la msingi mimuhusika mwenyewe anajiongeza vipi kwenye elimu aliyonyo.

Kuna jamaa yangu pia kasoma chemistry alikua anauza madawa(anasambaza kwenye hospital )lkn Sasa hivi kaingia kwenye uzalishaji wa Tambi lishe na anakiwanda chake Wazo ingawa kimeanza operate mwaka huu lkn anapiga hatua nzuri.

Kwahio ni namna ya muhusika mwenyewe kuifanya elimu iwe na manufaa kwake.

Kiufupi elimu hasa degree ni ufunguo wakufungua mageti mengi, lkn baada yakufungua Sasa ndio uliowakuta pale wanatazama huyu aliefungua ndio tunaemuhitaji?. Kama huna vyeti na unaufundi pekee hapa bongo utalipwa kama kibarua mpaka kufa kwako, hutokuja kugusa hata mshahara wa mil 1.

Kwanza waajiri wengi wanaangalia kama unajua kuongea kingereza vizuri na una vyeti vya bachelor, hii inawsaidia Kwenye ukaguzi pindi serikali inapoenda kuwafanyia audition juu ya waajiriwa walionao.

Sasa Kwa mtu alieishia veta ningumu mno kuongea kingereza nahata vyeti huna nani atakaekujari na Akulipe vizuri?, Utaendelea kua fundi mzuri mwenye maslahi duni.

Lakini ukiwa na degree na ukawa waijua kazi yako vizuri kwanza unjiamini, lugha waongea vizuri unapata maslahi mazuri na unaheshimika. Hata unapoanzisha kampuni Yako iwe ya taaluma Yako au nje ya taaluma yako unakua uko vizuri na unjiamini Kwa kile unachokifanya tofauti na watu wengi ambao hawajafika huko.

Assalamu Alleykum.
 
Ss hauoni kama serikali inafanya uzembe yaani walimu wanahitimu alafu kuna upungufu wa walimu mashuleni halafu la pili walimu wanashindwa kusimamia angalau kila mwanafunzi akapata C3 za muhimu kazi kusingizia mazingira mabovu ya shule
Serikali (wizara ya Elimu..)haijafanya uzembe kwani ili Serikali iweze kuajiri ni lazima kufuata utaratibu unaokubalika. Utaratibu wa kuajiri ni Mchakato mrefu (long Process ) kwamba Wizara ya Elimu ikitaka kuajiri ni lazima iombe kibali kwa kuzingatia yale maombi ya ajira yaliyotoka ngazi za chini maWilayani. Na hapo ndo utaikuta TAMISEMI halafu yakijumlishwa kwa pamoja yanafikishwa Serikali kuu i.e. Wizara ya Elimu sayansi.... Hayo mahitaji yataingizwa katika Budget itakayosomwa Bungeni na kama bajeti hiyo yenye mambo mengi mengineyo-sio ajira tuu; itapata ridhaa ya Bunge, ndipo hazina watapewa maelekezo kutoka kwa Katibu mkuu kwa utoaji wa mafungu(Release of funds). Hapo usisahau kwamba yapo makandokando yanayoweza kuathiri bajeti hata kama ilipitishwa bungeni e.g. ongezeko la gharama au kupungua kwa thamani ya shilingi ya Tanzania, kupanda kwa bei za mafuta(Petrol) n.k. kiasi kwamba kile kilichopangwa wakati ule na kutengewa mafungu, mafungu hayo kwa sasa (current situation) hayatoshelezi tena. Kwa mantiki hiyo kama kulikuwa na kuajiri waalimu 10 sasa wataajiriwa e.g. sita.Kati ya waajiriwa hao sita ni lazima kubalance Arts na Science subjects. Kwa kifupi ni shughuli pevu aisee sio eti ni Uzembe wa Serikali. Serikali yenyewe inatekeleza Utoaji wa Huduma kwa wananchi kwa Kutumia makusanyo ya Kodi . Hapo Sasa ina maana kama Serikali isipokusanya kadi ya kutosha zoezi zima litakwama kwa kukosa fedha ya utekelezaji. Halafu wananchi wenyewe ndo hao wanaona Kodi(TOZO) ni mojawapo ya Kero. Sasa Serikali ifanyeje? Fedha za Mikopo ni marufuku kabisa kuzitumia kwa ajili ya kugharamia Huduma. Huduma za kijamii hugharamiwa kutoka mafungu ya Own sources yaani Makusanyo ya Ndani (TOZO) Hii ndo vijana wanaita Maokoto.
Serikali imejitahidi sana kudhibiti wizi na ukwepaji kulipa kodi kwa kuanzisha mfumo wa kutumia mashine za EFD lakini wapi bhana; bado walipa kodi wanakwepa japokuwa sio wengi sana.
 
Mbona unafoka sana bwashee? Mngetumia usomi wenu kuwaelimisha watu wasiangaike na degree wasomee ujuzi ndio unalipa dunia ya leo.

Kuna mtu ana kozi ya certificate ya miezi minne tu analipwa mshahara wa dollar 50 kwa saa, kwa masaa 10 anakunja dollar 500 kwa siku, huyu ni form leavel aliyejiongeza kozi ya miezi minne mpaka 6 kwenye machine oparating.

Tatizo la wasomi wa Bongo kama mna bifu na watu waliokosa fursa ya kupata elimu ya juu, lakini bado wanao mlango wa kutokea na kuingiza pesa kuliko degree holder.

Mimi kwa exposure niliyonayo leo natamani ningekuwa fundi seremala kuliko taaluma niliyosomea ni ujinga mtupu, shida nyingine wenye taaluma ya useremala hawana connection nilizonazo mimi.
Ni kweli bro kuna watu wenye certificate zao wanapiga pesa kwa sababu ya skills zao, skills haimtupi mtu. Pamoja na degree ni muhimu kujiongezee ujuzi tofauti tofauti.
 
Haya mkuu unayosema ndio mawazo ya ujengaji sasa nasio mtu adharau taaluma za watu kisa baadhi ya watu wanaomzunguka hawana ajira.

Mimi degree yangu ni ya Mechanical Engineering, lakini ni mebase sana kwenye maintenance na ndio imenisaidia kunifikisha hapa nilipo.

Baada ya kumaliza chuo niligundua mapungufu niliyonayo kwenye taaluma yangu nikaenda kujifunza ufundi wa magari garage baada ya miezi 7 ya msoto nikapata kazi kwenye kiwanda Cha muhindi, lakini ajira niliyopata ilitokana na vyeti pamoja na uzoefu huo wa garage, nilipoenda pale niliajiriwa kama Mechanical Engineer lkn kiuhalisia nilikua nafanya kazi nyingi za ufundi hasa kwenye IMB, injection machine,petty machine, pneumatic machine, homogenizer, printing machine, pamoja na labeling machine, kuzifanyia maintenance nikawa kama fundi mkuu pale. Bila vyeti nisingepata nafasi hio Kwa muhindi.

Baada yahapo nilikaa mwaka mmoja nikapata kazi SBL kama maintenance engineer nikawa nafanya kazi vizuri hata miezi 7 haikuisha nikaja hapa nilipo mpaka Sasa na napata mshahara mzuri tu unanzia mil 3 na laki kadhaa. Lakini pia Kuna pesa nje ya mshahara ambazo Kwa mwezi zinaniwezesha kuishi, na nafanya taaluma yangu vizuri na vyeti vya degree ndio vilinifikisha hapa.

Ingawa niliziba mapengo pale penye mapungufu Kwa kujiongeza kutafuta uzoefu wakutumia mikono.

Lakini nimeshuhudia jamaa yangu mmoja akiwa CHEMISTRY IN CHARGE mahala fulani, kafanya kazi miaka sita kaacha na Sasa hivi yupo kwenye useremala ana workshop yake kubwa hapa mjini. Lakini asingeweza pata mtaji kama asingeanza kuajiriwa ili kupata mtaji wakumuwezesha kununua machine mablimbali za kufanyia kazi zake Kwa Sasa.

Kuna jamaa zangu pia nikama brothers walikua wanafanya kazi TBS baada yakupata mtaji wameacha kazi na walianzisha kampuni ambayo Ina kama miaka 5 Kwa Sasa lkn turnover Kwa mwezi nizaid ya mil 100.

Kwahio siwezi dharau elimu suala la msingi mimuhusika mwenyewe anajiongeza vipi kwenye elimu aliyonyo.

Kuna jamaa yangu pia kasoma chemistry alikua anauza madawa(anasambaza kwenye hospital )lkn Sasa hivi kaingia kwenye uzalishaji wa Tambi lishe na anakiwanda chake Wazo ingawa kimeanza operate mwaka huu lkn anapiga hatua nzuri.

Kwahio ni namna ya muhusika mwenyewe kuifanya elimu iwe na manufaa kwake.

Kiufupi elimu hasa degree ni ufunguo wakufungua mageti mengi, lkn baada yakufungua Sasa ndio uliowakuta pale wanatazama huyu aliefungua ndio tunaemuhitaji?. Kama huna vyeti na unaufundi pekee hapa bongo utalipwa kama kibarua mpaka kufa kwako, hutokuja kugusa hata mshahara wa mil 1.

Kwanza waajiri wengi wanaangalia kama unajua kuongea kingereza vizuri na una vyeti vya bachelor, hii inawsaidia Kwenye ukaguzi pindi serikali inapoenda kuwafanyia audition juu ya waajiriwa walionao.

Sasa Kwa mtu alieishia veta ningumu mno kuongea kingereza nahata vyeti huna nani atakaekujari na Akulipe vizuri?, Utaendelea kua fundi mzuri mwenye maslahi duni.

Lakini ukiwa na degree na ukawa waijua kazi yako vizuri kwanza unjiamini, lugha waongea vizuri unapata maslahi mazuri na unaheshimika. Hata unapoanzisha kampuni Yako iwe ya taaluma Yako au nje ya taaluma yako unakua uko vizuri na unjiamini Kwa kile unachokifanya tofauti na watu wengi ambao hawajafika huko.

Assalamu Alleykum.
Hapa nashauri madereva wajiongeze wakasome mashine oparating, kama bulldozer, scavetar, folk lift etc hizi kazi hata Bongo zinalipa na unalipwa kwa masaa.

Kwa sisi tulioukataa mfumo wa ajira za kibongo hizo field, za machine oparating, mechanics na carpenter zinalipa vizuri sana per hour mamtoni.

Kuna locomotive oparating hii kwa mtu anayeangalia fursa nchi za mbele ni bonge la goli, ndio utashangaa kuna mtu ameishinulaya muda mfupi lakini mambo aliyofanya Bongo ni makubwa.

Watu wajifunze skills watoke wakatafute maisha nje ya Bongo fursa ziko njenje zinahitaji nguvu kazi.

Wasomi wetu wengi wakiwa vyuoni wanawaza wakigraduate waje kupata kazi maofisi wavae tai na usafiri tako la nyani wengi ndio wanapotea hapo.

Meneja Wa Makampuni kawajazia link kibao humu za full funded skolaship lakini hakuna anayeomba vijana wamejaza kwenye kula tunda kimasihara.
 
Imani yangu nikua ukiwa na degree/diploma/certificate ukashindwa kuitumia bongo na ukashindwa kutoboa ningumu sana nchi nyingine. Kwangu Bongo Kuna furusa kibao.
 
Hizi degree zenu za Bongo wala hazitambuliki kwanza, mimi naongelea watu wenye ujuzi wazungu wala hawaitaji vyeti, wanataka ujuzi wako tu.
 
Back
Top Bottom