Wale wenye waume waliowatia mimba binti zao wa kazi mje tushauriane

Wale wenye waume waliowatia mimba binti zao wa kazi mje tushauriane

Mtu ufanye ujinga wote, lakini kumlala binti wa kazi, hapana aisee. Anakusaidia kulea watoto, anakuangalizia nyumba mkiwa hampo, anapika, anafua na jinsi tunavyoishi nao ni kama watoto/wadogo zetu. Binafsi nipo against na hii kitu, tafuta mwanamke mwingine huko sio ndani ya nyumba.
Hata mimi naona kama ni unyanyasaji , maana unaweza kuta wanakataa, ila wanakuwa waoga
 
Baada tu ya Miezi 6 ndani ya ndoa nilisafiri kwa wiki 2 . Niliporudi mume kansmbia nimpe nauli hg arudi kwao ufanisi umeshuka. Badae nikaambiwa namajirani kuwa hg yu mjamzito
Wa pili pia nilisafiri na watatu vilevile. Na wote hao nilipomuuliza mr alikubali kuwa ni kweli.
Du! watu muna moyo. Yaani bado upo tu unavumilia aje na wa nne.
 
Miaka kumi watatu, ikifika miaka 20 idadi itakuwa kubwa zaidi.

Kinachofuata ni maradhi maana mumeo hatumii kinga.

Yafuatayo huenda yakatia aibu zaidi.

Ongea naye.
Mie kidume lakini nyie wanawake mnatia ujinga mwingi sana. Sasa aongee nae ninj hapo? Ni kuchukua kilichochako na kusepa end of story.
 
Ushauri wako si wa kujenga. Kuolewa au kuoa ni haki ya kila mwanamke na mwanaume. Pia we wajua mahitaji ya mwili ni pamoja na hilo.
Huwezi amini kama kuna mtu anaishi bila kinyongo na mwanamke au mtu yeyote duniani ni mimi. Na ndo maana hadi leo nipo na mume wangu na ninaamini ananipenda sanaaa tu. Haya nimeyaweka huku ili kupata maoni ya wengine tu.
Watoto wangu nipo nao karibu sana na haya yanayotokea kwa ma hg wala hawayajui. Huwa tunayamaliza na baba yao faraghani sana. Watoto wapo vizuri sana maana wanapata upendo wa baba na mama.
Kwa taarifa yako nyumba yangu au maisha ninayoishi mimi na familia yangu ni ya amani na furaha kiasi kwamba majirani na watu kutoka sehemu zingine na ndugu zetu wengine wanakuja kuomba ushauri.
Wewe kweli ni wife material
 
Asante mbona nishakoma kitambo. Ila na wao wamekoma maana wanakomaaga na mimba zao na kulea watoto wao bila usaidizi. Sijawahi kuonana nao tangu niwafukuze kwangu, wanapambana huko vijijini
Pamoja na hayo, Sheria inasema Wanastahili Urithi. Hakuna mwanaharamu mbele ya Sheria bali wazazi haramu.
 
Back
Top Bottom